Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Subject "Chakula"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Baadhi ya vikokotooo muhimu kwa wasindikaji wa vyakula(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2014) Tiisekwa, B. P. MKipeperushi chenye maelezo yanayochanganua mahesabu kwa ajili ya wasindikaji wa vyakulaItem Mbinu bora za kilimo kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011-02) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. BMatunda na mbogamboga ni mazao muhimu katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, kama yalivyo muhimu katika ulimwengu wote. Mazao haya ni chanzo cha vitamini, madini, antioxidants, kambakamba za chakula and wanga ambayo ni mahitaji muhimu ya mwili. Virutubisho hivi huongeza ubora wa chakula na huzuia binadamu kupata magonjwa sugu. Hata hivyo, matunda na mbogamboga huharibika kirahisi sana na hivyo hupoteza kwa haraka sana thamani yake ya lishe na ya kiuchumi. Makadirio ya upotevu wa matunda na mbogamboga baada ya mavuno katika nchi zinazoendelea ni asilimia 40%. Hii inamaanisha kuwa katika kipindi ambacho siyo cha mavuno, kaya hukabiliwa na upungufu wa matunda na mbogamboga kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa namna ya kuhifadhi na kusindika kwa ajili ya matumizi katika mwaka mzima. Matokeo ya muda mrefu ya hali hii ni uhaba wa bidhaa iliyosindikwa katika ngazi ya chini na kutokidhi mahitaji ya viwango vya ubora kwa masoko ya ndani na nje nchi. Changamoto hizi zimeisukuma ASARECA kuwekeza katika utafiti na maendeleo katika teknolojia za mazao freshi na kuongeza thamani na mapato yatokanayo na bidhaa hizo.Item Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna. Kitabu na. 1(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Nafaka ni mazao makuu ya chakula ambayo hutumiwa na watanzania wote waishio mijini na vijijini. Nafaka zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko mazao mengine ya chakula na mara nyingi nafaka huzalishwa mara moja au mbili kwa mwaka. Kwa hiyo ili iweze kupatikana na kutumika kwa wakati wote ni lazima kuhifadhi. Aidha ili kuweza kuwa na bidhaa zenye thamani ni lazima kusindika. Jitihada zimekuwa zikifanywa na seikali kuongeza tija na uzalishaji wa mazao hayo. Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka. Pamoja na ongezeko la uzalishaji, teknolojia zinazotumika katika uvunaji, utayarishaji na hifadhi ni duni na husababisha upotevu mkubwa wa mazao hayo. Wastani wa tani 1,559,000 za mazao ya nafaka hupotea kila mwaka. Aidha upotevu mkubwa hutokea katika maghala kutokana na kuhifadhi nafaka ambayo haijakauka sawasawa na pia kutokana na mashambulizi ya wadudu waharibifu. Kuongeza uzalishaji pekee hakutakuwa na maana ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kupambana na matatizo yasababishayo upotevu wa mazao hayo. Teknolojia sahihi za utayarishaji wa mazao kabla ya kuhifadhi zisipotumika, nafaka itaharibika hata kama ingehifadhiwa katika ghala bora. Hivyo ni vyema kutumia njia bora za kutayarisha nafaka kama vile kukausha vyema, kusafisha na kufungasha ili kupunguza uharibifu unaosababisha upotevu wa mazao. Lengo la uandaaji wa kitabu hiki ni kuelimisha jamii kuhusu teknolojia sahihi za uvunaji, utayarishaji, ufungashaji, usindikaji na hifadhi ya mazao ya nafaka baada ya kuvuna. Aidha matumizi bora yanayokidhi mahitaji ya lishe ya mazao hayo yameainishwaili kupunguza tatizo la utapia mlo na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na kuongeza kipato. Walengwa wa kitabu hiki ni wakulima na wadau wengine ambao wamejiajiri katika sekta ya kilimo.