Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 56
Results Per Page
Sort Options
Item SACCOS(Unkown, 2000)Mwongozo wa uendeshaji na uratibu wa vikundi vidogo vidogo ya kuchangiana - SACCOSItem Mfumo wa stakabadhi wa maghala Tanzania(Warehouse Receipts Regulatory Board, 2000)Mfumo wa Stakabadhi za Maghala ni mfumo unaotumika nchini wa kutumia bidhaa zilizohifadhiwa kwenye maghala badala ya mali zisizohamishika kuwa dhamana ya kupata mikopo kutoka asasi za fedha. Mfumo kama huu pia unatekelezwa nchi nyingine za bara la Afrika pamoja na mabara ya Ulaya na Amerika. Kwa kufuata mfumo huu wakulima wadogo na wakati wakiwa kwenye Ushirika au Vikundi vya wakulima wanakuwa na nguvu ya soko na kuingia katika soko la ushindani ambalo ingekuwa vigumu kutokana na kukosekana kwa mitaji. Pia mfumo huu unasaidia kuzuia upotevu wa mazao unaotokana na uhifadhi dhaifu, kuhifadhi mazao ili kusubiri kuuza wakati muafaka na pia kuongezea bidhaaa thamani kabla ya kuziuza.Item MATATIZOYA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika VETA Tanga 24-26 Juni 2002(TARP II-SUA Project, 2002-06) Razack, O. M; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na pia kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na ., washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima waKanda ya Mashariki Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa VETA, Tanga, tarehe 24-26 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item MATATIZO YA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Kituo cha Anglikana, Iringa Juni 6-8, 2002(TARP II-SUA Project, 2002-06) Msangi, R. O; Malimbwi, R. EChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji ushirikishwaji wa wadau wote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogo wadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Anglikana, Iringa, tare he 6-8 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item Teknolojia za Hifadhi, Usindikaji na Matumizi ya Mazao ya Mbegu za Mafuta baada ya kuvuna(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Aina nyingi za mafuta ya kula yanayotumika hapa nchini hutokana na mazao ya mbegu za mafuta, mbata na michikichi. Mafuta hupatikana baada ya kusindika mbegu au mbata. Mafuta hutumika kama kiungo muhimu katika mapishi mbalimbali kwani huongeza ladha ya chakula. Mafuta pia ni muhimu kwa afya, huongeza joto na nguvu mwilini. Uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta nchini hautoshelezi mahitaji ya viwanda na kusababisha pengo lililopo kuzibwa kwa kuagiza mafuta toka nje ya nchi. Aidha uzalishaji mdogo wa mazao hayo, umesababisha viwanda vikubwa vya kusindika mafuta nchini kuwa vichache. Uzalishaji mdogo wa mazao haya umetokana na wakulima wengi kutozingatia kanuni za kilimo bora kama vile kupanda aina ya mbegu zenye kutoa mafuta mengi, jambo ambalo linafanya bidhaa ipatikanayo kutokana na mazao hayo kuwa kidogo na kutotosheleza mahitaji ya walaji. Wakulima wengi hutegemea kuuza mazao ya mbegu za mafuta kwa wasindikaji wadogo wanaotumia mashine ndogo ndogo zilizosambaa katika maeneo mengi yanayozalisha mazao hayo. Vilevile teknolojia za usindikaji za asili zinazoendelea kutumika katika maeneo mengi, husababisha upotevu wa mafuta wakati wa usindikaji kwani mafuta mengi hubakia kwenye mashudu. Lengo la uandaaji wa kitabu hiki ni kuelimisha jamii kuhusu hifadhi, usindikaji na matumizi ya baadhi ya mazao ya mbegu za mafuta baada ya kuvuna ili kuongeza usalama wa chakula pamoja na kipato. Walengwa wa kitabu hiki ni wakulima na wadau wengine ambao hujiajiri katika sekta ya kilimo Teknolojia zilizoanishwa katika kitabu hiki pia zitasaidia wasindikaji wadogo wa mazao ya mbegu za mafuta kupata uwezo wa kuchagua na kutumia mashine zenye ufanisi mzuri ili kuweza kukamua kiasi kikubwa cha mafuta kutoka kwenye mbegu na kupunguza upotevu wa bidhaa.Item Mwongozo wa Tekinolojia za Utunzaji wa Mazao ya Bustani Baada ya Kuvuna(Kituo cha Utafiti na Habari za Tekinolojia za Baada ya Kuvuna, Chuo Kikuu cha California, Davis, 2003) Kitinoja, L; Kader, A. ALicha ya kutumia kiwango cha kisasa cha teknolojia husika, utunzaji fanisi baada ya kuvuna ni jambo muhimu katika kufikia lengo linalokusudiwa. Wakati wazalishaji wa kiwango kikubwa wananufaika kwa utumiaji wa tekinolojia za kisasa za baada ya kuvuna kwa kuwekeza katika mitambo ya hali ya juu, siyo rahisi kwa wazalishaji wa kiwango kidogo kufanya hivyo, badala yake teknolojia rahisi na za gharama ndogo zinaweza kuwafaa. Wazalishaji wa kiwango kidogo ni walio na mitaji midogo, wakulima wanaouza mazao moja kwa moja sokoni na wafanyabiashara wa kati wanaowauzia mazao wasafirishaji wa nje ya nchi. Mambo mapya yaliyovumbuliwa hivi karibuni katika teknolojia zinazotumika baada ya kuvuna (mazao) yanajibu matamanio ya kuepuka matumizi ya gharama kubwa za utendaji kazi na kupata bidhaa bora. Njia hizi zinaweza zisiwe endelevu kwa kipindi kirefu kutokana na masuala ya kijamii na kiuchumi, kiutamaduni na au mazingira. Kwa mfano, matumizi ya viuatilifu baada ya kuvuna yanaweza kupunguza matukio ya mashambulizi ya wadudu waharibifu lakini yanaweza kuwa na matokeo yenye gharama kifedha na katika mazingira. Pamoja na hayo, kuongezeka kwa mahitaji ya matunda na mboga zinazozalishwa kwa kutumia kilimo hai/kilimo ogani, kunatoa fursa ya upatikanaji wa soko kwa wakulima wa kiwango kidogo na wauzaji. Hali halisi ya wanaohudumia (handlers) mazao kwa kiwango kidogo inajumuisha matumizi ya nguvu kazi ya ziada, ukosefu wa mikopo kwa ajili ya kuwekeza katika teknolojia zinazotumika baada ya kuvuna, nishati ya umeme isiyoaminika, ukosefu wa usafiri mbadala, vifaa vya kuhifadhi na au vifungashio na kuwepo kwa vikwazo vingine. Kwa bahati nzuri, kuna wigo mpana wa teknolojia rahisi za kutumia zinazoweza kuchaguliwa na mbinu nyingi zenye uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu ya watunzaji wa kiwango kidogo na wauzaji wa mazao. Kwa miaka mingi mbinu zilizopo katika mwongozo huu, zimefanikiwa kupunguza upotevu na kutunza ubora wa mazao ya bustani katika sehemu mbalimbali duniani.Item Teknolojia za Utayarishaji, Hifadhi na Usindikaji wa Mazao ya Mizizi baada ya Kuvuna(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Mihogo, viazi vitamu na viazi mviringo ni mazao muhimu ya mizizi nchini Tanzania. Mazao hayo ni chanzo cha virutubishi mbalimbali hususan wanga, vitamini A (viazi vitamu vya rangi ya karoti), vitamini B na protini (majani ya mihogo). Mazao ya mizizi hustawi katika sehemu nyingi nchini na yana sifa ya kustahimili hali ya ukame hasa mihogo na viazi vitamu. Mazao hayo yana matumizi mengi kama vile chakula cha binadamu, mifugo, katika viwanda ni mali ghafi katika utengenezaji wa karatasi, wanga, gundi na katika utengenezaji wa vyakula maalum vya mchanganyiko wa mazao kwa lengo la kuboresha virutubishi. Mazao ya mizizi huharibika haraka yakihifadhiwa katika hali ya ubichi kutokana na kuwa na maji mengi. Hali hii pia husababisha usafirishaji kwenda kwenye masoko ya mbali kuwa mgumu. Aidha, matumizi ya mbinu duni wakati wa kuvuna, kutayarisha, kufungasha na kusindika husababisha upotevu mkubwa wa mazao hayo hadi kufikia aslimia 45. Ili kupunguza upotevu wa mazao ya mizizi, Wizara ya Kilimo na Chakula imetoa kitabu hiki kuwa mwongozo wa kuwelimisha wakulima na wadau wengine matumizi ya mbinu bora za uvunaji, utayarishaji, usindikaji, ufungashaji na hifadhi ya mazao ya mizizi baada ya kuvuna. W akulima na wadaun wengine wakizingatia matumizi ya teknolojia zilizoainishwa, wataweza kupunguza upotevu wa mazao ya mizizi, kuongeza akiba ya chakula, kuongeza thamani, matumizi ya mazao hayo na kujiongezea kipato hivyo kupunguza umaskini.Item Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Matumizi ya Matunda na Mboga baada ya kuvuna(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Mboga na matunda ni tegemeo la binadamu katika kupata vitamini na madini mbali mbali yanayohitajika kuujenga na kuulinda mwili kila siku. Mazao haya ni ya msimu kwa maana kwamba kuna vipindi yanapatikana katika hali ya ubichi (fresh) kwa wingi na kuna kipindi hayapatikani kabisa. Vitamini na madini yapatikanayo katika mazao haya hayahifadhiki katika mwili wa binadmu kama vile protini na wanga. Viinilishe vinavyopatikana katika mazao haya husaidia kuboresha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.Hivyo kutokana na umuhimu wake na kutoweza kuhifadhika mwilini ni lazima mboga na matunda yajumlishwe kwenye mlo/milo ya siku. Hifadhi ya mboga na matunda ili kuhakikisha upatikanaji kwa muda wote ni ngumu kutokana na kwamba mazao haya yana maji mengi (80-90%). Maji haya husaidia kukuza na kuongezeka kwa vimelea vya bakteria na fangasi ambavyo husababisha uharibifu wa mazao hayo kama yakihifadhiwa kwa njia ya kwaida kama mazao mengine. Upotevu wa mazao haya baada ya mavuno unakadiriwa kuwa ni kati ya asilimia 40 hadi 80 kutegemea aina ya zao. Upotevu huu ni mkubwa na unasababisha uhaba mkubwa wa vyakula hivyo vya lazima kwa binadamu. Teknolojia za utayarishaji, hifadhi na matumizi pamoja na za usindikaji wa baadhi ya mtunda na mboga zimeainishwa katika kitabu hiki. Aidha katika toleo lingine mazao mengine yatajumuishwa na masahihisho au maboresho ya teknolojia yataainishwa. Ni matumaini ya wataalamu wa liokiandika kwamba teknolojia hizi zikitumika wakulima na walaji wengine wataweza kujipatia mboga na mtunda hata baada ya msimu ili kudumisha afya.Item Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna. Kitabu na. 1(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Nafaka ni mazao makuu ya chakula ambayo hutumiwa na watanzania wote waishio mijini na vijijini. Nafaka zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko mazao mengine ya chakula na mara nyingi nafaka huzalishwa mara moja au mbili kwa mwaka. Kwa hiyo ili iweze kupatikana na kutumika kwa wakati wote ni lazima kuhifadhi. Aidha ili kuweza kuwa na bidhaa zenye thamani ni lazima kusindika. Jitihada zimekuwa zikifanywa na seikali kuongeza tija na uzalishaji wa mazao hayo. Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka. Pamoja na ongezeko la uzalishaji, teknolojia zinazotumika katika uvunaji, utayarishaji na hifadhi ni duni na husababisha upotevu mkubwa wa mazao hayo. Wastani wa tani 1,559,000 za mazao ya nafaka hupotea kila mwaka. Aidha upotevu mkubwa hutokea katika maghala kutokana na kuhifadhi nafaka ambayo haijakauka sawasawa na pia kutokana na mashambulizi ya wadudu waharibifu. Kuongeza uzalishaji pekee hakutakuwa na maana ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kupambana na matatizo yasababishayo upotevu wa mazao hayo. Teknolojia sahihi za utayarishaji wa mazao kabla ya kuhifadhi zisipotumika, nafaka itaharibika hata kama ingehifadhiwa katika ghala bora. Hivyo ni vyema kutumia njia bora za kutayarisha nafaka kama vile kukausha vyema, kusafisha na kufungasha ili kupunguza uharibifu unaosababisha upotevu wa mazao. Lengo la uandaaji wa kitabu hiki ni kuelimisha jamii kuhusu teknolojia sahihi za uvunaji, utayarishaji, ufungashaji, usindikaji na hifadhi ya mazao ya nafaka baada ya kuvuna. Aidha matumizi bora yanayokidhi mahitaji ya lishe ya mazao hayo yameainishwaili kupunguza tatizo la utapia mlo na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na kuongeza kipato. Walengwa wa kitabu hiki ni wakulima na wadau wengine ambao wamejiajiri katika sekta ya kilimo.Item Teknolojia za hifadhi usindikaji, na matumizi ya mazao ya mikunde baada ya kuvuna(Wizara ya Kilimo na Chakula., 2003-08-07) Jamhuri ya Muungano wa T anzania, Wizara ya Kilimo na ChakulaMazao jamii ya mikunde yanayolimwa hapa nchini ni maharage, soya, kunde na mbaazi. Sifa kubwa ya mazao haya ni kuwa na kiwango kikubwa cha protini nyingi na uwezo wa kuongeza naitrojeni kwenye udongo. Uzalishaji wa mazao haya ni wastani wa tani 490,000 kwa mwaka. (Takwimu, Wizara ya Kilimona Chakula) Hata hivyo kiasi kikubwa cha mazao hayo hupotea baada ya kuvuna. huu husababishwa na matumizi ya mbinu duni katika uvunaji, ukaushaji, usafirishaji, usindikaji na hifadhi. Kiasi kikubwa cha mikunde hupotea wakati wa kuvuna kutokana na kuchelewa kuvuna ambapo mapodo hupasukia shambani. Hali hii huruhusu mashambulizi ya wadudu waharibifu kwa urahisi na punje nyingi kuachwa shambani. Katika uvunaji, mazao mengi hupotea kwani mbinu zinazotumiwa na wakulima bado ni duni na za kuchosha, hivyo mazao mengi huachwa shambani.Item Usindikaji wa muhogo: Utengenezaji wa rale - ongeza thamani na ubora wa bidhaa ya muhogo(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo - SUA, 2004)Muhogo ni moja ya mazao ya mizizi hapa Tanzania na nchi nyinqi za Africa. Muhogo una wanga mwingi. Zao hili hustahimili ukame na hivyo husaidia sana katika harakati za kupambana na njaa hasawakati wa ukame. Pamoja na umhimu wake, muhogo huharibika upesi sana. Mara baada ya kuvunwa muhogo huweza kuharibika ndani ya siku tatu au nne na kutofaa kwa matumizi ya binadamu. Pia usafirishaji wa muhogo kutoka sehemu moja hadi nyingine ni mgumu na wa gharama kubwa. Hii inatokana na mihogo kuwa na kiasi kikubwa cha maji. Mambo haya husababisha hasara kubwa kwa mkulima.Item Ujasiriamali katika biashara Tanzania(2005) Makindara, J. RKijitabu kinazungumzia kwa ujumla mambo ya kuangalia katika ujasiriamali uanzishaji na uendeshaji wa biashara katika mazingira ya TanzaniaItem Uboreshaji waVihenge, Hifadhi Bora na Udhibiti wa Viumbe Waharibifu wa Mazao Ghalani(Kurugenzi ya Utafiti na Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA, 2005-01) Makundi, R. H; Misangu, R. N; Reuben, S. O. W. M; Kilonzo, B. M; Ishengoma, C. G; Lyimo, H; Mwatawala, MHifadhi bora ya mazao inahakikisha familia inakuwa na chakula cha kutosheleza mwaka mzima. Pia mazao yanaweza kuuzwa wakati wowote ili kuongeza kipato. Mradi wa hifadhi bora ya mazao na udhibiti wa viumbe waharibifu umebuniwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA),na unafadhiliwa na Programu ya FOCAL,SUA. Mradi huu unawalenga wakulima katika wilaya tatu Tanzania ambazo ni Handeni, Mvomero na Iringa Vijijini. Hifadhi bora na udhibiti wa wadudu, panya na viumbe wengine wanaoharibu mazao ghalani ni muhimu ili kuhakikisha mazao kama mahindi, kunde, maharage, mpunga, n.k. yanayozalishwa na wakulima hayaharibiwi wakati yanapohifadhiwa. Utafiti shirikishi unafanyika juu ya mbinu za asili na za kisasa ili kuboresha hifadhi ya mazao na kudhibiti viumbe waharibifu wa mazao ghalani.Item Mbinu za ugani za matumizi ya picha kwa ajili ya majadiliano na vikundi vya wakulima: Njia Bora za Udhibiti Husishi wa Viduha(Kituo cha Utafiti - Ilonga, Morogoro Tanzania, 2005-04)NAKALA YA AWALI - MWONGOZO KWA MTUMIAJI ni kijitabu kinachotoa mwongozo kutoka Taasisi ya Utafiti wa mazao cha Ilonga ili kusaidia wakuliima na vikundi vya wakulima kuweza kuthibiti magugu na wadudu mbalimbali kwenye mazao yao mashambani.Item Job market surveys, training needs assessment and tracer studies for SUA undergraduate programmes.(SUA, 2008-06-25) PANTILSokoine University of Agriculture (SUA) through the FOCAL (Future Opportunities and Challenges in Agricultural Learning) Programme in 2005 commissioned studies to survey job markets, assess training needs and conduct tracer studies in relation to the current and future employment opportunities. The aim was to provide SUA with evidence of the required labour market demands hence training needs in terms of methods, contents and skills required. In order to facilitate the exercise, thirteen degree programmes were grouped into five agricultural and natural resources fields (clusters). Four firms were assigned consultancy works in the five clusters. These firms were: i) K-Rep Advisory Services (Cluster No. I), ii) Agrisystems (EA) Ltd (Cluster No.2), iii) Development Associates Ltd (Cluster No.3 & 4) and iv) Afrozone Ltd (Clusters No 5).Item Mihogo - njia bora za ukaushaji na usindikaji(Mitiki Blogspot, 2009-12)Mihogo mibichi iliyovunwa huoshwa mara mbili. Uoshaji wa kwanza ni ule wa kuondoa udongo baada ya kuvuna, na uoshaji wa pili ni baada ya kumenya mihogo kabla ya kukausha.Baada ya kuoshwa mihogo humenywa kwa kutumia kisu kikali, na kutumbukizwa ndani ya maji safi. Baada ya kumenya kiasi kinachotakiwa mihogo huoshwa na maji safi hadi kuwa myeupe.Item Mwongozo wa uendelezaji endelevu wa biofueli kimiminika Tanzania(Wizara ya Nishati na Madini, Tanzania, 2010-11)Katika miaka ya karibuni, uendelezaji wa biofueli umekuwa ni agenda ya kawaida duniani kote. Fueli zimiminikazo ambazo zinatokana na tungamotaka zinathibitisha kuwa mbadala wa fueli za fosili hususani bidhaa za petroli katika hali ya mafuta ya petroli na dizeli. Hivyo, biofueli zinaweza kutumika katika kupikia, kutoa mwanga, kuzalisha umeme na kuendeshea vyombo vya usafiri. Biofueli kwa ufafanuzi ni fueli zitokanazo na tungamotaka na zinaweza kuwa katika hali ya yabisi, gesi na kimiminika. Biofueli yabisi ni pamoja na mkaa na kuni; biofueli gesi ni biogesi, gesi inayozalishwa katika madampo yaliyofukiwa na udongo, n.k, na biofueli kimiminika inajumuisha mafuta yanayotokana na mbegu za mimea au mimea yenyewe kama, ethano na biodizeli.Item Mwongozo wa Mafunzo ya Usindikaji wa Nafaka za Jamii Kunde: Ongezeko la Thamani kwa Maharagwe, kunde , Karanga na Soya kwa Wakulima Wadogo Barani Afrika(Tropical Soil Biology and Fertility Institute ya International Centre for Tropical Agriculture (CIAT-TSBF), 2011)Ukulima wa maharagwe, kunde, karanga na maharagwe soya una faida nyingi kama vile kuweka naitrojeni kutoka hewani na kuboresha rutuba ya udongo. Ø Nafaka za jamii kunde zina protini kiwango cha juu na zaweza kutayarishwa ili kupata vyakula vyenye virutubisho zinazosaidia kukamilisha vyakula vya aina ingine. Ø Mchanganyiko wa nafaka kuu (k.v. mchele, mtama, mbaazi na mahindi) na jamii kunde ziwe kwa uwiano wa 70:30 ili kufikia kiwango kinachohitajika cha amino asidi. Ø Sifa na jinsi ya kutayarisha na kupika nafaka za jamii kunde nne muhimu wakati zinapopikwa zimeelezwa. Muhimu pia kwa mapishi ya nafaka hizi ni uzito na ujazo (ml) hivyo elimu kuhusu zana za vipimo imetolewa kwa njia rahisi ya kutumia vikombe na vijiko vya kawaida. Ø Kijitabu hiki kinasaidia watu wa mashinani Afrika kuboresha ufahamu wa kuandaa chakula cha nafaka za jamii kunde. Ø Kimetoa elimu ya utunzaji na maandalizi ya nafaka baada ya kuvuna, jinsi ya kulinda ubora wa nafaka ili kufikia viwango vilivyowekwa na viwanda hivyo kuongeza faida ya mazao na kusababisha nguvu kiuchumi na ustawi vijijini. Ø Vyombo muhimu na jinsi ya kuzitumia ili kuhakikisha ubora wa nafaka za jamii kunde baada ya kuvunwa na kabla zipelekwe sokoni pia zimeelezwa kwa kina. Ø Aidha kuna habari juu ya utungaji wa lishe ya jamii kunde hizi, jinsi ya kuzisindika ili kutoa mapishi ya thamani bora kutumia mbinu kadhaa na rahisi kutayarisha pamoja na taratibu na sheria za ugombea upishi.Item Utengenezaji wa vyakula vya kuku - Mwongozo kwa mfugaji(Rural Livelihood Development Company - RLDC, 2011)Mwongozo huu unaeleza mambo ya msingi katika kuandaa vyakula vya kuku wa rika tofauti. Kama mifugo wengine, kuku wanahitaji vyakula vyenye virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika na mwili kama wanga, protini, Madini, mafuta , vitamin na maji.Item Hatua za kuafuata katika usindikaji wa vipande vya embe kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. B; Chove, BKipeperushi kinacholezea njia ya usindikaji wa matunda na mboga mboga kibiashara.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »