Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Subject "Kilimo"
Now showing 1 - 4 of 4
Results Per Page
Sort Options
Item Masoko ya mazao ya kilimo(Sokoine university of A griculture, 2020-05-20) Mtega, WullystanMkulima anatakiwa kutafuta soko la mazao yake kabla hajaanza shughuli ya uzalishaji shambani. Ili kupata taarifa za kutosha, mkulima anashauriwa kufanya utafiti wa soko. Mkulima anaweza tumia njia kuu mbili: (i) kuandaa dodoso na kuwauliza wadau muhimu wa soko la zao alilozalisha na, (ii) kutembelea masoko ya mazao na kukusanya taarifa kwa njia ya kuona. Utafiti wa soko humwezesha mkulima kutoa maamuzi sahihi juu ya uuzaji wa mazao yake. Katika kuuza mazao, mkulima lazima azingatie sheria, kanuni na taratibu za nchi na soko husika. Pia, ni muhimu kuelewa namna nguvu ya soko inavyofanya kazi. Hii itamsaidia mkulima kujua lini ayapeleke mazao sokoni na hivyo kupata bei nzuri zaidiItem Mbinu bora za kilimo kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011-02) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. BMatunda na mbogamboga ni mazao muhimu katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, kama yalivyo muhimu katika ulimwengu wote. Mazao haya ni chanzo cha vitamini, madini, antioxidants, kambakamba za chakula and wanga ambayo ni mahitaji muhimu ya mwili. Virutubisho hivi huongeza ubora wa chakula na huzuia binadamu kupata magonjwa sugu. Hata hivyo, matunda na mbogamboga huharibika kirahisi sana na hivyo hupoteza kwa haraka sana thamani yake ya lishe na ya kiuchumi. Makadirio ya upotevu wa matunda na mbogamboga baada ya mavuno katika nchi zinazoendelea ni asilimia 40%. Hii inamaanisha kuwa katika kipindi ambacho siyo cha mavuno, kaya hukabiliwa na upungufu wa matunda na mbogamboga kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa namna ya kuhifadhi na kusindika kwa ajili ya matumizi katika mwaka mzima. Matokeo ya muda mrefu ya hali hii ni uhaba wa bidhaa iliyosindikwa katika ngazi ya chini na kutokidhi mahitaji ya viwango vya ubora kwa masoko ya ndani na nje nchi. Changamoto hizi zimeisukuma ASARECA kuwekeza katika utafiti na maendeleo katika teknolojia za mazao freshi na kuongeza thamani na mapato yatokanayo na bidhaa hizo.Item Mwongozo wa Kikundi Kuhusu Mafunzo ya Kukuza na Kuendeleza Kilimo Biashara(Vi Agroforestry, 2016) Ruto, Grace; Odhong', CharlesMWONGOZO HUU UMEANDALIWA ILI KUWEZESHA KUWAFUNDISHA wakulima katika ukuzaji wa biashara, hivyo kuwezesha wakulima wanaofanya kilimo cha kujikimu kubadilisha kutoka kulima kwa ajili ya chakula cha familia tu hadi kilimo kama shughuli ya kibiashara. Mwongozo huu una lengo la kuwapa wakulima ujuzi, mtazamo, na ustadi unaohitajika kubadilisha na kukuza biashara zao kwa namna endelevu ili ziwe biashara za kilimo zenye mafanikio. Mwongozo huu unaangazia dhana za msingi kuhusu uwekezaji, kanuni za msingi kuhusu mnyororo wa thamani, huduma muhimu za ukuzaji wa biashara, namna ya kutumia soko kwa mafanikio, usimamizi wa fedha na ujuzi wa upangaji wa biashara ulio muhimu katika kufanikiwa kwa mjasiriamali anayejihusisha na kilimo biashara.Item Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna. Kitabu na. 1(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Nafaka ni mazao makuu ya chakula ambayo hutumiwa na watanzania wote waishio mijini na vijijini. Nafaka zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko mazao mengine ya chakula na mara nyingi nafaka huzalishwa mara moja au mbili kwa mwaka. Kwa hiyo ili iweze kupatikana na kutumika kwa wakati wote ni lazima kuhifadhi. Aidha ili kuweza kuwa na bidhaa zenye thamani ni lazima kusindika. Jitihada zimekuwa zikifanywa na seikali kuongeza tija na uzalishaji wa mazao hayo. Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka. Pamoja na ongezeko la uzalishaji, teknolojia zinazotumika katika uvunaji, utayarishaji na hifadhi ni duni na husababisha upotevu mkubwa wa mazao hayo. Wastani wa tani 1,559,000 za mazao ya nafaka hupotea kila mwaka. Aidha upotevu mkubwa hutokea katika maghala kutokana na kuhifadhi nafaka ambayo haijakauka sawasawa na pia kutokana na mashambulizi ya wadudu waharibifu. Kuongeza uzalishaji pekee hakutakuwa na maana ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kupambana na matatizo yasababishayo upotevu wa mazao hayo. Teknolojia sahihi za utayarishaji wa mazao kabla ya kuhifadhi zisipotumika, nafaka itaharibika hata kama ingehifadhiwa katika ghala bora. Hivyo ni vyema kutumia njia bora za kutayarisha nafaka kama vile kukausha vyema, kusafisha na kufungasha ili kupunguza uharibifu unaosababisha upotevu wa mazao. Lengo la uandaaji wa kitabu hiki ni kuelimisha jamii kuhusu teknolojia sahihi za uvunaji, utayarishaji, ufungashaji, usindikaji na hifadhi ya mazao ya nafaka baada ya kuvuna. Aidha matumizi bora yanayokidhi mahitaji ya lishe ya mazao hayo yameainishwaili kupunguza tatizo la utapia mlo na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na kuongeza kipato. Walengwa wa kitabu hiki ni wakulima na wadau wengine ambao wamejiajiri katika sekta ya kilimo.