Misitu na Nyuki
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Misitu na Nyuki by Title
Now showing 1 - 20 of 45
Results Per Page
Sort Options
Item Asali na faida zake(Sokoine university of agriculture, 2022-12-22)Ikiwa ni tamu kuliko sukari, je asali, ni kimiminika asilia kinachochukua nafasi ya sukari? Mtaalamu wa lishe Jo Lewin anaainisha faida za kiafya na madhara ya asali. Asali hutengenezwa na nyuki. Hutokana na mkusanyiko wa vimiminika vyenye sukari nyingi itokayo kwenye mimea ya maua. Huhifadhiwa katika sega la asali ili kutoa chakula kwa nyuki.Item Athari za Uharibifu wa Mazingira Katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya - Warsha ya Saba ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki lIiyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003(TARP II-SUA Project, 2004) Bakari, A; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. . Chapisho hili Iinawasilisha mwenendo wa Warsha ya saba ya Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhusu Athari za Uharibifu wa Mazingira katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya iliyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima, watafiti na wataalamu wa ugani ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo.Item Controlling the -4 Greater Wax Moth(United States Department of Agriculture, 1981-01-23)The greater wax moth is also known as the bee moth, the bee miller, the wax miller, and the web worm. In its larval stages, it damages combs and honey and is responsible for large losses to bee keepers in the United States. This insect is found almost everywhere that bees are raised. Its greatest damage is done in the Southern States, where its season of activity. is longest.Item Fahamu Umuhimu Wa Ndege Kama Kiashiria Cha Hali Ya Mifumo Ya Ikologia Katika Maeneo Mbali Mbali(Sokoine university of agriculture, 2021-07-08) Mrosso, Hillary ThomasKiashiria ni alama ambayo inatoa taarifa au tahadhari juu jambo fulani zuri au baya na kukufanya uweze kuchukua hatua mapema. Katika uhifadhi au sayansi ya wanyamapori kiashiria ni biolojia ya viumbe ambayo hutumia kuwepo au kutokuwepo kwao katika ikolojia au mazingira Fulani kama kipimo cha afya, ubora au mabadiliko. Wanyama jamii ya amphibia na reptilia wanaweza kutumika kupima mabadiliko ya hali ya hewa kama , ukame, uchafuzi wa mazingira na kuharibika au kusitawi kwa ikolojia, nk.Item Grevillia - Silky oak (Grevillia robusta)(Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii - SUA, 2017-07)Kipeperushi kilicho na maelezo kwa ufupi juu ya miti ya Grevillia kuanzia upandaji, utunzaji na matumizi ya miti hiyo.Item Improved Tree seed Production Manual(Ministry of Natural Resources and Tourism - Forestry and Bee keeping Division, United Republic of Tanzania, 2020-11) Komakech, C; Nshubemuki, L; Swai, R. L; Kasase, A. SPlantation forestry resources are managed for the production of both timber and non-timber forestry products (NTFPs). The quality of these end-products is determined by both the quality of the germplasm used in the initial establishment of the plantations and the management practices applied to the planted trees. Broadly, two types of planting materials are used to establish plantations: seeds (sexual reproduction) and vegetative material (asexual reproduction). Regardless of which type of germplasm is used, however, various tree breeding operations need to be followed the planted forestry resources are to see sustainable improvements in both growth and wood quality. The development of tree breeding activity guidelines can help stakeholders involved in establishing research infrastructures apply standardised procedures which will guarantee that they meet their research objectives.Item Jarida la mbinu