Chakula cha GMO
Loading...
Files
Date
2022-10-04
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Shirika la chakula duniani
Abstract
Pengine umesikia kuhusu uhandisi jeni wa vyakula (GMO) na unaweza ukawa unajiuliza inahusu nini, hapa tunakueleza.
Kenya wiki hii imeidhinisha kilimo na uingizaji wa mazao na vyakula vilivyobadilishwa vinasaba, (GMO) na hivyo kumaliza marufuku ya muongo mmoja iliyokuwa imewekwa kutokana na hofu ya kiafya. Inakuja wakati nchi inakabiliwa na ukame mbaya.
Ukame mbaya zaidi katika miaka 40 umeacha mamilioni ya watu wakikabiliwa na njaa. Serikali ya Rais William Ruto imegeukia mimea iliyobadilishwa vinasaba kama njia ya kusaidia kuongeza mavuno. Inasema nchi inahitaji mbegu zinazostahimili ukame, wadudu na magonjwa.
Muongo mmoja uliopita uzalishaji na uagizaji wa mazao ya GM ulipigwa marufuku kwa sababu ya wasiwasi juu ya hatari zinazowezekana za kiafya. Kwa wazi ulikuwa uamuzi usiopendwa na Amerika, ambayo ni nyumbani kwa wazalishaji wakuu wa mbegu zilizotengenezwa kwa vinasaba.
Description
Jarida
Keywords
Chakula, G.M.O, Vinasaba