Mifugo na Uvuvi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Mifugo na Uvuvi by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 134
Results Per Page
Sort Options
Item Udder diseases of diary cows(U. S. DEPARTMENT OF AGRICULTURE, 1961-05-08) Brown, Richard Y.T IlE DAIRY cow'S udder (fig. 1) has been highly developed by cen turies of careful, selective breeding. It is complex in its structure and physiology. The secretory tissue of the gland is made up of great numbers of alveoli or hollow balls composed of milk-secreting cells which are mi croscopic in size and grouped like clusters of grapes around the ducts (fig. 2). The milk is formed in the alveoli and travels down through the ducts to the gland cistern and teats. The size of the passageway through the teat is greatly reduced at its lower end. This constriction prevents escape of milk from the udder and acts as a barrier against entrance of micro-organisms. Each quarter of the udder is separate and milk is being continually secreted in active glands. Much of it, however, is only forced down.Item Kichaa cha mbwa ni hatari(Ukulima wa kisasa, 1982-06)Kichaa cha mbwa ni ugonjwa wa hatari sana unaoleta vifo kwa binadamu na wanyama.Una dalili zinazoambatana na mishipa ya fahamu ambazo mwanzo huwa ni kuongezeka kwa furaha au hasira,kupoteza fahamu na mwishowe kupooza kwa viungo vya mwili,Item Jarida la uenezi wa ufugaji wa samaki kwa wakulima(ALCOM/FAO/SUA, 1984)Jarida hili linajumuisha kwa pamoja majarida matatu; Jinsi ya kutengeneza bwawa lako la samaki, Jinsi ya kulisha samaki wako na Jinsi ya kutunza bwawa lako la samaki yaliyotolewa na ALCOM kwa matumizi ya jimbo la mashariki, Zambia. Kufuatia matokeo ya utafiti, marekebisho kadhaa yamefanywa ili kuimarisha elimu ya ufugaji wa samaki Tanzania.Item Kulima na kufuga kwa njia ya kisasa(INADES-FORMATION, 1987-11-13) Inades-formation, TanzaniaKijitabu kidogo hiki kina mambo ya msingi. Yafaa ukisome kabla hujaanza kujifunza. Kinaelekeza mambo muhimu matano: Masomo haya yatamsaidia na kumfaidi nani?, Zipo faida gani katika kujifunza?, Yakupasayo kujua juu ya masomo haya, Jinsi ya kujifunza masomo haya, Jinsi ya kufanya kazi za mazoezi.Item Mafunzo ya ufugaji(inades formation Tanzania, 1992) Inades formation TanzaniaTanzania ina idadi kubwa ya kuku wa kienyeji wanaofugwa kwa mtindo wa huria vijijini na hata mijini. Katika mtindo huu wa ufugaji, kuku huachwa huru mchana kutwa kujitafutia chakula wao wenyewe. Pengine baadhi ya wakulima huwatupia kuku wao mabaki ya chakula, chenga za nafaka au nafaka zenyewe. Wapo pia wakulima walio na utaratibu wa kuwapa kuku wao pumba za nafaka na maji ya kunywa kila inapowezekana. Zinapofika nyakati za jioni kuku hulala jikoni, au ndani ya nyumba ya mkulima mwenyewe. Ingawaje ufugaji wa aina hii ni rahisi, lakini faida inayopaikana (kama ipo) ni ndogo sana. Kutokana na kuzaana wenyewe wa wenyewe (kutobadili jogoo), lishe duni n.k., kuku hawa wana umbo dogo. Hutaga mayai machache, tena madogo madogo. Nyama yao ina ladha nzuri, lakini kwa vile wana umbo dogo, kiasi cha nyama wanayotoa ni kidogo tu. Katika kijitabu hiki “Kufuga na Kuboresha Kuku wa Kienyeji” tutazungumzia jinsi ya kuboresha kuku wa kienyeji kwa njia ya uzalishaji, kutumia jogoo bora, kuboresha lishe ya kuku. Tutazungumzia pia njia mbalimbali za kufuga zinazoweza kumnufaisha mfugaji mdogo. Kutokana na maarifa haya wewe mkulima utaweza kuona haja ya kufanya mabadiliko katika ufugaji wako. Hi uweze kunufaika na ufugaji ni lazima uwe na mifugo bora. Kitabu hiki kimeandikwa ili kukupatia maarifa na mbinu za kutumia ili upate kuku bora kutokana na kuku wako wa kienyeji. Katika kitabu kingine “ Kufuga kuku wa biashara” Utajifunza maarifa na mbinu bora za ufugaji wa kuku wa biashara. Hawa ni kuku wa kigeni. Wanahitaji matunzo maalum tofauti na yale ya kuku wa kienyeji wanaoboreshwa.Item Faida za mifugo kwa wakulima(Ukulima wa kisasa, 1993-09) Magembe, A.Kilimo na ufugaji wa ngombe,mbuzi au kondoo ni shughuli ambazo zina manufaa mengi kwa mkulima,kwani zinategemeana sana.Mkulima ambaye pia ni mfuaji hunufaika zaidi kuliko yule asikuwa na mifugo:na mfugaji naye pia hunufaika zaidi iwapo analima pia mazao.Item Ufugaji bora wa samaki katika maji matamu (yasiyo na chumvi)(Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), 1994)Kitabu hiki kimechapishwa na shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO). Dhumuni ni kumpatia mkulima elimu juu ya ufugaji bora wa samaki katika maji matamu (yasio na chumvi) ikiwa ni pamoja na kufahamu namna bora ya uandaaji wa madimbwi ya maji ya samaki, utunzaji pamoja na uvunaji wa samaki. Elimu hii itampatia mkulima usitawi na kusitawisha uchumi wake kwa ujumla.Item Use of cassava and sweet potatoes in animal feeding(Food and Agricultural Organization - FAO, 1995) Ravindran, VMwongozo uliotolewa wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa unaoelezea na kuchambua matumizi ya muhogo na viazi vitamu kama chakula cha wanyama.Item Mwongozo kuhusu ufugaji wa ngamia(Heifer Project International, 1996)Ufugaji wa ngamia unafanywana watu wengi katika mataifambalimbali ulimwenguni kw ajili ya kujipatia maendeleo katika sehemu zilizo na ukame.Ngamia wamekuwa wakisaidia katika shughuli nyingi kama vile kubeba mizigo, kubeba watu kwa kupandwa mgongoni, kulima kwa kutumia jembe la kukokotwa linalovutwa pia na maksai.kuvuta mikokoteni na kutoa mazima na nyama kwa matumizi ya binaadamu. Nchini Tanzania ufugaji umeanza hivi karibuni tu na tena katika maeneo machache sana. Mwongozo huu ni muhimu na utamsaidia mfugaji kuelewa mambo mengi kuhusiana na ufugaji wa ngamia.Item Duck management Guide(CENTRAL POULTRY DEVELOPMENT ORGANISATION (SOUTHERN REGION) -India, 1998)Ducks occupy an important position next to chicken farming in India. They form about 10% of the total poultry population and contribute about 6-7% of total eggs produced in the country. Ducks are mostly concentrated in the Eastern and Southern States of the country mainly coastal region with non-descriptive indigenous stocks, which however are poor layers. Central Duck Breeding Farm under Ministry of Agriculture, Government of India was established in the year 1981 during the 5th Five Year plan with technical collaboration of Government of United Kingdom in order to introduce high yielding variety of ducks for the benefit of farming community.Item Sera ya Taifa ya ufugaji nyuki(KIUTA Dar es Salaam - Tanzania, 1998-03) Wizara ya maliasili na utaliiSekta ya ufugaji nyuki Tanzania imeendeshwa bila ya kuwa na sera tangu mwaka 1949 wakati ilipoanzishwa rasmi kama idara katika Wizara ya Kilimo. Tangu wakati huo, mwongozo wa kuendeleza na kusimamia rasilimali za nyuki na mimea ya chakula chao umekuwapo kupitia maagizo ya kitaalamu na kiutawala. Madhumuni makuu ya mwongozo huo yalikuwa ni kuufanya ufugaji wa nyuki uwe wa kisasa kwa kuanzisha mizinga ya masanduku, kuongeza uzalishaji wa asali na nta na kuongeza mapato yatokanayo na uuzaji wa asali na nta nchi za nje . Mabadiliko mengi ya kijamii, kiuchumi na kimazingira yanayotokea pamoja na marekebisho ya sera kuu ya uchumi yaliyotekelezwa nchini, na ongezeko la kujali uhifadhi wa mazingira ili kuleta maendeleo endelevu ya ufugaji nyuki yamepelekea kuundwa kwa Sera ya Ufugaji Nyuki. Sera hii inazingatia nafasi ya ushirikiano na uratibu wa sekta mtambuka ambao utaimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za nyuki na mimea ya chakula chao katika mashamba ya kilimo, misitu na maeneo ya wanyamapori yaliyohifadhiwa. Rasimu ya sera ya ufugaji nyuki awali ilitayarishwa kama sehemu ya Sera ya Misitu na utayarishaji wa rasimu hii ulihusisha washikadau husika katika warsha tatu tofauti, mikutano mbali mbali ya Idara ya Misitu na Nyuki, Washauri wa Kitaalamu na kikosi maalumu cha utekelezaji. Rasimu ya mwisho ilitayarishwa kwa kuboresha na kuunganisha hoja, mapendekezo na maazimio yaliyopitishwa na warsha hizo tatu na katika mikutano mingine ya kiushauri. Chanzo kingine muhimu cha habari zilizotumika katika rasimu hii ya mwisho ni Mpango wa Utekelezaji wa Misitu Tanzania (TFAP) ambao unajumuisha Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki (NBP). Masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya sekta ya ufugaji nyuki yaliyokuwamo katika Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ambayo yalitayarishwa mwaka 1989 yakiwahusisha washikadau wakuu katika mikutano ya vijiji na warsha za kitaifa, yamejumuishwa katika sera hii. Iliamuliwa kuwa rasimu inayojitegemea ya Sera ya Ufugaji Nyuki iandikwe badala ya kuijumuisha na ile ya Misitu, ili malengo na madhumuni yake yawe bayana na yenye kueleweka. Hii pia inatazamiwa kuwa itawezesha kuzingatiwa kikamilifu kwa masuala ya sekta ya ufugaji nyuki na yale ya sekta mtambuka zenye misingi yake katika ufugaji nyuki na matamko ya sera ambayo ndiyo msingi wa uundaji wa Sheria ya Ufugaji Nyuki. Sheria ya Ufugaji Nyuki itakuwa ndiyo nyenzo kuu ya utekelezaji wa sera hii.Item Ufugaji bora wa sungura(SUA - TU Linkage Project, 2000) Laswai, G. H; Mnembuka, B. V; Lugeye, S. CKijitabu hiki kimetayarishwa ili kukidhi mahitaji ya wafugaji wa sungura katika Tanzania. Kinajihusisha zaidi na kanuni muhimu ambazo mfugaji wa sungura anapashwa kuzifuata au kuzingatia wakati akitunza wanyama hawa.Item Mwongozo wa magonjwa ya kuku vijijini(Sokoine university of agriculture, 2002) TARP II-SUA ProjectUtambuzi yakinifu wa magonjwa ya ndege wafugwao ni mgumu kupita ule wa magonjwa ya mifugo mengine. Hii ni kwa sababu dalili za ugonjwa kwa mnyama hai peke yake hazitoshi kusema ugonjwa usumbuao kwa hakika, hivyo uchunguzi wa mnyama aliyekufa ni muhimu sana katika kutoa uamuzi wa ugonjwa usumbuao kwa ndege wafugwao. Mara nyingi, dalili za mgonjwa hai na za yule aliyekufa kwa magonjwa ya ndege wafugwao huwa zinaoana. Pia kwa magonjwa mengi, kuna upungufu au kutokuwepo kabisa kwa ugunduzi yakinifu wa kuaminika, hivyo historia ya ugonjwa pamoja na kufuatilia kwenye kundi ni vitu muhimu katika uchunguzi wa ugonjwa. Pale popote inapowezekana, uchunguzi wa mnyama aliyekufa ufanywe kwenye zaidi ya mnyama mmoja toka kwenye kundi la waathirika na pia uchunguzi wa maabara ufanyike kwenye vipimo vilivyochukuliwa na kuhifadhiwa vyema.Kijitabu hiki cha magonjwa ya ndege wafugwao vijijini kinadhamiria kutoa taarifa za haraka na muhimu kwa magonjwa yaliyozoeleka kwa ndege wafugwao vijijini nchiniTanzania. Kimedhamiriwa kwa wasaidizi wa waganga wa mifugo wanaofanya kazi vijijini ambako kuna upungufu wa vitabu vya kusoma. Msisitizo umewekwa kwa magonjwa yaliyozoeleka ambayo yanaripotiwa mara kwa mara kwa kuku wanaotunzwa kwa ufugaji huria hapa Tanzania. Maelezo mengi yanahusu mfululizo wa magonjwa yaliyozoeleka yasababishwayo na virusi, bakteria, na ukosefu wa virutubisho mwilini.Item Chemical composition of poultry feedstuffs in tanzania(SUA, 2002-01-23) Laswai, G. H.; Mutayoba, S. K.Balancing feeds for monogastric animals requires reliable information with regard to the nutritional values of the available feed resources. Such information is limited for Tanzanian feedstuffs. In most cases feed formulations are based on the data obtained from other parts of the world. It is well known that chemical composition and hence feed values are influenced to a large extent by the processing techniques and ecological characteristics of the area and these make the acquired information not precisely representing the nutritional values of those feeds. leading into imbalanced compounded diets. Realizing this problem. researchers at Sokoine University of Agriculture (SUA) saw the need to develop this catalogue of feed tables of poultry "feedstuffs with the major purpose of improving the quality of poultry feeds produced in Tanzania.Item Preparation of reptile skins Crocodile, Lizard and Snakes(2002-04-19) Prince, K. W. TREPTJ LE skins, such as crocodile, alligator, lizard and snake, make very attractive and durable leather. Unfortunately, owing to faulty preparation, reptile skins often reach the tanners in too bad a condition to tan. The usual blemishes are cuts, gouge marks, bad shape, scale slip and putrefaction. Damage due to delayed flaying or dragging over rough ground is also common. So is damage due to overdrying or over-exposure to the sun, to distortion and overextension, or to the action of beetles after the skins have been dried.Item Kuku wa kienyeji(Chuo cha kilimo cha Sokoine, 2002-12) TARP II SUA ProjectWarsha iliandaliwa na Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania (TARP II SUA) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoinc cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula pamoja na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo (NLH). Lcngo kuu la warsha lilikuwa ni kubaini sababu zinazofanya uzalishaji wa kuku wa kienyeji kutokidhi mahitaji ya soko na kubuni mbinu za kukabiliana nazo ili mkulima aweze kuongeza uzalishaji wa kuku wa kienyeji na anufaike na soko lililopo la kuku wa kienyeji. Warsha ilikuwa na madhumuni mahsusi yafuatayo ili kufanikisha lengo hilo.Item Ufugaji bora wa sungura - 3(International Tanfeed Ltd, 2004)Kwa mazingira yetu haya ya joto, unyevunyevu mkubwa na jua kali hivyo katika uchaguzi wa sehemu sahihi kwa ajili ya ufugaji wa sungura inategemeana na vitu vifuatavyo; Mahali maalum Hali ya hewa Mtaji Ukubwa wa mradi.Item Malisho ya kupandwa(Mradi wa uhakika wa chakula na pato la kaya kwa wakulima wadogowadogo Tanzania (TARP II-SUA Project), 2004-08-19) Mugasha, A. G.Mifugo aina ya ngombe, mbuzi, kondoo na punda wanahitaji vyakula vya aina kuu tano, ili waweze kukua na kutoa maziwa mengi au kufanya kazi mbalimbali.Item Ufugaji bora wa sungura - 1(International Tanfeed Ltd, 2005)Ufugaji wa sungura ni moja wapo ya chanzo kizuri cha mapato nchini Tanzania kama watanzania watafanya yafuatayo, • Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji. • Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa sungura. • Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi. • Hulka ya uvumilivu na kuthubutu. • Malengo thabiti ya ufugaji wa sungura. • Tathmini ya soko la bidhaa za sungura. • kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa sunguraItem Ongeza maziwa na upunguze gharama kwa kulisha mifugo kaliandra(World Agroforestry Centre - ICRAF, 2005) Lyamchai, C. J; Kweka, E. S; Mwikari, M. M; Kingamkono, M. N; Wambugu, CKaliandra (Calliandra calothyrsus) ni mmea aina ya mikunde wenye asili ya Amerika ya Kati na Mexico. Ulipandwa mara ya kwanza nchini Indonesia kwa ajili ya kivuli katika mashamba ya kahawa, lakini kwa sasa mti huo umeonyesha faida zaidi kwa kutumika kama chakula cha mifugo, kuni na kuhifadhi udongo. Katika nchi nyingi ikiwemo Kenya, Tanzania na Uganda, Kaliandra hutumika kama lishe ya ng’ombe wa maziwa na mifugo wengine. Kaliandra ina kiasi kikubwa cha protini (asilimia ishirini hadi ishirini na tano) na huchanganywa na aina nyingine za majani yenye kiwango kidogo cha protini kama vile matete au majani tembo (Napier kwa Kiingereza) ili kuongeza lishe kwa mifugo, uzalishaji wa maziwa na kiasi cha mafuta katika maziwa. Ijapokuwa Kaliandra haichavulishwi na nyuki, imekuwa chanzo kikubwa cha asali. Nchini Indonesia, nyuki wameweza kutengeneza kilo elfu moja ya asali kwa mwaka kutoka ekari mbili za shamba iliyopandwa Kaliandra. Faida zingine ni kuboresha uchavushaji wa kahawa na kuni ambazo hukauka vizuri na kuwaka kwa urahisi.