Misitu na Nyuki
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Misitu na Nyuki by Author "Bakari, A"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za Uharibifu wa Mazingira Katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya - Warsha ya Saba ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki lIiyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003(TARP II-SUA Project, 2004) Bakari, A; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. . Chapisho hili Iinawasilisha mwenendo wa Warsha ya saba ya Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhusu Athari za Uharibifu wa Mazingira katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya iliyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima, watafiti na wataalamu wa ugani ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo.