Chakula na Lishe
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Chakula na Lishe by Subject "Afya"
Now showing 1 - 9 of 9
Results Per Page
Sort Options
Item Chakula, lishe na saratani - vidokezo muhimu(COUNSENUTH, 2010-07)Saratani (Cancer) ni ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida. Seli hizo huweza kugawanyika bila mpangilio maalum na kuharibu mkusanyiko wa seli nyingine. Seli za saratani hutokea sehemu moja ya mwili na zinaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu na limfu (lymph). Saratani inaweza kuwa ya kurithi au kusababishwa na hali ya mazingira ya vitu mbalimbali kama vile ulaji wa vyakula vyenye visababisha saratani (carcinogenic compounds), km. nyama iliyochomwa mpaka kuungua kidogo, ulaji usio bora, pombe, uvutaji sigara au mionzi hatari, aina ya madini kama “asbestos” na “lead”. Zipo pia baadhi ya saratani zinazosababishwa na virusi kama vile saratani ya shingo ya kizazi.Item Huduma za wagonjwa majumbani: Chakula bora kwa anayeishi na VVU (MVIU), nini wajibu wa familia?(Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Tanzania., 2018)Chakula bora ni mlo kamili ulioandaliwa kutokana na mchanganyiko wa makundi matano ya chakulaItem Jinsi ya kumlisha mtoto baada ya miezi sita(Quality Assurance Project - University Research Co., LLC, 2017)Kipeperushi kinachoelezea utaarishaji wa chakula kwa watoto wanaoanza kula kuanzia miezi sitaItem Mimea muhimu kwa ajili ya chakula Tanzania(Food Plants International - FPI, 2016)This guide is based on information from the Food Plants International (FPI) database developed by Tasmanian agricultural scientist Bruce French. The source material and guidance for the preparation of the book has been made possible through the support of Food Plants International, the Rotary Clubs of District 9830, particularly the Rotary Club of Devonport North who founded Food Plant Solutions, (previously the LearnGrow project), and many volunteers who have assisted in various ways. The selection of plants included in this guide has been developed by Lyndie Kite working in a voluntary capacity using the selection criteria developed by Food Plant Solutions. These selection criteria focus on the local plants from each of the main food groups with the highest levels of nutrients important to human nutrition and alleviation of malnutrition. It is intended as a Draft Guide only to indicate some important food plants that serve as examples for this purpose. Other important nutritious plants may be equally useful, and it is recommended that the FPI database be used to source information on the full range of plants known to occur in Tanzania. This guide has been developed with the best intention to create interest and improve understanding of the important local food plants of Tanzania, and on the understanding that it will be further edited and augmented by local specialists with appropriate knowledge and understanding of local food plants.Item Tathmini ya Hali ya Lishe, Unasihi na Huduma za Lishe (NACS) - KITABU CHA MWEZESHAJI Mafunzo kwa Watoa Huduma katika Ngazi ya Jamii(Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, 2017)Lishe ina uhusiano mkubwa na afya. Lishe duni au utapiamlo unaotokana na ulaji duni na maradhi ni mojawapo ya matatizo makubwa ya afya nchini Tanzania. Utapiamlo unawaathiri zaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano na akina mama walio katika umri wa kuzaa hasa wajawazito na wanaonyonyesha. Utapiamlo kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha unaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwa watoto wao. Pia, utapiamlo unahusishwa na magonjwa sugu kama vile kifua kikuu (TB) na UKIMWI, ambayo ni matatizo makuu hapa nchini Tanzania. Upungufu wa lishe katika kipindi cha miaka miwili (siku 1,000) ya mwanzo ya maisha ya mtoto unahusishwa na maradhi, vifo na uchelewaji wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili. Upungufu huo unaweza kuathiri utendaji wa akili, matokeo ya uzazi, afya na tija ya kiuchumi wakati wa utu uzima. Watoto wachache tu wenye utapiamlo pamoja na watu wazima wametambuliwa na kutibiwa kwa kupitia vituo vya kutolea huduma ya afya. Lakini wengi wa watu hawa wakisha ruhusiwa toka vituo vya kutolea huduma ya afya baada ya kutibiwa utapiamlo huwa hawarejei tena kwa ajili ya ufuatiliaji. Watoa huduma katika ngazi ya jamii watasaidia katika kuimarisha utoaji wa huduma kati ya vituo vya kutolea huduma ya afya na jamii ili watu wenye utapiamlo waweze kutambuliwa, kutibiwa na kufuatiliwa mapema na hivyo kuboresha hali zao za lishe, kugundua dalili za utapiamlo mapema na kuepuka maambukizi. Shughuli hizi zitaimarisha mwendelezo wa utoaji wa huduma kati ya vituo vya kutolea huduma ya afya na jamii.Item Uboreshaji Lishe na Afya Kupitia Mikakati Endelevu Ya Kilimo - Mwongozo wa Kitaalam 02(CIALCA, 2010) Ekesa, BUtoaji wa makala hii ni sehemu ya mradi wa ushirikiano baina ya CIALCA na MtandaoAfya (HealthNet) TPO ujulikanayo kama “destuli endelevu za kilimo na afya kwa uimalishaji lishe na afya kwa jamii ndogondogo nchini Burundi (upande wa afya Kanda ya Gitera) na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo- DR Congo (upande wa afya Kanda ya Butembo). Makala hii imekusudiwa kutumika na wataalam kilimo, wachumi wa masuala ya nyumabani, wataalam lishe, na watumishi wa afya katika kuwajengea uwezo wawezeshaji katika jamii husika (community own resource persons) (CORPs). Matarajio kwa ujumla ni kuimalisha kiwango cha lishe miongoni mwa wanajamii kupitia destuli sahihi za ulaji na mikakati endelevu ya kilimo. Maudhui yaliyomo katika makala hii yalichambuliwa kufuatia mapungufu yaliyoonekana katika ngazi ya jamii kupitia mahojiano ya vikundi na mapitio ya kaya. Mwongozo huu kwanza unaelezea mlolongo unaojumuisha kilimo, lishe na afya. Halafu, unatoa elimu ya msingi ya lishe juu ya aina za virutubishi na vyanzo vyake katika maeneo husika. Mwongozo pia unaangalia masuala ya uhakika wa chakula, mambo yanayoathiri uhakika wa chakula na mikakati ya kuimalisha upataji chakula. Mkakati mkubwa unaosisitizwa kwenye makala hii ni uanzishaji wa bustani za mfano zitakazowezesha uanzishaji wa bustani za majumbani. Vilevile makala hii inatoa taarifa za kina juu ya uzalishaji, thamani ya chakula na mbinu za mapishi ya mazao ya vyakula yaliyobainishwa ya bustani za majumbani. Mazao husika yamebainishwa kwa kigezo cha umuhimu wake kwa jamii za afrika ya kati, mazao haya ni ndizi, viazi vitamu, maharagwe na mchicha. Pia katika makala hii kuna taarifa kuhusu usalama na usafi wa chakula.Item Uboreshaji Lishe na Afya Kupitia Mikakati Endelevu Ya Kilimo: Mwongozo wa Kitaalam 02(Healthnet TPO, 2010) Ekesa, BUtoaji wa makala hii ni sehemu ya mradi wa ushirikiano baina ya CIALCA na MtandaoAfya (HealthNet) TPO ujulikanayo kama “destuli endelevu za kilimo na afya kwa uimalishaji lishe na afya kwa jamii ndogondogo nchini Burundi (upande wa afya Kanda ya Gitera) na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo- DR Congo (upande wa afya Kanda ya Butembo). Makala hii imekusudiwa kutumika na wataalam kilimo, wachumi wa masuala ya nyumabani, wataalam lishe, na watumishi wa afya katika kuwajengea uwezo wawezeshaji katika jamii husika (community own resource persons) (CORPs). Matarajio kwa ujumla ni kuimalisha kiwango cha lishe miongoni mwa wanajamii kupitia destuli sahihi za ulaji na mikakati endelevu ya kilimo. Maudhui yaliyomo katika makala hii yalichambuliwa kufuatia mapungufu yaliyoonekana katika ngazi ya jamii kupitia mahojiano ya vikundi na mapitio ya kaya. Mwongozo huu kwanza unaelezea mlolongo unaojumuisha kilimo, lishe na afya. Halafu, unatoa elimu ya msingi ya lishe juu ya aina za virutubishi na vyanzo vyake katika maeneo husika.Item Vyakula vya afya na aina ya vinywaji mashuleni(Department of Health - Australia, 2016)Kipeperushi kinachoelezea vyakula mbalimbali pamoja na matayarisho yake kwa ajili ya kupewa watoto/wanafunzi wanapokuwa mashuleni ili viweze kuwasaidia kutokaa na njaa lakini pia kujenga afya zao.Item Zijue nafaka zenye afya zaidi(Shirika la chakula duniani, 2023-04-29) Shirika la chakula DunianiNafaka ni aina ya nyasi inayokuzwa kwa ajili ya "tunda" lake linaloweza kuliwa, linalojulikana zaidi kama nafaka.Nafaka hulimwa nyingi na hutoa virutubisho vingi zaidi vya chakula kuliko zao lolote, iwe ni moja kwa moja kwa chakula cha binadamu na kwa njia isiyo ya moja kwa moja ya malisho ya mifugo.Katika hali ya asili, nafaka ina wingi wa vitamini, madini, wanga, mafuta, na protini. Mara nyingi buckwheat na quinoa huchanganywa kama kundi la nafaka lakini ni ukweli ni kwamba hizi ni mbegu za mimea. Lakini kwa kuwa matumizi yao ya upishi yanafanana, imejumuishwa katika orodha hii