Browsing by Author "Lyimo-Macha, J. G"
Now showing 1 - 9 of 9
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za Uharibifu wa Mazingira Katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya - Warsha ya Saba ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki lIiyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003(TARP II-SUA Project, 2004) Bakari, A; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. . Chapisho hili Iinawasilisha mwenendo wa Warsha ya saba ya Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhusu Athari za Uharibifu wa Mazingira katika Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya iliyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es Salaam, 2-4 Desemba 2003. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima, watafiti na wataalamu wa ugani ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo.Item MATATIZOYA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika VETA Tanga 24-26 Juni 2002(TARP II-SUA Project, 2002-06) Razack, O. M; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na pia kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na ., washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima waKanda ya Mashariki Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa VETA, Tanga, tarehe 24-26 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item MATUMIZI BORA YA ARDHI- Mafunzo kutoka Mlima Meru(Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania - TARP II - SUA Project), 2002-09) Lyimo-Macha, J. G; Malimbwi, R. E; Kiranga, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo Wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Wagani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha mafunzo yatokanayo na ziara iliyofanyika Septemba 2002. Ziara hii iliwashirikisha wakulima na washauri wa wakulima kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha wilaya za Kilosa, Handeni, Pangani, Mkuranga na Morogoro na kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwajumuisha wakulima na wagani kutoka wilaya za Mbeya, Mafinga, Njombe, Mbinga na Mbozi ambao walitembelea wakulima wa wilaya ya Arumeru, Arusha walioshiriki katika rnradi wa SCAPA. Makala hii pia inapatikana katika lugha ya kiingereza.Item UENDELEZAJI WA VIKUNDI VYA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI - Warsha ya Nane ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika Ukumbi wa CCM, Lushoto, Tanga - 21-23 Juni 2004(TARP II-SUA Project, 2005) Vallery, F; Kawamala, P; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: • Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji • Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo • Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele • Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya nane ya wakulima wa Mikoa ya kanda ya Mashariki kuhusu Uendelezaji wa Vikundi vya Wakulima iliyofanyika ukumbi wa CCM, Lushoto, Tanga, 21-23, Juni 2004. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item UENDELEZAJI WA VIKUNDI VYA WAKULIMA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI - Warsha ya Nane ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Ukumbi wa Allamano wa Vijana wa Kikatoliki Makambako, Njombe 7-9 Juni 2004(TARP II-SUA Project, 2004-06) Vallery, F; Kiranga, E; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLT-I), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula la Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Mradi huu arnbao ulianza rasrni mwczi Septernba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: I. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pandc zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 11a ufugaji 2. Kucharnbua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutarnbua mambo gani yapewc uzito au kipaumbele 4. Kushiriki katika kupeana uzocfu wa maenco muhimu ya kilimo na mifugo. Chapisho hili linawasilisha rnwenendo wa warsha ya nane ya wakulima wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhusu Uendelezaji wa Vikundi vya Wakulirna- iliyofanyika ukurnbi wa Allamano wa Vijana wa Kikatoliki, Makambako, Njombe, 7-9, Juni 2004. Mwenendo wa warsha umcchapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item UFUGAJI NYUKI NA KILIMO MSETO Mafunzo kutoka Wilaya za Moshi Vijijini, Hai na Rombo(TARP II-SUA Project, 2005-06) Kawamala, P. M; Lyimo-Macha, J. G; Malimbwi, R. EChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha Kilimo chaNorway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway na Serikali ya Tanzania. Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malenqo ya mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na wataalarnu wa ugani ni kupanga utaratibu na kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Ziara hizo za kimafunzo zina madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani ili kujifunza zaidi kutoka kwa wakulima wenzao na hata wakulima wabunifu kwa lengo la kufanikisha kilimo na ufugaji 2. Kutambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo na mifugo. Chapisho hili linawasilisha ripoti ya ziara ya wakulima wadogowadogo waliotoka Kanda ya Mashariki na Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika Aprili 2005. Wakulima hawa waliwatembelea wenzao wa Mkoa wa Kllirnanjaro, wilaya za Hai, Moshi Vijijini na Rombo.Item UHUSIANO WA UHAKIKA WA CHAKULA, UKIMWI NA LISHE BORA: Warsha ilifanyika Makambako - Njombe Tarehe 30 Novemba - 04 Desemba 2004(TARP II-SUA Project, 2005-02) Lyimo, C. S; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. G; Macha, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH) wakishirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), wamekuwa wakitekeleza mradi wa "Uhakika Wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo" (TARP II - SUA Project). Mradi ulianza mwaka 2000 na unagharamiwa na Serikali ya Norway pamoja na serikali ya Tanzania. Madhumuni ya warsha hii yanalenga kuleta ushirikiano wa karibu kati ya wakulima wadogo wadogo ngazi ya kaya, wagani, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na watafiti wa kilimo na mipango katika kuinua uwezo wa maisha ya mtanzania katika ngazi ya kaya; kiuchumi, kiafya na maendeleo kwa ujumla. UKIMWI ni tatizo kubwa linatishia kuwepo kwa binadamu. UKIMWI hauishii kumuua muathirika na kupoteza nguvu kazi tu, lakini pia jamii ya muathirika huathirika kwa narnna moja au nyingine. Nguvu kazi ya muathirika hupotea kwa ajili ya kumuuguza mgonjwa; fedha nyingi hutumika kwani mgojwa anahitaji chakula maalum na dawa; watoto hukosa huduma ya wazazi na hivyo kushindwa kusoma au kupata lishe bora; mgonjwa anapofariki kuna gharama za mazishi na nguvu kazi-hupotea kuhudumia misiba. Warsha ililenga kubaini mtazamo wa jamii kuhusu athari za UKIMWI katika uhakika wa chakula na kukuza elimu ya UKIMWI na lishe bora kwa kutumia wataalamu walioshiriki.Item Vikundi vya Wakulima na Teknolojia: Mafunzo toka Turiani, Morogoro na Mbozi, Mbeya(TARP II Project - SUA, 2002) Lyimo-Macha, J. G; Batamuzi, E. KMakala hii inawasilisha ripoti ya ziara mbili zilizofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba na Novemba 2001. Ziara ya kwanza ya kimafunzo ya wakulima iliwashirikisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Kilosa, Kilombero, Rufiji na Morogoro Vijijini, ambao waliwatembelea wakulima wa mpunga wa Mkindo, Turiani wilaya ya Morogoro. Ziara ya pili iliwajumuisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Mbeya vijijini, Iringa Vijijini, Njombe, Ludewa na Chunya ambao walitembelea vikundi vya wakulima wa wilaya ya Mbozi. Taarifa hii pia inapatikana katika lugha ya kiingereza.Item Ziara ya mafunzo kwa wakulima kati ya nyanda za mashariki na ya nyanda za juu kusini(TARP II - SUA Project, 2001) Lyimo-Macha, J. G; Batamuzi, E. K; Tarimo, A. J. PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula, pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Washauri wa Ugani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara mbili (kanda moja kwenda kanda nyingine) zilizofanyika mwezi Agosti na Septemba 2001. Ziara ya kwanza ya kimafunzo ya wakulima iliwashirikisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Mbinga, Njombe, Makete na Mbeya (Kanda ya nyanda za juu kusini) hawa waliwatembelea wakulima wenzao wa wilaya ya Lushoto. Ziara ya pili iliwajumuisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Bagamoyo, Morogoro Vijijini na Kilosa (Kanda ya Mashariki) ambao waliwatembelea wakulima wa wilaya za Njombe na Mbarali.