Upokeaji wa Teknolojia na Mtizamo wa Mkulima: Mwenendo wa Warsha ya Pili ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika Katika Chuo cha Ufundi, Mikumi (VETA) 11-13 Juni 2001

dc.contributor.authorMtenga, N
dc.date.accessioned2020-10-07T06:20:26Z
dc.date.available2020-10-07T06:20:26Z
dc.date.issued2001
dc.description.abstractChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway, kinatekeleza mradi huu wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Matokeo yanayotarajiwa yako makuu matano, nayo ni: 1. Matokeo ya tafiti za kilimo zinazolenga matatizo ya wakulima wadogowadogo. 2. Kuimarishwa kwa uhusiano kati ya wakulima, watafiti na washauri wa wakulima. 3. Wahitimu 32 wa Wizara ya Kilimo wenye shahada zajuu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. 4. Rasimu ya mapendekezo kwa Serikali na wahisani juu ya mfumo endelevu wa ' kugharamia shughuli za utafiti wa kilimo. 5. Tathmini ya mabadiliko yatokanayo na tafiti zilizokwishafanyika na zinazofanyika sasa. Kwa hiyo kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo. 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo. 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi. 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha Mwenendo wa Warsha ya pili ya ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki kuhusu Upokeaji wa Teknnolojia na Mtizamo wa Mkulima, iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi, Mikumi (VETA) tarehe 11 - 13 Juni 2001. Japo warsha iliendeshwa kwa Kiswahili, Mwenendo wa Warsha umechapishwa na kutolewa kwa Kiswahili na kwa Kiingereza.en_US
dc.identifier.isbn9987 605 38 9
dc.identifier.urihttp://10.10.11.5/handle/123456789/510
dc.language.isootheren_US
dc.publisherTARP II-SUA Projecten_US
dc.relation.ispartofseries;TS 2-24
dc.subjectTekinolojiaen_US
dc.subjectWakulimaen_US
dc.titleUpokeaji wa Teknolojia na Mtizamo wa Mkulima: Mwenendo wa Warsha ya Pili ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika Katika Chuo cha Ufundi, Mikumi (VETA) 11-13 Juni 2001en_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Upokeaji wa Teknolojia Mtazamo wa Mkulima Kanda ya Mashsriki0001.pdf
Size:
26.41 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:

Collections