bora(Echo community, 2011) Kinsey, ErwinUfugaji wa mifugo kiasili ni mfumo wa maisha ambao watu au jamii husika wanaishi maisha yao kwa kutegemea mifugo. Katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, wafugaji hawa hutegemea zaidi mifugo ya aiana mbali mbali kama; ng’ombe, kondoo, mbuzi, punda, na ngamia ili kukimu maisha yao na familia zao. Mifugo iliyotajwa, imeorodheshwa kwa kigezo cha kuanzia na lile kundi ambalo sio stahimilivu sana (ng’ombe) na kumalizia na lililo stahimilivu zaidi (punda na ngamia), pia kwa kuzingatia maeneo ya ufugaji kuanzia na yaliyo makame kiasi hadi makame zaidi. Wafugaji hawa wana mchango mkubwa sana katika sekta/idara husika lakini bado hawajaweza kuthaminiwa ipasavyo. Kwa mfano: uwezo wa kutunza/ kuendeleza kizazi cha ng’ombe wa asili. Katika utunzaji wa mifugo yao, wafugaji hawa wana uwezo wa kipekee wa kutumia maeneo yanayokabiliwa na ukame kwa njia ya kuhama hama kwa ajili ya kupata malisho bora na maji. Ni ukweli usiopingika kwamba, katika/ ukanda wa Afrika ya mashariki maeneo ya hifadhi nyingi tunazozifurahia kwa sasa ni matokeo ya wafugaji kuhamahama na kuweza kuyatunza maeneo haya kwa ajili ya malisho na hasa kuweza kuyalinda/kuzuia yasiingiliwe na shughuli za kilimo.Item Jarida la TAFORI(Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), 2019-06-15) TANZANIA FORESTRY RESEARCH INSTITUTION (TAFORI)Siku ya nyuki duniani ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza viumbe wanaochavusha mimea hususan nyuki, kutambua madhara ambayo yanakabili viumbe hao na kujua mchango wake kwa maendeleo endelevu. Nyuki ni mdudu muhimu sana katika mfumo ikolojia na maisha ya mwanadamu, kwani huchavusha asilimia 70 ya mimea inayohudumia asilimia 90 ya watu duniani. Nyuki wana mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu, hivyo jamii inatakiwa kuwatunza. Kwa kutambua umuhimu wa nyuki, Baraza la Umoja wa Mataifa (“The United Nations General Assembly”) lilipitisha azimio kuwa kila tarehe 20 Mei iwe Siku ya Nyuki Duniani. Azimio hilo liliridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuatia pendekezo la Solvenia la Desemba 2017 la kuifanya tarehe 20 Mei kuwa siku ya nyuki duniani. Chimbuko la siku ya nyuki duniani lilitokana na Bwana Anton Jansa aliyezaliwa siku ya tarehe 20/5/1734. Bwana Anton alikuwa mwalimu na mwasisi wa ufugaji nyuki duniani. Alifafanya ufugaji wa nyuki kitaalamu, aliandika vitabu na kufundisha ufugaji nyuki nchini Slovania. Bwana Anton aliwathamini sana nyuki na moja ya kati ya vitabu vyake alivyoandika ni“Bees are a type of fly, hardworking, created by God to provide man with all honey and wax” maana yake nyuki ni wadudu wachapakazi walioumbwa na Mungu kumpatia mwanadamu mahitaji yake yote ya asali na nta. Hivyo, sherehe za kuadhimisha siku ya nyuki duniani hufanyika kila mwaka tarehe 20 Mei kwa heshima ya Bwana Anton JansaItem Kijarida cha mradi wakuongeza dhamani ya milima katika misitu ya Tao la mashariki(Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania, 2016-03) Shirika la kuhifadhi misitu ya asili TanzaniaIli lengo la mradi la kusaidia vijiji kutekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Jamii litimie, Mradi unaendelea kupanua elimu na kusaidia vijiji vingine 2 (Ndole na Magunga) kuanzisha misitu ya Hifadhi ya Kijiji na pia kijiji kingine cha Diburuma kilipata elimu na uamasishwaji wa usimamizi wa misitu ya jamii. Sheria ya msitu ya mwaka 2002 inatoa fursa nyingi kwa jamii kusimamia na kulinda misitu Sheria inasema kuwa miongoni mwa malengo yake makuu ni kuwapa wajibu na haki ya kusimamia misitu wananchi ndani na kandokando ya misitu Wanajamii walielimishwa kwamba wakiweza kutunza misitu yao watapata motisha kama: ❖ Kubaki na 100% ya mapato yatokanayo na mauzo ya mazao ya misitu. ❖ Kubaki na tozo na faini. Faini inayotozwa katika ardhi ya kijiji kutokana na Misitu ya Hifadhi ya Kijiji au Misitu ya jamii inabaki kijijini ili mradi imeelezwa kwenye sheria ndogo za kijiji. ❖ Utaifishaji wa mazao ya misitu na vifaa kutokana na uvunaji haramu. ❖ Wanaweza kufanya uvunaji endelevu wa mazao ya misitu ili mradi imeelezewa kwenye mpango wa uvunaji wa kijiji Baada ya kuelimishwa wanavijiji wa vijiji vya Ndole, Diburuma na Magunga walianza mchakato wa kusimamia Misitu ya Hifadhi yaVijiji.Vijiji vyote vitatu viliunda kamati ya maliasili ya kijiji yenye wajumbe 12 ikijumuisha wanaume na wanawake. Vijiji vya Magunga na Ndole walifanikiwa kutenga maeneo ya Misitu. Ndole hekta 1,238.81 na Magunga hekta 1,277.3, pia waliandaa mpango wa usimamizi wa misitu, sheria ndogo na kuidhinishwa na Mkutano mkuu wa kijiji na kupelekwa kwenye Halmashauri ya Wilaya kwa idhini na kwaajili ya kusajiliwa kwenye daftari la usajili wa misitu ya vijiji. Hii inapelekea kufanya jumla ya hekta 10,131.22 kwa vijiji 8 (Bwage, Mziha, Difinga, Msolokelo, Masimba, Makuyu Magunga na Ndole) ambavyo vinatekeleza Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Jamii na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa kijiji. Kwa kipindi cha mwaka 2015 mpango wa usimamizi wa misitu na sheria ndogo za vijiji 3 (Makuyu, Msolokelo na Masimba) zimeidhinishwa na Halmashauri yaWilaya ya Mvomero na kusajiliwa kwenye daftari la usajili wa misitu ya vijiji.Item Maswali mbalimbali yanayoulizwa na wafugaji wa nyuki vijijini(Idara ya Biolojia ya Misitu, Sokoine University of Agriculture - SUA, 2013) Msalilwa, JNYUKI NI NINI? Nyuki ni wadudu wadogo wenye uwezo wa kuruka na hutengeneza vyakula vyao wenyewe kutokana na maji matamu yanayopatikana kwenye maua ya miti na ungaunga unaopatikana katika maua. Wadudu hawa wanauwezo wa kuziba matundu yanayojitokeza kwenye viota vyao kwa kutumia utomvu wa miti. Wadudu hawa ni wasafi sana hawapendi kuishi mahali palipo na harufu ya uozo wa kitu, ukungu, au maji maji (unyevu nyevu).Item Mazao ya nyuki: Sifa, usindikaji na uuzaji(CTA, 2010) Mutsaers, Marieke; Blitterswijk, Henk van; ’t Leven, Leen van; Kerkvliet, Jaap; Waerdt, Jan van deKitabu kinachoelezea ufugaji nyuki na mazao yanayopatikana kutokana na ufugaji huo na jinsi ya kuyaendeleza hadi kufikia hatua ya uuzaji na kujipatia faida.Item Mgomalizi, Mdodoma(Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii - SUA, 2017)Kipeperushi kinachoelezea upandaji, utunzaji na matumizi ya miti ya Mgomalizi au MdodomaItem Mifumo endelevu ya nishati ya miti (mkaa na kuni) Tanzania : mwongozo wa mafunzo ya awali(WORLD AGROFORESTRY CENTRE, 2018-10-09) TAREANishati ya miti (mkaa na kuni) ni aina ya nishati inayotumika zaidi kwenye kupikia na kwenye kuota moto kusini mwa Jangwa la Sahara na hutumika kwenye biashara ndogo ndogo kama migahawa, uokaji, biashara za mamantilie, utengenezaji wa matofali, pamoja na ukaushaji wa mazao kama chai na tumbaku. Zaidi ya 90% ya wakazi kusini mwa Jangwa la Sahara inategemea ama kuni au mkaa. Nishati ya miti huchangia yapata 90% ya nishati ya miti nchini Tanzania. Mkaa unatumika zaidi mijini wakati kuni hutumika zaidi vijijini. Yapata 70% ya kaya za mijini hutegemea mkaa. Afrika huzalisha 62% ya mkaa wote duniani ambao unakisiwa kufikia tani milioni 52. Tanzania inashika nafasi ya saba kwa uzalishaji wa mkaa duniani, ikichangia kama 3% ya uzalishaji wa mkaa wote duniani, kwa kiasi cha zaidi ya tani 1.6.Item Misitu na hifadhi ya Mazingira(Tanzania Educational publishers L.T.D, 2002) Ngara, LulengeItem Miti ya matunda kwa hifadhi ya mazingira na stahamili ya mabadiliko ya tabia nchi(Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme, 2012-03) Kusolwa, Paul M; Mghembe, E. R; Mwaitulo, SKilimo ni uti wa mgongo wa mkulima vijijini. Kulingana na kukua kwa familia, kupungua kwa rutuba na mabadiliko ya mahitaji ya wakulima vijijini wakulima wameendelea kufungua mashamba mapya ili kuongeza mavuno na kipato. Upanuzi huu wa mashamba mara nyingi huambatana na kukatwa kwa miti au misitu. Hali hii inaleta ukame na ongezeko la joto katika maeneo husika. Ukataji wa miti kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa mashamba ya mazao hasa ya chakula yanahusishwa na dalili kubwa za mabadiliko ya tabia nchi. Jitihada nyingi zimefanyika ili kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira kwa kampeni za kupanda miti na kuhamasisha wananchi kutokata miti bila kupanda mti. Hata hivyo mwongozo huu, mara nyingi hulenga miti ya misitu peke yake. Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa mbinu za ustawishaji wa miti ya matunda kama njia nyingine ya kuhifadhi mazingira na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi. Kulingana na tafiti zilizofanyika juu ya miti ya misitu, inatarajiwa kwamba miti ya matunda pia itasaidia kupungua hewa ya ukaa, kupunguza ongezeko la joto, na kuboresha mkusanyiko wa mawingu ya mvua, kuimarisha utunzaji wa maji aridhini katika maeneo ya mashambani. Zaidi ya yote, mit ya matunda itasaidia kuongeza uhakika wa chakula na kipato cha kaya vijijini. Kwa kuwa miti ya matunda itakuwa na thamani kubwa kwa familia, hivyo si rahisi kukatwa kwa matumizi mengine (kama vile kuni au mkaa). Hivyo basi elimu ya uzalishaji wa miche na utunzaji mzuri wa bustani za matunda ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya uoto wa kijani, kuhifadhi ardhi na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi. Kitabu hiki kinatoa maelezo ya mbinu bora za uzalishaji wa miche na ustawishaji wa Miparachichi, Miembe, na Michunga. Chimbuko la kazi hii ni moja ya miradi inaloyenga utekelezaji wa shughuli za mpango mpya unaohusu hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change Impacts Adaptation and Mitigation - CCIAM).Item Mitiki - Teak(Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii - SUA, 2017)Kipeperushi kinachoelezea upandaji na utunzaji wa miti ya mitikiItem Mkangazi(Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii - SUA, 2017)Kipeperushi kinachoelezea upandaji na utunzaji wa miti ya MkangaziItem Mkaratusi(Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii - SUA, 2017)Kipeperushi kinachoelezea utuzanji na upandaji wa miti ya mikaratusiItem Mkongo(Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii - SUA, 2017)Kipeperushi kinachoelezea upandandaji, utunzaji na matumizi ya miti ya mkongoItem Muongozo wa utunzaji bora wa mashamba ya miti ya wananchi(Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme - CCIAM, 2012-01) Malimbwi, Rogers E; Zahabu, Eliakimu; Katani, Josiah; Mugasha, Wilson; Mwembe, UhuruUpandaji wa miti nchini Tanzania umekuwa ukisisitizwa kwa miongo kadhaa lakini kukubalika kwa shughuli hizi kumekuwa hakuridhishi. Tofauti na watu wa sehemu nyingine za nchi, watu wa Wilaya ya Makete wamehamasika kupanda miti kutokana na hali mbaya ya hewa na ukosefu wa rutuba kwenye udongo sababu ambazo zilisababisha mazao duni ya kilimo. Pia kwa muda mrefu, wananchi wa Wilaya ya Makete wameshajua umuhimu wa miti kwa kuwa kwa kiasi kikubwa mauzo ya miti na mbao yanachangia kipato cha wakulima. Kabla ya kujikita kwenye kilimo cha miti, kipato cha wananchi wa Wilaya ya Makete kilitegemea zaidi mazao ya kilimo kama vile mahindi, ngano, mchele, viazi miviringo na pareto. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, uzalishaji wa mazao hayo umepungua kwa kiasi kikubwa na wakati mwingine kusababisha tishio la njaa.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »