Misitu na Nyuki
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Misitu na Nyuki by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 45
Results Per Page
Sort Options
Item Controlling the -4 Greater Wax Moth(United States Department of Agriculture, 1981-01-23)The greater wax moth is also known as the bee moth, the bee miller, the wax miller, and the web worm. In its larval stages, it damages combs and honey and is responsible for large losses to bee keepers in the United States. This insect is found almost everywhere that bees are raised. Its greatest damage is done in the Southern States, where its season of activity. is longest.Item UFUGAJI NYUKI(MUMARU (REMP)Mradi wa Usimamizi wa Mazingira Rufiji, 1999) Kisenga, NarcisTokea zama za kale binadamu wamekuwa wakitafuta asali inayozalishwa na nyuki. Kwa azma hiyo shughuli yoyote ya ufugaji nyuki ni kuendeleza zaidi ufanisi wa haya. Binadamu na nyuki hutegemeana. Kwani kwa upande wa nyuki badala ya kuwindwa na kuuawa kwa ajili ya asali yao hutunzwa na kulindwa. Matokeo ya haya siyo tu kupatikana kwa asali na nta bali pia kutambuliwa kwa nyuki kama rasilimali muhimu ya kuhifadhiwa kulindwa na kustawishwa. Ukusanyaji wa asali na nta ni shughuli ya kijadi katika karibu bara lote la Afrika. Wafugaji nyuki wa jadi hutumia mizinga rahisi ambayo njia ya uvunaji asali huluta maangamizo ya makundi ya nyuki. 1 Kwa hiyo iko haja ya kubadilisha njia hii kali ya ufugaji nyuki na kuanzisha ufugaji nyuki mzuri wenye ufanisi zaidi. Huu ni ufugaji wa kutumia mizinga ya masanduku yenye viunzi vya juu au masanduku yenye fremu. Shughuli yenyewe inaweza ikawa ni mradi wa kiwango kidogo ambao unaweza kuendeshwa kirahisi. Nyuki wanasaidia kuchavusha mimea ya asili na ile ya kilimo na biashara. Mizinga haichukui eneo lolote la ardhi na haitegemei pembejeo kutoka nchi za nje. Yeyote anaweza akaanza ufugaji nyuki na familia nzima ikaweza kushirikishwa. Njia nzuri ya kujifunza juu ya ufugaji nyuki ni kufanya kwa vitendo.Item Misitu na hifadhi ya Mazingira(Tanzania Educational publishers L.T.D, 2002) Ngara, LulengeItem Athari za Uharibifu wa Mazingira Katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya - Warsha ya Saba ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki lIiyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003(TARP II-SUA Project, 2004) Bakari, A; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. . Chapisho hili Iinawasilisha mwenendo wa Warsha ya saba ya Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhusu Athari za Uharibifu wa Mazingira katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya iliyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima, watafiti na wataalamu wa ugani ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo.Item Watu na nyuki: Mwongozo (kwa lugha nyepesi) wa Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Wizara ya Maliasili na Utalii, 2004-08)Kijitabu hiki kunatoa mwongozo kwa lugha nyepesi kuhusu Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki Tanzania inayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2001–2010. Programu hii iliidhinishwa na Serikali mwezi Novemba 2001. Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki (PTUN) inakidhi mahitaji ya jumla ya mpango wa maendeleo nchini, hasa Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU). PTUN imeundwa kutokana na mawazo makuu au misingi inayohusiana na maendeleo endelevu na Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Nyuki (UERN). Hii ina maana kwamba mipango ya maendeleo lazima ipangwe kwa kushughulikia masuala ya mazingira, jamii na uchumi. Kama uchumi utakua wakati mazingira yanaharibika na watu wengi wanakuwa maskini, maendeleo hayatakuwa endelevu. Kwa hivyo PTUN inalenga katika uhifadhi wa mazingira, ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini kwa wakati mmoja. Kama uchumi utakua wakati mazingira yanaharibika na watu wengi wanakuwa maskini, maendeleo hayatakuwa endelevu Mtazamo wa PTUN unahusisha mabadiliko ya Sera za Serikali yanayohimiza ushirikishwaji wa jamii, sekta binafsi, washirika katika maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya ufugaji nyuki na vyama mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za nyuki. Ushiriki sawa wa wanawake na wanaume utahimizwa na hii itasaidia katika maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini. Huu ni mtazamo thabiti na wa kusisimua ambao unaleta changamoto na manufaa mengi.Yote haya yamefafanuliwa katika kijitabu hiki.Item Upandaji wa mimea tofauti tofauti: Mwongozo wa nyanjani(Coast Development Authority - Kenya, 2005) Ramezanpour, C; Kamau, M. N; Nguma, B; Muinde, T; Chai, E. C; Karisa, TKenya ina maeneo mengi tofauti tofauti. Jimbo la kati ni baridi, kule mkoa wa Nyanza kuna mvua nyingi, kuna jangwa kaskazini, na hapa pwani ni joto sana. Kila eneo lina sifa maalum – hali ya hewa, hali ya joto, kiasi cha mvua, na udongo. Kwa sababu hiyo kila eneo lina faida tofauti tofauti shambani. Ustawi wa kilimo hapa Kilifi utategemea uwezo wa wakulima. Ni bora watambue faida na nafasi ya ardhi. Kwa mfano: 1. Mimea gani hufanya vizuri hapa? 2. Wakulima wanaweza kukuza mimea gani hapa kupita maeneo mengine? 3. Mimea gani tunaweza kupanda ambayo wale wa sokoni wanataka kununua? 4. Mimea ipi inastahimili kiangazi? 5. Mimea ipi ina uhitaji wa juu katika soko? Tutaona uwezekano mkubwa wa shamba wakati zile taratibu za kulima zinatumia kikamilifu sifa ya ardhi yake. Hili wazo ni msingi ya Upandaji wa Mimea Tofauti Tofauti (Crop Diversification).Item UFUGAJI NYUKI NA KILIMO MSETO Mafunzo kutoka Wilaya za Moshi Vijijini, Hai na Rombo(TARP II-SUA Project, 2005-06) Kawamala, P. M; Lyimo-Macha, J. G; Malimbwi, R. EChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha Kilimo chaNorway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway na Serikali ya Tanzania. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malenqo ya mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na wataalarnu wa ugani ni kupanga utaratibu na kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Ziara hizo za kimafunzo zina madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kujifunza zaidi kutoka kwa wakulima wenzao na hata wakulima wabunifu kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kutambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo. Chapisho hili linawasilisha ripoti ya ziara ya wakulima wadogowadogo waliotoka Kanda ya Mashariki na Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika Aprili 2005. Wakulima hawa waliwatembelea wenzao wa Mkoa wa Kllirnanjaro, wilaya za Hai, Moshi Vijijini na Rombo.Item Ukame: Athari na mbinu za kukabiliana - Warsha ya Kwanza ya Wakulima lliyofanyika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), MOROGORO Tarehe 23-27 Aprili 2006(PANTIL - SUA, 2006) Mwaseba, D. L; Matee, A. Z; Wambura, R. MShughuli za utafiti chini ya Programu ya Mageuzi ya Kilimo na Maliasili kwa Maisha Bora (PANTIL) zilianza rasmi mwanzoni mwa mwezi Januari 2006. Lengo la programu hii ambayo itatekelezwa kwa muda wa miaka minne (2005-2009) ni kuchangia ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuboresha ustawi wa jamii kwa njia ya uboreshaji wa sekta za kilimo na mali asili. Programu hii inazo sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inashughulikia utafiti na uwezeshaji wa wakulima; na sehemu ya pili inashughulikia mageuzi ya kitaasisi na kuboresha uwezo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kiweze kutekeleza majukumu yake ya kitaaluma. Shughuli za uwezeshaji wa wakulima zina lengo la kuwaongezea uwezo wakulima ili waweze kudai elimu husika, teknolojia inayofaa, pamoja na habari ill kuboresha tija, faida na kuchangia katika kuongeza kipato na kupunguza umaskini. Baadhi ya shughuli kadhaa ambazo zitafanyika katika kipindi cha 2006 hadi 2009 ni kama zifuatazo: • Uimarishaji wa vyama/vikundi vilivyopo vya wakulima na uanzishaji wa vikundi vipya kupitia mafunzo ambayo yatahusu uanzishaji vikundi, uendeshaji wake, na uongozi. Shughuli hizi zitahusisha uongozi husika, wadau katika ugani zikiwemo asasi zinazofundisha maafisa ugani. • Kusaidia kuanzisha shule za wakulima katika vijiji na wilaya zitakazochaguliwa • Uchapishaji na usambazaji wa nyenzo za ugani kama vile vipeperushi, vijitabu, n.k. • Uimarishaji wa mbinu za wakulima ili waweze kushiriki katika kutoa mafunzo na usambazaji wa teknolojia mpya kwa wakulima wengine, na kuyafikia maeneo yaliyo nje ya programu ili yaweze kufaidika na programuItem Wanyamapori Tanzania(Wizara ya maliasili na utalii, 2006-12) Wizara ya maliasili na utaliiTaarifa za wataalam zinaonyesha kuwa vina vya maji katika Ziwa Victoria na Ziwa Rukwa vimepungua sana kutokana na uharibifu wa mazingira ambao nchi zilizoendelea hupendelea kuuita Mabadiliko ya Hali ya Hewa" ili kuficha ukweli wakati ni malokeo ya uharibifu wa mazinbgira. Kwa ujumla, mabadiliko ya hali ya hewa ni matokeo ya uharibifu wa mazingira unaotokana na binadamu. pia hutokana na kazi za viwandani ambazo pia zimekuwa zikisababisha moshi ambao huharibu kiambaza kinachozuia watu wa.siaihirike na niiale ya jua.Item A Practical Manual of BEEKEEPING:(How To Content, 2008) Cramp, DavidThis book will help you to start and continue to be a beekeeper. It offers advice in a very practical manner, with step-by-step guidance at each stage of the way. The advice and information it contains are based on general beekeeping knowledge, my own experiences, my successes in beekeeping and, more importantly, my frequent early failings.Item Mazao ya nyuki: Sifa, usindikaji na uuzaji(CTA, 2010) Mutsaers, Marieke; Blitterswijk, Henk van; ’t Leven, Leen van; Kerkvliet, Jaap; Waerdt, Jan van deKitabu kinachoelezea ufugaji nyuki na mazao yanayopatikana kutokana na ufugaji huo na jinsi ya kuyaendeleza hadi kufikia hatua ya uuzaji na kujipatia faida.Item Shughuli za kimaisha na thamani mbalimbali za bioanuwai katika mandhari ya Usambara Mashariki(Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania - TFCG, 2010)Kuna mawazo ya kina yanayokubalika kwamba usimamizi shirikishi utawezekana tu pale mawazo na vipaumbele vya jamii husika yatahusishwa katika mipango ya matumizi bora ya ardhi kama hifadhi na uangalizi unafanyika kwa makini. Hii ni mahususi hasa kwa hifadhi ya bioanuwai kwenye maeneo ya vijiji yaliyo nje ya maeneo yaliyohifadhiwa lakini yana misitu na miti ya hapa na pale. Maeneo haya yanahitaji utafiti wa kina zaidi. CIFOR na ICRAF walikutana 2006 na kufanya ubia, ambao lengo ni kufanya utafiti kuhusu matumizi endelevu ya maliasili, Uhifadhi wa bioanuwai na kuhakikisha kila jamii inanufaika sawa na rasilimali hizi. Shughuli za utafiti wa kimaendeleo zilifanyika kwenye maeneo ya mandhari yenye matumizi ya ardhi na viumbe aina mbalimbali (Landscape mosaics) ambazo zimelenga aina ya misitu, kilimo na shughuli nyingine za kimaisha. Mradi umechangia kuboresha shughuli za kimaisha za jamii za vijijini na uhifadhi wa bioanuwai. Mradi huu umechambua majumuisho ya shughuli za kimaisha za watu wa vijijini ambao wanaishi kwenye eneo la mradi (land scape mosaics) kupitia mfumo endelevu wa shughuli za kimaisha.Item Jarida la mbinu bora(Echo community, 2011) Kinsey, ErwinUfugaji wa mifugo kiasili ni mfumo wa maisha ambao watu au jamii husika wanaishi maisha yao kwa kutegemea mifugo. Katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, wafugaji hawa hutegemea zaidi mifugo ya aiana mbali mbali kama; ng’ombe, kondoo, mbuzi, punda, na ngamia ili kukimu maisha yao na familia zao. Mifugo iliyotajwa, imeorodheshwa kwa kigezo cha kuanzia na lile kundi ambalo sio stahimilivu sana (ng’ombe) na kumalizia na lililo stahimilivu zaidi (punda na ngamia), pia kwa kuzingatia maeneo ya ufugaji kuanzia na yaliyo makame kiasi hadi makame zaidi. Wafugaji hawa wana mchango mkubwa sana katika sekta/idara husika lakini bado hawajaweza kuthaminiwa ipasavyo. Kwa mfano: uwezo wa kutunza/ kuendeleza kizazi cha ng’ombe wa asili. Katika utunzaji wa mifugo yao, wafugaji hawa wana uwezo wa kipekee wa kutumia maeneo yanayokabiliwa na ukame kwa njia ya kuhama hama kwa ajili ya kupata malisho bora na maji. Ni ukweli usiopingika kwamba, katika/ ukanda wa Afrika ya mashariki maeneo ya hifadhi nyingi tunazozifurahia kwa sasa ni matokeo ya wafugaji kuhamahama na kuweza kuyatunza maeneo haya kwa ajili ya malisho na hasa kuweza kuyalinda/kuzuia yasiingiliwe na shughuli za kilimo.Item Nakala ya Ufugaji wa Nyuki (1)(Gay Marris, UK National Bee Unit (Fera), 2011) Gregory, PamImetambulika ya kuwa ufugaji wa nyuki inaweza kuwapa watu wa mashambani njia ya kujipatia mapato zaidi. Ijapokuwa ufugaji wa nyuki sio rahisi kila wakati. Nyuki wanaweza kudunga mara nyingi bila kutarajiwa. Uvunaji wa asali inategemea mbinu nyingi kama vile hali ya anga na kwa kupata soko. Asali ya hali ya juu lazima uwe na ubora zaidi. Nta pia ni bidhaa ya muhimu na wakati mwingine huaribiwa. Mwongozo huu wa shambani imetengenezwa ili kusaidia wakufunzi wanaofanya kazi katika Afrika kusini mwa Sahara. Picha yenye rangi ziko na maneno machache. Nakala hii pia inaeleza mbinu rahisi zinazohitajika kuanzisha biashara ya ufugaji wa Nyuki. Pia inatupatia mawazo au mbinu zinazohitajika kuanzisha ufugaji wa Nyuki kwa kutengeneza vyombo vyao wenyewe wakitumia vifaa vya kiasili. Natumaini kuwa hii itasaidia watu kuanzisha ufugaji wa nyuki kwa bei nafuu na labda kufanya majaribio na vitu vipya. Picha hizi zinaonyesha kati ya njia nyingi ambazo watu hutumia kufuga nyuki. Hii inatarajiwa kuwezesha majadiliano na ushirikiano ili kusaidia watu kutatua shida zao wenyewe. Nakala hii inaegemea ufugaji wa nyuki kutumia mzinga wa ‘top bar’ lakini kuna mbinu nyingi na mawazo zinazoweza kutumika na wafugaji nyuki wa kitamaduni na wale wa kisasa wanaotumia mzinga wa fremu. Inatarajiwa kuwa wakufunzi wataweza kutafsiri mbinu hizi kwa lugha ya kiasili. Shukrani kwa usaidizi wa Waterloo Foundation, kwani nakala nyingine itakuwa tayari ifikapo mwaka 2010. Hii itajumuisha mbinu za kisasa za ufugaji wa nyuki na mbinu za kutatua shida. Nakala ya maandishi pekee kwa wakufunzi pia inaweza kupatikana, kwa kutuma ombi kwa Pam Gregory ambayo inafafanua ‘sababu’ na ‘njia’ za ufugaji wa nyuki. Tuma barua pepe kwa: pamgregory@phonecoop.coopItem Mwongozo wa kilimo bora cha uyoga kukabiliana na athari za mabadiliko hali ya hewa na tabianchi, Tanzania(Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme, 2012) Augustino, S; Makonda, F. B. S; Gillah, P. R; Ishengoma, R. C; Migunga, G. A; Ericksen, SInakadiriwa kuwa zaidi ya watu millioni 20 nchini Tanzania hususan kutoka katika jamii zinazozunguka raslimali za misitu hutegemea Mazao si Timbao kwa ajili ya kuboresha hali ya maisha yao na kipato kazi. Licha ya utegemezi huo, haijulikani bado ni kwa kiasi gani Mazao si Timbao na jamii zinazotegemea mazao hayo zimeathiriwa na kutishiwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi; likiwemo suala zima la jinsi ya kukabiliana na athari hizo. Programmu ya Kujenga Uwezo wa Kudhibiti na Kukabiliana na Athari za Mabadiliko Hali ya hewa na Tabianchi, Tanzania (au CCIAM kwa lugha ya Kiingereza) unafadhili Mradi ujulikanao kama Mazao si Timbao na Ubora wa Maisha ya Jamii zinazoishi Kutegemea Raslimali za Misitu: Athari, Tishio na Ukabilianaji wa Mabadiliko Hali ya hewa na Tabianchi, Wilaya za Kilolo na Kilombero, Tanzania. Mradi huu wa miaka mitatu (2011 – 2013) unalenga kujenga uwezo wa Taifa na wananchi kuelewa chanzo, tishio na athari za mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi na kuwapa mbinu za kukabiliana na athari za mabadiliko hayo katika kaya na jamii nzima kwa ujumla. Hii itasaidia kupunguza uharibifu wa raslimali za misitu, umasikini katika kaya na jamii nzima kwa kuwa na mbinu sahihi za kukabiliana na changamoto za mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi ndani ya mfumo mzima wa matumizi endelevu ya Mazao si Timbao, ambayo ni moja ya huduma muhimu zinazotolewa na raslimali za misitu. Inategemewa kwamba mwisho wa Mradi huu taarifa muhimu kuwasaidia wadau mbalimbali wakiwemo watunga sera na sheria za kukabiliana na athari za mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi Tanzania. Mradi huu pia utachangia katika jitihada za serikali kupitia Mkakati wa Kupunguza Hewa Ukaa na uharibifu wa Misitu yaani MKUHUMI huku ukihakikisha uendelevu wa kipato kazi kwa jamii na usimamizi endelevu wa raslimali za misitu. Mwongozo huu wa Kilimo cha Uyoga kukabiliana na mabadiliko hali ya hewa na tabianchi ni moja ya matokeo ya utafiti wa Mradi kwa kushirikiana na jamii zinazoishi kuzunguka Msitu wa Hifadhi wa New Dabaga-Ulongambi, Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa katika kutafuta mojawapo ya Mazao si Timbao ambayo ni muhimu katika jitihada za awali za kukabiliana na athari za Mabadiliko hali ya hewa na tabianchi. Utafiti wa Mradi umekwisha bainisha na jamii kukubali kuwa kuna mabadiliko hali ya hewa na tabianchi katika eneo hilo ambayo yanaleta athari na tishio kwa jamii hizo na Mazao si Timbao. Katika utafiti wa Mradi, zao la Uyoga unaokusanywa toka msituni lilipewa kipaumbele kama kati ya Mazao si Timbao manne yaliyo katika kipaumbele katika mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko hali ya hewa na tabianchi. Hata hivyo, katika maeneo ya Msitu wa Hifadhi wa New Dabaga-Ulongambi, Uyoga unaonekana kuanza kuadimika kutokana na athari za mabadiliko hayo ambayo yamebadili msimu wa upatikanaji na hata kupunguza kiasi cha uyonga mabo ungeweza kukusanywa na kutumiwa kikamilifu na jamii husika. Kuotokana na hayo, mbinu za kuotesha zao la Uyoga karibu na jamii lilijitokeza. Zao hilo la Uyoga lilionekana linaweza kuisaidia jamii kujipatia chakula na kipato na hivyo kuweza kusaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko hali ya hewa na tabianchi lakini jamii haikuwa na utaalamu au teknolojia rahisi ya jinsi ya kuuotesha nje ya mazingira ya misitu. Kutokana na hali hiyo, Mradi uliona ni vema kuandaa Mwongozo utakaosaidia kutoa mafunzo kwa jamii juu ya Kilimo bora cha Uyoga kama njia mojawapo ya kukabiliana na athrai zinazoletwa na Mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi. Mwongozo huu umeandaliwa kwa kupitia majarida na machapisho mbalimbali ya kiutafiti na hivyo unaweza kutumika hata katika maeneo mengine ya Tanzania na sehemu nyingine ili kuinufaisha jamii husika.Item Mwongozo wa Mafunzo kwa vitendo wa kutayarisha na kutunza bustani ya miche ya miti kwa wanavikundi vya misitu(Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme, 2012) Abdalah, J. M; Augustino, S; Lyaruu, H. V; Silayo, D. A; Kiparu, S. SMradi wa Kuongeza Teknolojia za Kupunguza Hewa ya Ukaa na Kuboresha Maisha ya Jamii zinazozunguka misitu ni sehemu ya Mradi wa Kuweka Mikakati ya Kuokoa Misitu iliyo hatarinini kutoweka nchini Tanzania yaani ‘Strategic Interventions’. Mradi huu upo chini ya Programu ya Kudhibiti na Kukabiliana Mabadiliko ya Tabia ya Nchi Tanzania unaotambuliwa kwa kiingereza kama ‘Climate Change Impact Adaptation and Mitigation (CCIAM) Programme in Tanzania’ unaoratibiwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro. Mradi huu unavishirikisha vyuo vikuu vitatu nchini Tanzania ambavyo ni Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo kikuu cha Ardhi (ARU) pamoja na mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA). Pia mradi unavihusisha vyuo vikuu nchini Norway chini ya uratibu wa Chuo kikuu cha Sayansi cha Norway (UMB). Madhumuni ya Mradi wa Kuongeza Teknolojia za Kupunguza Hewa ya ukaa na Kuboresha Maisha ya Jamii zinazozunguka misitu ni kusaidia juhudi za jamii (watu) husika katika kutekeleza hatua mbalimbali za kulinda, kurejesha na usimamizi endelevu wa misitu ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Mradi huu umepangwa kutekelezwa katika Mji Mdogo wa Masasi, Wilayani Masasi. Mji mdogo wa Masasi una eneo la kilometa za mraba 376.7 na idadi ya watu ni zaidi ya 101,059 (kwa mwaka 2007) ambao wanaoishi katika kata sita za mji huo. Ukiondoa kata ya Mkuti, kata tano zilizosalia ambazo ni Sita, Temeke, Migongo, Jida na Mtandi zinazunguka Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi ambao ni msitu wa asili. Mnamo tarehe 15 – 22 Mei 2011 timu ya wataalamu watano wa mradi walitembelea mji huo kwa madhumuni ya kufanya upembuzi wa awali ndani ya msitu na kufanya mikutano na wadau mbalimbali kama vile wafanyakazi wa mji ndogo, vikundi vya mazingira na serikali za kata za Temeke, Migongo na Mtandi kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo. Upembuzi huo wa awali ulibaini kwamba Msitu huo wa hifadhi wa milima ya Masasi ulikuwa umeharibiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli za binadamu kama vile kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa, mbao na kuni, kulima ndani ya msitu na kuchoma moto. Maeneo mengi ya msitu yalikuwa yameathirika ikiwemo kupungua kwa vyanzo vya maji na vyanzo vya maji vilivyosalia maji yake yalikuwa machafu na hayatoshelezi mahitaji ya jamii inayozunguka msitu. Shughuli za uharibifu wa msitu ziliendelea kufanyika na watu wengi wanaoishi kwenye kata zinazozunguka msitu waliendelea kutegemea rasilimali za msitu huo ili kujipatia mahitaji mbalimbali yakiwemo maji na mazao mbalimbali.Item Woodlot Management Guidelines for Smallholder Farmers(Faculty of Forestry and Nature Conservation, Sokoine University of Agriculture - SUA, 2012-01) Malimbwi, R. E; Zahabu, E; Mugasha, W; Katani, J; Mwembe, UTree planting programme in Tanzania has been advocated for decades but adoption of these activities is not promising in most parts of the country. To the contrary, people in Makete district responded positively to tree planting due to unfavorable climatic conditions and poor soils that contributed to poor agricultural crop production. Also they already know the importance of trees as they contribute highly to the economy of individual households and to the District at large. Previously the income of people in Makete district depended on agricultural products such as maize, wheat, rice, round potatoes and pyrethrum but later due to climate variability and change crops production failed tremendously. This resulted in threatening food security and the wellbeing of rural people of Makete.Item Muongozo wa utunzaji bora wa mashamba ya miti ya wananchi(Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme - CCIAM, 2012-01) Malimbwi, Rogers E; Zahabu, Eliakimu; Katani, Josiah; Mugasha, Wilson; Mwembe, UhuruUpandaji wa miti nchini Tanzania umekuwa ukisisitizwa kwa miongo kadhaa lakini kukubalika kwa shughuli hizi kumekuwa hakuridhishi. Tofauti na watu wa sehemu nyingine za nchi, watu wa Wilaya ya Makete wamehamasika kupanda miti kutokana na hali mbaya ya hewa na ukosefu wa rutuba kwenye udongo sababu ambazo zilisababisha mazao duni ya kilimo. Pia kwa muda mrefu, wananchi wa Wilaya ya Makete wameshajua umuhimu wa miti kwa kuwa kwa kiasi kikubwa mauzo ya miti na mbao yanachangia kipato cha wakulima. Kabla ya kujikita kwenye kilimo cha miti, kipato cha wananchi wa Wilaya ya Makete kilitegemea zaidi mazao ya kilimo kama vile mahindi, ngano, mchele, viazi miviringo na pareto. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, uzalishaji wa mazao hayo umepungua kwa kiasi kikubwa na wakati mwingine kusababisha tishio la njaa.Item Woodlot Management Guidelines for Smallholder Farmers(Faculty of Forestry and Nature Conservation - SUA, 2012-01) Malimbwi, R. E; Zahabu, E; Katani, J; Mugasha, W; Mwembe, UTree planting programme in Tanzania has been advocated for decades but adoption of these activities is not promising in most parts of the country. To the contrary, people in Makete district responded positively to tree planting due to unfavorable climatic conditions and poor soils that contributed to poor agricultural crop production. Also they already know the importance of trees as they contribute highly to the economy of individual households and to the District at large. Previously the income of people in Makete district depended on agricultural products such as maize, wheat, rice, round potatoes and pyrethrum but later due to climate variability and change crops production failed tremendously. This resulted in threatening food security and the wellbeing of rural people of Makete. Responding to this situation, local people of Makete district have established tree woodlots as an alternative source of household income. Makete district is among the southern highlands areas of Tanzania reported to have successful woodlots.Item Miti ya matunda kwa hifadhi ya mazingira na stahamili ya mabadiliko ya tabia nchi(Climate Change Impacts, Adaptation and Mitigation Programme, 2012-03) Kusolwa, Paul M; Mghembe, E. R; Mwaitulo, SKilimo ni uti wa mgongo wa mkulima vijijini. Kulingana na kukua kwa familia, kupungua kwa rutuba na mabadiliko ya mahitaji ya wakulima vijijini wakulima wameendelea kufungua mashamba mapya ili kuongeza mavuno na kipato. Upanuzi huu wa mashamba mara nyingi huambatana na kukatwa kwa miti au misitu. Hali hii inaleta ukame na ongezeko la joto katika maeneo husika. Ukataji wa miti kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa mashamba ya mazao hasa ya chakula yanahusishwa na dalili kubwa za mabadiliko ya tabia nchi. Jitihada nyingi zimefanyika ili kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira kwa kampeni za kupanda miti na kuhamasisha wananchi kutokata miti bila kupanda mti. Hata hivyo mwongozo huu, mara nyingi hulenga miti ya misitu peke yake. Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa mbinu za ustawishaji wa miti ya matunda kama njia nyingine ya kuhifadhi mazingira na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi. Kulingana na tafiti zilizofanyika juu ya miti ya misitu, inatarajiwa kwamba miti ya matunda pia itasaidia kupungua hewa ya ukaa, kupunguza ongezeko la joto, na kuboresha mkusanyiko wa mawingu ya mvua, kuimarisha utunzaji wa maji aridhini katika maeneo ya mashambani. Zaidi ya yote, mit ya matunda itasaidia kuongeza uhakika wa chakula na kipato cha kaya vijijini. Kwa kuwa miti ya matunda itakuwa na thamani kubwa kwa familia, hivyo si rahisi kukatwa kwa matumizi mengine (kama vile kuni au mkaa). Hivyo basi elimu ya uzalishaji wa miche na utunzaji mzuri wa bustani za matunda ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya uoto wa kijani, kuhifadhi ardhi na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi. Kitabu hiki kinatoa maelezo ya mbinu bora za uzalishaji wa miche na ustawishaji wa Miparachichi, Miembe, na Michunga. Chimbuko la kazi hii ni moja ya miradi inaloyenga utekelezaji wa shughuli za mpango mpya unaohusu hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change Impacts Adaptation and Mitigation - CCIAM).
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »