Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Title
Now showing 1 - 20 of 56
Results Per Page
Sort Options
Item Baadhi ya vikokotooo muhimu kwa wasindikaji wa vyakula(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2014) Tiisekwa, B. P. MKipeperushi chenye maelezo yanayochanganua mahesabu kwa ajili ya wasindikaji wa vyakulaItem BRICS: Mkakati mbadala wa ushirikiano wa kimaendeleo?(Policy Forum, 2014) Mutalemwa, Darlene K; Mutalemwa, Deo PMandhari ya hali halisi ya ushirikiano wa kimaendeleo inabadilika huku kukiwa na ongezeko la washirika wapya ambao ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, unaojulikana kwa pamoja kama BRICS . Washirika hawa wapya ambao wanawakilisha fursa mpya, rasilimali mpya na makubaliano mapya ya mikataba; huku mkazo mkubwa zaidi ukilenga katika mwelekeo thabiti wa ukuaji wa kiuchumi, kupunguza umaskini na kupata maendeleo ndivyo vinavyoleta changamoto kwa mashirika ya kimaendeleo na wajasiriamali wa nchi za magharibi. Utafiti huu unatokana na kusoma vitabu pamoja na nyaraka mbalimbali za kitaalam, unachangia katika uchambuzi wa maslahi ya sasa ya BRICS kwa Tanzania kwa upande mmoja, (na maslahi ya Tanzania-kwa nchi hizi-kwa upande mwingine), kwa kutoa mtazamo wa kuongeza maarifa na ufahamu wa nafasi ya BRICS na, faida na athari zake kwa Tanzania.Item Design Considerations when Shopping for Used Equipment or Fabricating Equipment(Sokoine University of Agiculture - SUA, 2011-02) Tiisekwa, B. P. M; Chove, B. E; Ndibakunze, B. K; Suleiman, ROne must remember that food process equipment should be designed for sanitary operation and ease of maintenance and cleaning. 1. Food contact should be constructed of non-corrosive and non-toxic materials...Item Elimu ya Ujasiriamali: Kuelekea kwenye Maendeleo Endelevu Tanzania(Haki Elimu, 2021) Muhura, ChirakaNchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa mfano, zimejaliwa raslimali ambazo zinaweza kub- adilishwa kuwa mali. Lakini suala ni jinsi ya kuzigeuza raslimali hizo ili kuwa vitu halisi. Elimu isiyofaa imeelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha kuzibadilisha raslimali hizo kuwa vitu halisi. Elimu ya Tanzania inasemekana kuwa ni elimu inayowaandaa watu kuwa waajiriwa wa maofsini, japokuwa nafasi za kazi ni chache ukilinganisha na idadi ya watu wanaotafuta kazi za kuajiriwa. Kwa ufupi, elimu yetu haijengi ubunifu na udadisi ambao ungewawezesha watu ama kujiajiri (ujasiriamali) au kuzipanua fursa za ajira ambazo zingewawezesha watu wengi kupata ajira. Fursa za ajira hazijatumiwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuweza kuwachukua watu wote wenye sifa za kuajiriwa. Chapisho hili kwa hiyo linaibua jinsi elimu ya ujasiriamali inavyoweza kuibadilisha nchi kutoka kwenye utegemezi na kuwa nchi yenye kujitegemea.Item FAHAMU KUHUSU BIASHARA YA MKONGE NCHINI TANZANIA NA CHANGAMOTO ZAKE(Jamii Forum, 2017-01) Jamii forumMkonge au Katani ni moja kati ya zao la biashara Jina la kisanyansi inaitwa Agave sisalana. Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi nyingine, kwa mara ya kwanza lilitambushwa katika nchi za kitropikia na subtropikia India,Tanzania, Brazil, Kenya south Africa, Angola, Mozambique Morocco Uganda, Zimbabwe na Mauritius. Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka Pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan na kuisafisha kwa kupitia Frolida, Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo Kikokwe huko Pangani Tanga. Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanganyika mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka 1960 Tanganyika ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na mexico kwa mauzo ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi. Kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miaka ya 1970 uzalishaji ulipungua toka tani 230,000 hadi tani 19,700 kwa mwaka 1997. Hata ivyo mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 ambayo yalilenga katika ubinafisishaji na biashara huria , uhuru wa taasisi za kifedha za ndani na nje ya nchi yalifufua kilimo cha mkonge na hasa kukamilika kwa ubinafishaji mwaka 2005 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40,000 mwaka 2015 hii inatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mkonge na bidhaa zake pamoja na kupanda bei kwenye soko la dunia pamoja na ndani. Soko kuu la mkonge wa Tanzania ni china, Saudi Arabia , India, Uhispania, Ujerumani, Uingereza, Kenya, Uganda na Nigeria.Item Good Agrucultural Practices for Trainers and Processors(ASARECA, 2011-02) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Tiisekwa, A. B; Suleiman, RFruits and vegetables are important crops in Eastern and Central Africa, just as they are the world over. They are a source of essential vitamins, minerals, antioxidants, fibres and carbohydrates which our bodies crucially need. These nutrients improve the quality the human diet and protect us from chronic diseases. Fruits and vegetables, however, are highly perishable leading to drastic nutritional and economic losses. Estimated post harvest losses for fruits and vegetable in developing countries is 40%. This means that during the off-season, households face shortage of fruits and vegetables due to lack of knowledge on how to preserve and process them for year-round consumption. The long term implication is that supplies of locally processed products are inadequate and do not meet the required quality standards for domestic and international markets. These challenges have spurred ASARECA to invest in research and development on fresh produce technology to add onto their value and increase incomes. In response to this particular challenge, ASARECA initiated a project; “Processing for commercial exploitation of selected tree-fruits and vegetables in Tanzania and Rwanda” to validate the existing protocols for processing dried products and fruit juices on commercial but small scale basis.Item Hatua za kuafuata katika usindikaji wa vipande vya embe kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. B; Chove, BKipeperushi kinacholezea njia ya usindikaji wa matunda na mboga mboga kibiashara.Item Hatua za ukaushaji wa mchicha kwa kutumia kaushio la mionzi ya jua: Mradi wa kusindika kibiashara kwa baadhi ya matunda na mbogamboga hususan maembe, makarara na mchicha Tanzania na Rwanda.(ASARECA, 2011-02) Tiisekwa, A. B; Suleiman, R; Ndibakunze, B. K; Tiisekwa, B. P. MMchicha wenye vishindo. Ulionyauka au kuharibika hauchambuliki kwa urahisi na pia hushusha ubora wa bidhaa ya mwisho. Mchicha ulio zeeka hua na nyuzinyuzi ambazo ni ngumu kuiva, kutafunikika na haziwezi kumeng’enywa katika mfumo wa chakula na hivyo kuukoseshea mwili virutubisho.Item Hatua za utengenezaji wa juisi ya makakara kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011-11) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. B; Chove, BKipeperushi kinachoeleza jinsi ya usindikaji wa jiusi ya makakara - passion kwa ajili ya biashara.Item Jinsi ya kuhifadhi chakula vizuri kwa muda mrefu(2020-05) Fam Radio Internationa, Fam Radio InternationaKutokana na kuzuiwa watu kutembea katika nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), masoko mengi ya vyakula halisi yamefungwa au kuzuiwa. Hii inathiri wachuuzi, wafanyabiashara, na watumiaji. Wakati, hadi sasa, minyororo ya thamani ya nafaka na kunde haijaathiriwa sana, watumiaji hawawezi kupata chakula halisi kwa ajili ya familia zao, haswa matunda na mboga, maziwa, na nyama. Vyakula hivi vinaweza kuharibika na, bila njia bora za kuweza kuzihifadhi na kubaki katika uhalisia vinaweza kuoza haraka. Ni vigumu kusisitiza sana umuhimu wa kula vyakula halisi. Matunda na mboga ni chanzo kingi na kisicho ghali cha nishati, virutubisho vya kujenga mwili, vitamini, na madini. Thamani yake kama lishe ni kubwa yanapokuwa halisi, lakini matunda na mboga nyingi hukaa katika hali ya uhalisi kwa muda mfupi sana, isipokuwa ikiwa yamehifadhiwa haraka na vizuri baada ya kuvunwa. Katika nchi ambazo vyakula halisi vinapatikana tu katika kipindi fulani cha mwaka, watu wametengeneza njia tofauti za kuhifadhi na kuongeza muda wa vyakula kubakia kuwa halisi ili viweze kuliwa wakati wa kipindi ambacho vyakula halisi havipatikani. Njia hizi ni muhimu sana kwa wakulima, wachuuzi, na wasindikaji. Vyakula halisi kwa kawaida huoza isipokuwa pale vinaposindikwa kwa njia fulani au kuhifadhiwa katika hali maalum. Mchakato wa kuoza ni kwa sababu ya vitendo vya viumbe-vidogo vinavyopatikana kwenye vyakula hivyo. Lakini kuoza kunaweza kupunguzwa kwa kuongeza uhifadhi, kusindika vyakula, na kutumia njia bora za uhifadhi. Matunda na mboga zinapaswa kutayarishwa kuhifadhiwa haraka iwezekanavyo baada ya kuvuna, ndani ya masaa 4 hadi 48. Uwezekano wa kuharibika huongezeka haraka kadiri wakati unavyopita.Item Job market surveys, training needs assessment and tracer studies for SUA undergraduate programmes.(SUA, 2008-06-25) PANTILSokoine University of Agriculture (SUA) through the FOCAL (Future Opportunities and Challenges in Agricultural Learning) Programme in 2005 commissioned studies to survey job markets, assess training needs and conduct tracer studies in relation to the current and future employment opportunities. The aim was to provide SUA with evidence of the required labour market demands hence training needs in terms of methods, contents and skills required. In order to facilitate the exercise, thirteen degree programmes were grouped into five agricultural and natural resources fields (clusters). Four firms were assigned consultancy works in the five clusters. These firms were: i) K-Rep Advisory Services (Cluster No. I), ii) Agrisystems (EA) Ltd (Cluster No.2), iii) Development Associates Ltd (Cluster No.3 & 4) and iv) Afrozone Ltd (Clusters No 5).Item Kifahamu kilimo cha maua(Jamii Forums, 2016-10-13) Jamii ForumsKilimo cha maua ni sayansi au sanaa ya kukuza matunda, mboga mboga, maua, au mimea ya mapambo. ). Wafanyabiashara wa maua wanafahamu sana katika uwanja huu, lakini ufafanuzi wake kamili ungeenea zaidi ya kile tunachofikiri kawaida kama bustani au kilimo.Item Kilimo bora cha pilipili kichaa(Mjasiriamali Hodari, 2020-01) Mjasiriamali HodariZao la Pilipili kichaa 'Hot pepper' au 'Chilli pepper' (Capsicum frutescens) hulimwa maeneo mengi ulimwenguni ikiwemo nchini Tanzania. Matunda ya pilipili hutumika kwa matumizi mbali mbali kama chakula au kama tiba (medicinal properties) na kuimarisha afya ya mraji. Kwa upande wa chakula pilipili hutumika kama kionjo cha vyakula mbalimbali kama Supu, kachumbali, nyama choma, nyama rosti, maharage, mboga za majani, kutengenezea chilli sauce n.k. Kwenye chakula pilipili huongeza radha maridhawa kabisa, ndio maana mtu aliyezoea kula vyakula vyenye pilipili huwa hafurahii chakula kisichokua na pilipili. Kwa upande wa tiba pilipili/pilipili kichaa ina vitamini nyingi (Capsaicin compounds) ikiwemo niacin, pyridoxine, riboflavin, na thiamine n.k. Uwepo wa vitamini hizi pilipili hutumika katika kutengenezea madawa (Ointment) ya kuondoa maumivu ya viungo na misuli. Kufahamu faida nyingi za kiafya za kutumia pilipili.Item Kutunza kumbukumbu za biashara kwa wakufunzi na wasindikaji: Mradi wa kusindika kibiashara matunda na mbogamboga unaotekelezwa Tanzania na Rwanda(ASARECA, 2011-10) Tiisekwa, F. A; Kashindye, ABaada ya kusoma kijitabu hiki msomaji anatefgemewa kuweza: - Kutunza vizuri kumbukumbu na hati za biashara. - Kuujua umuhimu na thamani ya kumbukumbu za biashara. - Kuzitathmini benki na kuweza kuchagua akaunti ya benki inayofaa. - Kuambatisha gharama kwenye bidhaa na kupanga bei na mishahara ambavyo vitawasaidia katika uainishaji. - Kujua umuhimu wa orodha ya bidhaa na jinsi ya kuisimamia ili kupunguza gharama.Item Mafuta-mwali ya nazi(Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Mikocheni, 2016)Kipeperushi kinachoelezea utengenezaji na matumizi ya mafuta ya naziItem Majaribio kuhusu uhifadhi wa nafaka kijiji cha Mlali(Wizara ya Kilimo na Chakula, Tanzania, 2014)Wakulima wengi Tanzania wanapata hasara kubwa inayosababishwa na wadudu waharibifu wa mazao yanapohifadhiwa kwenye maghala. Uharibifu huu unatishia uhakika wa chakula kwa kaya. Kaya zingine zina uwezo wa kununua madawa ya kuulia wadudu, lakini madawa haya yana gharama kubwa na yaweza kuwa na madhara kwa afya zao, (na kama yakiwa yameharibika huwa hayafai kwa matumizi). Mradi huu umebuniwa kutafiti ubunifu kwa ajili ya wakulima kuhusu matumizi ya madawa asilia ya “diatomaceous earths” (vumbivumbi linalotokana na masalia ya zamani ya viumbe wa majini), katika kuhifadhi mazao kama njia mbadala vijijini. Kwa njia hiyo watafiti watawajibika kwanza kufanya majaribio na kulinganisha uwezo wa madawa mbalimbali katika zoezi zima la kudhibiti wadudu waharibifu wa nafaka, ziwapo ghalani. Awali, majaribio haya linganifu yatafanywa kwa kipindi cha miezi 8 kuendana na msimu wa kuhifadhi mazao, kuanzia Julai 2002 hadi Machi 2003.Item Masoko ya mazao ya kilimo(Sokoine university of A griculture, 2020-05-20) Mtega, WullystanMkulima anatakiwa kutafuta soko la mazao yake kabla hajaanza shughuli ya uzalishaji shambani. Ili kupata taarifa za kutosha, mkulima anashauriwa kufanya utafiti wa soko. Mkulima anaweza tumia njia kuu mbili: (i) kuandaa dodoso na kuwauliza wadau muhimu wa soko la zao alilozalisha na, (ii) kutembelea masoko ya mazao na kukusanya taarifa kwa njia ya kuona. Utafiti wa soko humwezesha mkulima kutoa maamuzi sahihi juu ya uuzaji wa mazao yake. Katika kuuza mazao, mkulima lazima azingatie sheria, kanuni na taratibu za nchi na soko husika. Pia, ni muhimu kuelewa namna nguvu ya soko inavyofanya kazi. Hii itamsaidia mkulima kujua lini ayapeleke mazao sokoni na hivyo kupata bei nzuri zaidiItem MATATIZO YA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Kituo cha Anglikana, Iringa Juni 6-8, 2002(TARP II-SUA Project, 2002-06) Msangi, R. O; Malimbwi, R. EChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji ushirikishwaji wa wadau wote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogo wadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Anglikana, Iringa, tare he 6-8 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item MATATIZOYA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika VETA Tanga 24-26 Juni 2002(TARP II-SUA Project, 2002-06) Razack, O. M; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na pia kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na ., washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima waKanda ya Mashariki Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa VETA, Tanga, tarehe 24-26 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item Mbinu bora za kilimo kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011-02) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. BMatunda na mbogamboga ni mazao muhimu katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, kama yalivyo muhimu katika ulimwengu wote. Mazao haya ni chanzo cha vitamini, madini, antioxidants, kambakamba za chakula and wanga ambayo ni mahitaji muhimu ya mwili. Virutubisho hivi huongeza ubora wa chakula na huzuia binadamu kupata magonjwa sugu. Hata hivyo, matunda na mbogamboga huharibika kirahisi sana na hivyo hupoteza kwa haraka sana thamani yake ya lishe na ya kiuchumi. Makadirio ya upotevu wa matunda na mbogamboga baada ya mavuno katika nchi zinazoendelea ni asilimia 40%. Hii inamaanisha kuwa katika kipindi ambacho siyo cha mavuno, kaya hukabiliwa na upungufu wa matunda na mbogamboga kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa namna ya kuhifadhi na kusindika kwa ajili ya matumizi katika mwaka mzima. Matokeo ya muda mrefu ya hali hii ni uhaba wa bidhaa iliyosindikwa katika ngazi ya chini na kutokidhi mahitaji ya viwango vya ubora kwa masoko ya ndani na nje nchi. Changamoto hizi zimeisukuma ASARECA kuwekeza katika utafiti na maendeleo katika teknolojia za mazao freshi na kuongeza thamani na mapato yatokanayo na bidhaa hizo.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »