Chakula na Lishe
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Chakula na Lishe by Title
Now showing 1 - 20 of 133
Results Per Page
Sort Options
Item Baadhi ya vyakula na viungo vinavyosaidia kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya.(Taasisi ya chakula na lishe., 2018) Taasisi ya chakula na lisheWatu wanaishi na virusi vya ukimwi na wenye ukimwi mara nyingi hupata matatizo ya ulaji ,umeng'enywaji, ufyonzwaji wa chakula mwilini ,mengine ni kupoteza hamu ya kula,mafua ya mara kwa mara ,vidonda vya kooni na kuharisha.Baadhi ya vyakula na viungo hivyo tangawizi,karoti nk.Item Chakula cha Nguruwe na ulishaji(2017-02-07) Mitiki, MiTiki blog.Chakula bora kwa Nguruwe ni moja ya suala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa Nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha Nguruwe kinagharimu kama asilimia sabini ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa Nguruwe yanatokana na lishe duni. Lakini kama wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.Item Chakula dawa(Taasisi ya chakula na lishe Tanznaia, 2019-05-17) Taasisi ya chakula na lishe TanzaniaItem Chakula dawa(Sokoine university of agriculture, 2022-10-22) Taasisi ya chakula na lisheChakula dawa ni chakula kilichotengenezwa na kurutubishwa kwa nishati,vitamin na madini.Chakula hiki kimetengenezwa ma mafuta na hakihitaji kuchanganywa na maji.Chakula dawa hutumika katika kutibu utapiamlo kwa sababu huwa kina nishati,vitamin na madini kiasi kikubwa.Item Chakula tiba,maana,faida na uhifadhi wake.(Taasisi ya chakula na lishe Tanznaia, 2016-06) Taasisi ya chakula na lishe TanzaniaItem Chakula, lishe na saratani - vidokezo muhimu(COUNSENUTH, 2010-07)Saratani (Cancer) ni ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida. Seli hizo huweza kugawanyika bila mpangilio maalum na kuharibu mkusanyiko wa seli nyingine. Seli za saratani hutokea sehemu moja ya mwili na zinaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu na limfu (lymph). Saratani inaweza kuwa ya kurithi au kusababishwa na hali ya mazingira ya vitu mbalimbali kama vile ulaji wa vyakula vyenye visababisha saratani (carcinogenic compounds), km. nyama iliyochomwa mpaka kuungua kidogo, ulaji usio bora, pombe, uvutaji sigara au mionzi hatari, aina ya madini kama “asbestos” na “lead”. Zipo pia baadhi ya saratani zinazosababishwa na virusi kama vile saratani ya shingo ya kizazi.Item Cookery Book: The Tanzanian way(1995) White, CKaribu I would first of all like to thank all those who wrote to Anna with the recipes and quickly remind all those with good intentions to send more as the recipes can be added at a later date. So, thanks go to VSOs in Bukoba, Babati, Moshi, Morogoro, Dar, Marangu…. This book's objective is to make life (and what is life without food!) a little more interesting in the kitchen and on the table. Of course, there are many variations and a lot of the time it is enjoyable to just experiment with what you have in the cupboard. I would like to remind you that there are many easy recipes in the Baby Belling Cook Book and, don't forget, the Pressure Cooker Cook Book. Also, it is always handy to know other people with cook books to borrow! The recipes on the whole have been tried and tested and given the OK before getting in the book. The recipes which are scrummy and impressive I have coded as BHC -British High Commission. I thought it would be useful to know which ones may help you to influence and enable you to ask for funds! What I would like to suggest is that whenever you are in the big cities, hunt out the herbs and spices shops and also the wazungu shops. Here you can top up on the essentials for interesting cooking. You can also ask visitors to bring in those difficult to get hold of herbs and spices and, of course, there is always the post!Item Dagaa-faida 5 za dagaa(BBC swahili, 2021) BBC swahiliDagaa, ni chakula maarufu duniani, kwa ukanda wa afrika Mashariki ni kitoeo maarufu na mara nyingi kutumiwa kama mboga ya kula na wali ama ugali. Kuna aina nyingi za dagaa, kuanzia wanaotoka baharini hadi