Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Subject "Ghala"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Mfumo wa stakabadhi wa maghala Tanzania(Warehouse Receipts Regulatory Board, 2000)Mfumo wa Stakabadhi za Maghala ni mfumo unaotumika nchini wa kutumia bidhaa zilizohifadhiwa kwenye maghala badala ya mali zisizohamishika kuwa dhamana ya kupata mikopo kutoka asasi za fedha. Mfumo kama huu pia unatekelezwa nchi nyingine za bara la Afrika pamoja na mabara ya Ulaya na Amerika. Kwa kufuata mfumo huu wakulima wadogo na wakati wakiwa kwenye Ushirika au Vikundi vya wakulima wanakuwa na nguvu ya soko na kuingia katika soko la ushindani ambalo ingekuwa vigumu kutokana na kukosekana kwa mitaji. Pia mfumo huu unasaidia kuzuia upotevu wa mazao unaotokana na uhifadhi dhaifu, kuhifadhi mazao ili kusubiri kuuza wakati muafaka na pia kuongezea bidhaaa thamani kabla ya kuziuza.Item Mwongozo wa uendeshaji mfumo wa stakabadhi ghalani(Bodi ya Utoaji Leseni za Ghala Tanzania, 2013)Bodi ya Utoaji wa Leseni za Ghala Tanzania ni wakala ya serikali chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda. Wakala hii ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Stakabadhi Ghalani Namba 10 ya mwaka 2005. Dhamira ya Bodi ni kusimamia na kuhimiza Mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaohakikisha upataji endelevu na usio na upendeleo wa mifumo rasmi ya mikopo na uuzaji wa bidhaa, na inatarajiwa kutimizwa kwa kutekeleza kazi zake za utoaji wa leseni za biashara ya ghala, waendesha na wakaguzi wa maghala kwa kusimamia mfumo wa jumla. Katika kufanya hivyo, Bodi inakusudia kufikia dira yake ya kuwa shirika linaloongoza katika kuwaunganisha wazalishaji wa bidhaa kwenye utafutaji mikopo rasmi kwa kutumia njia yenye tija na yenye ufanisi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani. Tangu Bodi hii ilipoanzishwa, imeendelea kutekeleza kazi zake kwa kutumia muundo wa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Stakabadhi Ghalani, Kanuni za Ghala, Mwongozo wa Uendeshaji na miongozo elekezi ya mara kwa mara. Ni maoni yangu kwamba, kwa kuwa na uendeshaji wenye tija na ufanisi wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, mwongozo huu utawasaidia watendaji wakuu kupata uelewa wa jumla, maarifa, uzingatiaji wa taratibu, majukumu yao na haki katika kuendesha mfumo huu. Umetayarishwa kutokana na uzoefu, changamoto na mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chote cha uendeshaji wa mfumo kwa mazao mbalimbali na maeneo ya kijiografia nchini Tanzania.Item Uboreshaji waVihenge, Hifadhi Bora na Udhibiti wa Viumbe Waharibifu wa Mazao Ghalani(Kurugenzi ya Utafiti na Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA, 2005-01) Makundi, R. H; Misangu, R. N; Reuben, S. O. W. M; Kilonzo, B. M; Ishengoma, C. G; Lyimo, H; Mwatawala, MHifadhi bora ya mazao inahakikisha familia inakuwa na chakula cha kutosheleza mwaka mzima. Pia mazao yanaweza kuuzwa wakati wowote ili kuongeza kipato. Mradi wa hifadhi bora ya mazao na udhibiti wa viumbe waharibifu umebuniwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA),na unafadhiliwa na Programu ya FOCAL,SUA. Mradi huu unawalenga wakulima katika wilaya tatu Tanzania ambazo ni Handeni, Mvomero na Iringa Vijijini. Hifadhi bora na udhibiti wa wadudu, panya na viumbe wengine wanaoharibu mazao ghalani ni muhimu ili kuhakikisha mazao kama mahindi, kunde, maharage, mpunga, n.k. yanayozalishwa na wakulima hayaharibiwi wakati yanapohifadhiwa. Utafiti shirikishi unafanyika juu ya mbinu za asili na za kisasa ili kuboresha hifadhi ya mazao na kudhibiti viumbe waharibifu wa mazao ghalani.