Upokeaji wa Teknolojia na Mtizamo wa Mkulima: Mwenendo wa Warsha ya Pili ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika Katika Chuo cha Ufundi, Mikumi (VETA) 11-13 Juni 2001

Loading...
Thumbnail Image

Date

2001

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

TARP II-SUA Project

Abstract

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway, kinatekeleza mradi huu wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Matokeo yanayotarajiwa yako makuu matano, nayo ni: 1. Matokeo ya tafiti za kilimo zinazolenga matatizo ya wakulima wadogowadogo. 2. Kuimarishwa kwa uhusiano kati ya wakulima, watafiti na washauri wa wakulima. 3. Wahitimu 32 wa Wizara ya Kilimo wenye shahada zajuu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. 4. Rasimu ya mapendekezo kwa Serikali na wahisani juu ya mfumo endelevu wa ' kugharamia shughuli za utafiti wa kilimo. 5. Tathmini ya mabadiliko yatokanayo na tafiti zilizokwishafanyika na zinazofanyika sasa. Kwa hiyo kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo. 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo. 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi. 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha Mwenendo wa Warsha ya pili ya ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki kuhusu Upokeaji wa Teknnolojia na Mtizamo wa Mkulima, iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi, Mikumi (VETA) tarehe 11 - 13 Juni 2001. Japo warsha iliendeshwa kwa Kiswahili, Mwenendo wa Warsha umechapishwa na kutolewa kwa Kiswahili na kwa Kiingereza.

Description

Keywords

Tekinolojia, Wakulima

Citation

Collections