ziwani. Mtaalamu wa lishe aliyesajiliwa Nicola Shubrook anatuambia kama dagaa ni nzuri na ni faida gani za lishe tunazoweza kutarajia kutokana na kuzitumia.Item Daily Mail(daily industry in Africa, 2007-01-12) Slabbet, Karienvery minute of every day, some where in the world 21 children die of Malnutrition and preventable diseases it is a given party that sustainable school milk programs can help alleviate hunger, while at the same time building a future consumer base.Item Dawa za asili za kuotesha nywele na kuondoa upara(Zenji Shoppers, 2016)Kiepeperushi kinachoelezea vyakula na bidhaa ambazo zikitumika zinaweza kusaidia kukuza nywele na kuondoa upara katika kichwa.Item Elimu ya Lishe: Matumizi ya viazi vitamu - MWONGOZO WA MAFUNZO Kwa Walimu wa shule za Msingi(2016) Nkuba, D. E. M; Bundala, N. HUtapiamlo ni miongoni mwa matatizo makubwa ya kiafya ambayo yanaathiri watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wanaonyonyesha, kutokana na mahitaji yao kilishe kuwa makubwa. Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, mamilioni ya watoto na kinamama wanaendelea kupata matatizo yatokanayo na lishe duni yakiwemo, uzito mdogo, udumavu, ukondefu, upungufu wa vitamini A, upungufu wa madini joto na upungufu wa wekundu wa damu (anemia). Utapiamlo husababisha ukuaji duni kimwili na kiakili na vifo vingi miongoni mwa watoto wadogo nchini Tanzania. Huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa umaskini katika jamii, kwani hupunguza nguvu kazi kutokana na magonjwa, hivyo hupelekea kupungua kwa uzalishaji mali. Sababu ya karibu inayosababisha utapiamlo nchini ni ulaji duni na maradhi. Sababu zilizojificha ni pamoja na upungufu wa uhakika wa chakula katika kaya, upungufu katika utunzaji wa makundi maalum mfano; watoto, wajawazito, nk. na upungufu wa huduma za kimsingi za binadamu mfano elimu, afya, maji, nk. Sababu za msingi ni elimu duni; mfumo wa siasa, itikadi na uchumi; mila na desturi. Kwa sasa jitihada za kutatua matatizo ya lishe nchini zimeelekezwa zaidi katika sekta ya afya, zikijumuisha chanjo, utoaji madawa na virutubishi katika vyakula. Zipo njia nyingine za kutatua tatizo la utapiamlo kama utumiaji wa vyakula vyenye virutubishi mbalimbali na elimu ya lishe lakini bado havijatiliwa mkazo unao stahili. Kuna uhitaji wa sekta mbalimbali kushirikiana katika kutatua tatizo la utapiamlo. Mwongozo huu umetengenezwa kuwawezesha walimu wa shule za msingi na watumishi katika ngazi ya jamii kutumia elimu ya lishe kupitia vyakula katika kutatua tatizo la utapiamlo. Chakula kitakachopewa kipaumbele katika Mwongozo huu ni viazi vitamu na bidhaa zake. Viazi vya rangi ya chungwa, hutumika kuondoa tatizo la upungufu wa vitamini A na vitamini nyingine pamoja na utapiamlo. Viazi vitamu vyote vina viinilishe vya vitamini C, E, K, pamoja na kundi la vitamini B, lakini viazi vya rangi ya chungwa vina vitamini A zaidi. Kulingana na tafiti zilizofanyika, kiasi cha gramu 125 (nusu kikombe cha chai) za viazi vilivyochomwa au kuokwa zina uwezo wa kukidhi mahitaji ya vitamini A ya watoto na kinamama ambao wanamahitaji makubwa ya kimwili ya vitamini A kwa siku. Matumizi ya viazi vya rangi ya chungwa na majani yake kutaimarisha lishe na usalama wa chakula katika kaya na pia kunaweza kuzalisha kipato cha ziada katika kaya.Item Fahamu kuhusu kilimo cha pilipili mbuzi(WIZARA YA KILIMO, 2018) WIZARA YA KILIMOPilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha masaa 6 kwa siku. Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji. Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa PH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefka 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.Item Faida 20 Mwilini za kula Bamia(Global, 2024-10-03) GlobalpublishersJAPOKUWA bamia huchukuliwa na wengi kuwa ni chakula rahisi kinachotumiwa zaidi na kundi la watu wenye uchumi wa chini na kati, ukweli kwamba aina hiyo ya mboga ina maajabu ya aina yake mwilini. Walaji wa bamia hunufaika kwa kupata utitiri wa viinilishe vilivyomo kwenye zao hilo, ambavyo humpatia mlaji faida za kiafya takribani 20Item Faida ya mafuta yatokanayo na mazao ya mbegu(Wizara ya kilimo, 2003) Wizara ya kilimo Tanzania, wizara ya kilimo TanzaniaFaida ya mafuta yatokanayo na mazao ya mbeguItem Faida za chai katika kupambana na magonjwa(Shirika la chakula duniani, 2024-05-30) Shirika la chakula dunianiKuna faida za kiafya za kunywa chai ambazo labda huzijui. Chai ni mojawapo ya vinywaji vinavyotumiwa sana duniani na imekuwa ikitumiwa kwa karne nyingi. Kuna aina tofauti za chai; nyeusi, kijani, nyeupe na rangi zingine. Kila moja ina ladha yake ya kipekee na sifa na aina ya jani la chai na usindikaji wake.Mei 21 pia huadhimishwa kama Siku ya Chai Duniani. Je, chai ina faida gani kwa afya ya binaadamu?Item Faida za kiafya za embe mbichi.(Sokoine university of agriculture, 2023-11)Lakini je! Unajua kuwa maembe mabichi au yasiyokomaa pia yana faida kubwa kiafya? Kachchi kairi au embe mbichi huzaa Vitamini C kama tufaha 35, ndizi 18, ndimu tisa na machungwa matatu, inasema utafit Mbali na vitamini, pia hubeba chuma na zaidi ya asilimia 80 ya magnesiamu na kalsiamu inayohitajika kila siku. Maembe mabichi huliwa vizuri bila kupikwa kwani virutubisho vingi kama vitamini C vitapotea wakati wa mchakato wa kupika.Leo, tutaangalia faida za kula embe mbichi au kijani inaweza kuwa na afya yakoItem Faida za kiafya za Mayai(Uly Clinic, 2020-04-05) Uly ClinicMayai ni aina ya chakula muhimu kwa binadamu, huwekwa kwenye kundi la vyakula vyenye protini. Mbali na kuwa na protini mayai ni chanzo kizuri cha vitamini A, B, B12 na D, kolesto kwa wingi na madini ya lutein na zeaxanthin . Yai huweza kuliwa likiwa bichi, kuchemshwa au kukaangwa. Kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula, yai hupoteza virutubisho linapochemshwa kwa muda mrefu au kukaangwa. Vitamin D kwenye yai hupungua kwa kiwango kikubwa endapo yai litapikwa kwa muda mrefu. Hata hivyo kuchemsha au kukaanga yai kwa muda mrefu hupunguza kwa asilimia kwa asilimia 90 hivyo kupoteza umuhimu wake katika mwiliniItem Faida za kiwi kama tunda(Sokoine university of agriculture, 2021-03-11) medicover hospitalKiwifruit kwa ujumla hukua mviringo na ni sawa na yai ya kawaida ya kuku. Ngozi yao ina rangi ya caramel, nyuzinyuzi, na kufunikwa na fuzz nyepesi. Licha ya mipako yake ya fuzzy, ngozi ya kiwi ni chakula na tindikali. Ni matunda madogo ambayo yana ladha nyingi na faida nyingi za kiafya. Massa yake ya kijani ni tamu na siki. Pia ina vitamini C nyingi, vitamini K, vitamini E, folate, na virutubishi vya potasiamu. Pia wana antioxidants nyingi na ni chanzo kizuri cha nyuzi. Mbegu zake ndogo nyeusi zinaweza kuliwa, sawa na ngozi ya kahawia isiyo na rangi, ingawa wengi hupenda kumenya kiwi kabla ya kula. Kiwi inaweza kuwa katika msimu mwaka mzima. Hupandwa California kuanzia Novemba hadi Mei na New Zealand kuanzia Juni hadi Oktoba. Inawezekana pia kupata kiwi katika fomu ya ziada.Kiwi ya kijani ya Hayward ni aina maarufu zaidi ya kiwi kwenye masoko. Mwingine ni kiwi ya dhahabu. Kiwi za dhahabu zina ngozi ya shaba na kofia iliyoelekezwa upande mmoja. Ladha ya kiwi ya kijani wakati fulani hufafanuliwa kuwa mchanganyiko wa sitroberi, ndizi, na nanasi. Kiwi ya dhahabu ina massa ya njano ambayo haina asidi kidogo kuliko kiwi ya kijani na ina ladha ya kitropiki.Item faida za mboga za majani na matunda(Ukulima wa kisasa, 1989-07)Mboga na matunda ni muhimu kwa ajili ya miili yetu.Hutupatia vitamini na madini,viini ambavyo hulinda miili yetu isishambuliwe na magonjwa pamoja na kujenga na kuimaiisha meno na mifupa.Item FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO(Mzizi Mkavu Blog, 2006-02) Katuma BlogMchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu. Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana aida kubwa kiafya. Mafuta vya mchaichai hutumika katika viwanda vinavyotengeza pafyumu na sabuni. Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupamban ana athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Wengine huamini kuwa mchaichai huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli. Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa.