Mifugo na Uvuvi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Mifugo na Uvuvi by Subject "Biashara"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Baiashra ya ufugaji bora wa kuku wa asili: kitabu cha mwongozo(Rural Livelihood Development Company - RLDC, 2008)Ufugaji wa kuku ni nyenzo nzuri ya kujipatia kipato katika kaya kwa sababu ufugaji wa kuku hauhitaji mtaji mkubwa na hauna kazi kubwa kiuendeshaji. Katika ufugaji huria kuku hujitafutia chakula wenyewe. Pia inapowezekana hupewa mabaki ya chakula, chenga, pumba au nafaka yoyote inayopatikana katika mazingira husika. Kwa walio wengi ifikapo nyakati za jioni, kuku hulala jikoni au ndani nyumbani kwa mfugaji mwenyewe. Ufugaji huu ni rahisi kwa kuwa hauna gharama kubwa ila faida yake ni kitoweo tu au fedha kidogo sana. Kutokana na lishe duni na kuzaana wenyewe kwa wenyewe (bila kubadili jogoo), kuku wa kienyeji walio wengi wana uzito mdogo. Wana wastani wa uzito wa robo tatu za kilo hadi kilo moja wakiwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja. Ila wakitunzwa vizuri zaidi na kuboreshwa wana uwezo wa kufikia uzito wa kilo moja hadi moja na nusu katika umri wa miezi sita hadi nane. Kwa upande wa utagaji wa mayai kuku wa kienyeji kwa wastani hutaga mayai 50 hadi 65 kwa mwaka. Wakitunzwa vizuri zaidi huweza kufikia uzalishaji wa mayai 80 hadi 100 kwa mwaka. Kijitabu hiki kinatoa maelezo ya njia na kanuni mbalimbali rahisi za kuzingatia ili mfugaji aweze kuzitumia kupata mazao mengi na bora zaidi yatakayomnufaisha kimapato na kwa matumizi mengine. Kanuni hizi ni pamoja na: √ Kuchagua njia bora ya kufuga na sifa za mabanda bora ya kuku √ Kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga, kuzaliana na kutotolesha √ Utunzaji wa vifaranga √ Kutengeneza chakula bora cha kuku √ Kudhibiti na kutibu magonjwa √ Kutunza kumbukumbu √ Kutafuta masokoItem Ufugaji wa nyuki kibiashara na ubora wa mazao yake.(Wakala wa misitu Tanzania, 2019-05-02) Wakala wa misitu TanzaniaKarne mbili zilizopita, ufugaji wa nyuki kibiashara ulianza baada ya kuibuka kwa teknolojia za kukabiliana na wadudu hao na kupanuka kwa soko la asali na mazao yake ikiwamo nta inayotumika viwandani. Licha ya kuwa na zaidi ya miaka 100 ukifanyika, bado biashara ya asali duniani ni fursa kwa wananchi, lakini wengi hawajui kama ipo na imekumbatia utajiri mkubwa. Tanzania ni nchi ya pili duniani katika uzalishaji asali; zao kuu litokanalo na nyuki ikiwa nyuma ya Ethiopia. Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), inaratibu shughuli za ufugaji wa nyuki na ushauri wa kibiashara kwa wazalishaji na wauzaji wa asali na mazao yake. Kalenda ya ufugaji wa nyuki nchini imegawanyika katika misimu minne kulingana na majira kwa mwaka, ambayo hutofautiana kati ya mkoa na mkoa. Kaimu meneja mawasiliano wa TFS, Tulizo Kilaga anasema katika kila msimu, kazi ya ufugaji wa nyuki hutegemea na kundi la nyuki linahitaji nini na mfugaji afanye nini kuweza kuzalisha mazao ya nyuki. “Ipo misimu minne ya nyuki kwa mwaka ambayo ni msimu wa njaa, kujijenga kwa nyuki, mtiririko wa asali na msimu wa mavuno kwa mfugaji wa nyuki,” anasema Kilaga.