Chakula na Lishe
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Chakula na Lishe by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 133
Results Per Page
Sort Options
Item faida za mboga za majani na matunda(Ukulima wa kisasa, 1989-07)Mboga na matunda ni muhimu kwa ajili ya miili yetu.Hutupatia vitamini na madini,viini ambavyo hulinda miili yetu isishambuliwe na magonjwa pamoja na kujenga na kuimaiisha meno na mifupa.Item Manufaa ya kilimo bora cha maboga(Ukulima wa kisasa, 1990-07) Magembe, AMaboga ni zao la chakula ambalo hulimwa katika sehemu nyingi nchini Tanzania, lakini kwa kiasi kidogo kidogo sana, aghalabu hua linapandwa katika mashamba ya mahindiItem Maziwa ya mama(Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, 1992-10-17) Kisanga, P.; Mella, O.; Masako, R.; Navetta, D.Kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kimojatu kati ya vijitabu kumi vinavyotolewa aa Shirika la Chakula na Lishe Tanzania kutokana na barua za wasikilizaji wa vipindi vya redio vya "Chakula na Lishe". Vijitabu hivi ni: 1. Ujauzito 2. Maziwa ya Mama 3. Ulikizaji 4. Ukuaji wa mtoto 5. Kuharisha 6. Surua 7. Anemia 8. Upungufu wa Vitamini A· 9. Upungufu wa Madini ya joto 10. Muhogo Kila kijitabu kina maswali 10 tu na kijitabu kitakachofuaria katika fani moja kitaendeleza idadi ya maswali. Vijitabu hivi vinafaa sana kusomwa na wanafunziwa shule za msingi na sekondari na watu wote vijijini na mijini wanaopenda kuelewa zaidikuhusu Lishe bora. Mara kwa mara Shirika la Chakula na Lishe litatoa zoezi katika redio au gazeti la kiswahili kwa ajili ya watu wa vikundi mbali mbali na atakayepata alama nyingi atazawadiwa.Item Zuia upungufu wa wekundu wa damu(TFNC Readers series, 1994) Maganga, S.Mwili wa binadamu unahitaji maji na virutubisho vya aina mbali mbali. Virutubisho hivyo ni vile vya aina ya nishati, utomwili, madini na vitami-ni. Vyote hivi huhitajika katika kulinda na kujenga mwili ikiwa ni pamojana kutengeneza damu na kuupa mwili nguvu. Upungufu wa virutubishohivi ukitokea huweza kusababisha upungufu wa wekundu wa damu.Item Zuia upungufu wa vitamini A(Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, 1994-04-14) Missano, H.; Temalilwa, C. R.; Maganga, S.Kijitabu hiki ni kimojawapo kati ya vijitabu vyenye lengo la kuelimisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya lishe. Wazo la kuandika kijitabu hiki limetokana na ukweli kwamba hakuna maandiko ya kutosha yanayohusu elimu ya lishe kwa wananchi. Vile vile uandishi wa kijitabu hiki umelenga kutoa fursa kwa jamii iweze kuelewa na kutafakari matatizo yake ya kiafya na kilishe hasa ya upun gufu wa vitamini A. Maudhui yaliyotumika ni rahisi na yanayoeleweka. Hivyo ni matarajio ya Wizara ya Afya kuwa maandiko haya iwapo yatasomwa na kutekelezwa yatachangia kuinua afya na lishe ya jamii.Item Upungufu wa madin ya joto mwilini(Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, 1994-08-13) Kimboka, Dr. SabasUpungufu waa madini ya joto mwilini ni tatizo kubwa la kiafya hapa Tanzania. Idadi ya watu wanaoathirika inakadiriwa kuwa milioni 5.6 au asilimia 25 ya watu wote. Madini ya joto hupatikana ardhini na huchukuliwa na aina zote za viumbe (mimea, wanyama) na maji, vinavyopatikana katika eneo hilo. Kupitia katika vyakufa madini hayo huingia kwenye mwili wa binadamu. Kutokana na mlolongo huo iwapo ardhi ya eneo fulani ina upungufu wa madini ya joto binadamu nao kupungukiwa na hatimaye kupatwa na madhara. Sababu za upungufu wa madini ya joto ni zaidi ya moja, lakini kubwa na ya muhimu niile ya kijiografia. Sehemu za miinuko, kwa miaka mingi tangu kuumbwa kwa dunia, zimepoteza madini ya joto ambayo huchukuliwa na maji (mvua, mito, mafuriko n.k.) na kupelekwa nyanda za nchini yaani bondeni, baharini na kwenye maziwa. Nd'iyo maana tatizo ni kubwa sana katika mikoa yenye miinuko na siyo katika ukanda wa pwani.Item Upungufu wa wekundu wa damu (Anaemia)(Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, 1994-10-11) Maganga, S. J.; Kimboka, S.; Tatala, S.; Mduma, B.; Ballart, A.; Temalilwa, C. R.; Missano, H. M.; Kisanga, P.; Magalia, A. W.; Ng'wawasya, B. M.; Kayombo, J. K.; 5imonje, L. W.; Ndossi, G. D.; Rwebangira, C. G.; Kayombo, L. C.; Ntoga, B. A.Upungufu wa wekundu wa damu ni moja ya matatizo sugu ya utaptamlo yanayoathiri watu na kusababisha vito vingi hapa Tanzania. Kutokana na takwimu zilizopo Shirika la Chakula na Lishe Tanzania, inakadiriwa kuwa asilimia 32 ya watu milioni 23 (Sensa ya mwaka 1988) wanaathirika. Wanaoathirika zaidi ni wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa wanawake wajawazito wanaoathirika ni asilimia 80 na watoto chini ya umri wa miaka mitano ni asilimia 45. Tatizo la upungufu wa wekundu wa damu hutokana na sababu nyingi zikiwemo ulaji duni yaani kutokula chakula cha mchanganyiko na cha kutosheleza mahitaji ya mwili. Magonjwa mbalimbali hasa malaria na minyoo ni chanzo kimojawapo cha tatizo. Vile vile uzazi wa karibu karibu huchangia upungufu wa wekundu wa damu. Tatizo la upungufu wa wekundu wa damu hapa nchini limeenea zaidi sehemu ambazo magonjwa ya safura, malaria na kichocho hujitokeza kwa wingi. Kitabu hiki kina lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea wataalam wa ugani na viongozi katika ngazi ya wilaya, kata na kijiji ujuzi, maarifa na uwezo wa kuelewa chanzo, dalili na athari za upungufu wa wekundu wa damu katika jamii. Maarifa haya yatawawezesha kuishirikisha jamii katika kuchunguza, na kupima ukubwa wa tatizo, kufanya uchambuzi wa kina wa tatizo na kubuni mbinu za kulitatua. Kitabu kina sura tano. Sura ya kwanza inazungumzia dhana ya utapiamlo na jinsi inavyotumika katika kuchanganua tatizo la upungufu wa wekundu wa damu. Sura ya pili inaelezea umuhimu wa madini ya chuma, vitamini aina ya folic acid na B12 katika mwili wa binadamu na madhara yatokanayo na upungufu wake. Sura ya tatu inaelezea dalili na athari za upungufu wa wekundu wa damu. Sura ya nne inaelezea mbinu za kukabili tatizo la upungufu wa wekundu wa damu na sura ya tano inaelezea majukumu na wajibu wa jamii katika ngazi mbalimbaliItem Cookery Book: The Tanzanian way(1995) White, CKaribu I would first of all like to thank all those who wrote to Anna with the recipes and quickly remind all those with good intentions to send more as the recipes can be added at a later date. So, thanks go to VSOs in Bukoba, Babati, Moshi, Morogoro, Dar, Marangu…. This book's objective is to make life (and what is life without food!) a little more interesting in the kitchen and on the table. Of course, there are many variations and a lot of the time it is enjoyable to just experiment with what you have in the cupboard. I would like to remind you that there are many easy recipes in the Baby Belling Cook Book and, don't forget, the Pressure Cooker Cook Book. Also, it is always handy to know other people with cook books to borrow! The recipes on the whole have been tried and tested and given the OK before getting in the book. The recipes which are scrummy and impressive I have coded as BHC -British High Commission. I thought it would be useful to know which ones may help you to influence and enable you to ask for funds! What I would like to suggest is that whenever you are in the big cities, hunt out the herbs and spices shops and also the wazungu shops. Here you can top up on the essentials for interesting cooking. You can also ask visitors to bring in those difficult to get hold of herbs and spices and, of course, there is always the post!Item Maelezo ya msingi kuhusu mti wa mlonge (Moringa Oleifera)(Bustani ya Tushikamane, 2000)Moringa (Moringa spp.) maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji.Item Mafunzo ya mpango wa huduma za chakula katika shule za msingi tanzania(Wizara ya elimu, 2000-03-12)Kitabu boo kimetayarishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa viongozi wanaohusika na utekelezaji wa mipango ya huduma za chakula cha mchana katika shule za msingi. Watakaoshirikishwa katika mafunzo hayo kwenye ngazi mbalimbali ni kama ifuatavyo: (a) Waratibu wa Sayansi Kimu wa Wilaya ambao watawajibika kuwafun disha walimu wakuu wa shule za msingi amoja na Waratibu Tarafa na Kata wa Elimu ya Watu Wazima, (b) Walimu Wakuu watawafundisha walimu wengine wa shule za msingi. Walimu wa shule za msingi na Waratibu Tarafa na Kata na Elimu ya Watu Wazima watafundisha wFzi na viongozi wa vijiji.Item Unyonyeshaji bora wa maziwa ya mama(Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya - COUNSENUTH, 2003)Kunyonyesha ni tendo la kumpa mtoto maziwa kutoka katika titi la mama moja kwa moja au kumnywesha mtoto maziwa ya mama yaliyokamuliwa kwa kutumia kikombe. Maziwa ya mama ni chakula na kinywaji cha kwanza, na cha pekee kwa mtoto tangu azaliwapo mpaka kufikia umri wa miezi sita. Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto mchanga kuliko maziwa mengine au chakula kingine chochote. Mtoto afikishapo umri wa miezi sita apewe vyakula vingine laini vya nyongeza huku akiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama hadi kufikia miaka miwili au zaidi. Kwa jamii ya Kitanzania unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni kitu cha kawaida. Zaidi ya asilimia 98 ya wanawake huwanyonyesha watoto wao, na wengi wao huendelea kuwanyonyesha hadi kufikia umri wa miaka miwili au zaidi. Pamoja na jitihada za wanawake wengi kunyonyesha watoto wao, zipo kasoro ambazo hujitokeza na kuwafanya wanawake hawa wasiweze kunyonyesha kikamilifu, na hivyo kufanya wengi wao pamoja na watoto wao wasifaidike kikamilifu na faida za unyonyeshaji. Kijitabu hiki kina taarifa muhimu kwa jamii, ambazo zitasaidia mama aweze kunyonyesha kikamilifu. Kimekusudiwa kutumiwa na jamii, ikijumuisha wazazi (baba na mama), walezi, vikundi katika jamii vinavyoshughulikia afya ya mama na mtoto, na yeyote anayependelea kufahamu kuhusu afya, lishe na ulishaji wa watoto wadogo.Item Pesti ya nyanya(TARP-Sua, 2003) TARP II-SUA ProjectNyanya ni moja ya mazao ya mbogamboga muhimu Tanzania hususan katika wilaya ya Muheza. Zao la nyanya humwongezea mkulima kipato na kuboresha lishe ya mlaji. Pamoja na faida zake hizi. zao la nyanya ni la msimu na linakabiliwa na matatizo mcngi likiwemo la kuharibika haraka mara tu baada ya kuvunwa. llali hii pia humlazimisha mkulima auze nyanya zake haraka na kwa bei ya chini ambayo humpunguzia kipato. Wakulima wa Muheza kama walivyo wakulima wa sehemu nyingine Tanzania hawasindiki nyanya zao kwa sababu hawana ujuzi huo. Kijitabu hiki kimetayarishwa ili kumsaidia mkulima au mtu yeyote mwingine kusindika pesti ya nyanya na kuhifadhi katika chupa kwa ajili ya matumizi ya baadaye.Item Faida ya mafuta yatokanayo na mazao ya mbegu(Wizara ya kilimo, 2003) Wizara ya kilimo Tanzania, wizara ya kilimo TanzaniaFaida ya mafuta yatokanayo na mazao ya mbeguItem Uhifadhi wa nyama kwa njia ya kukausha kwa kutumia mionzi ya jua na moshi wa kuni(Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, 2003) Mtenga, L.AMradi wa uboreshaji wa mauzo, uhifadhi na ulaji wa nyama vijijini unafadhiliwa na Serikali ya Norway kupitia shirika lake la maendeleo (NORAD) chini ya mradi mkubwa wa Uhakika wa Chakula na Palo la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania (TARP 11 - SUA). Mradi huu unacndeshwa katika ukanda wa mashariki ya Tanzania katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Watafiti wanatoka Chuo Kikuu cha Sokoinc cha Kilimo na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula. Kwa kuanzia kuna vijiji vitatu vinavyoshiriki katika mradi huu; Chamakweza (Chalinze) katika mkoa wa Pwani, Mnjilili na Nyumbanhitu (Gairo) katika mkoa wa Morogoro. Kijarida hiki kimeandaliwa ili kitumike katika uenezaji wa mbinu mbalimbali zinazohusika na mradi. Hizi ni pamoja na njia za maandalizi ya mwanzo, matayarisho (kukausha kwa kufukiza moshi na kutumia mionzi ya jua) na kuhifadhi nyama iliyokaushwa.Item Mazao ya jamii ya mizizi(chuo cha kilimo cha Sokoine, 2003-06) Shetto, M.C.Wanawarsha pia waliorodhesha mazao ya jamii ya mizizi ili kuelewa aina za mazao haya. Aina tano za mazao ya jamii ya mizizi yaliorodheshwa nayo ni: Muhogo, Viazi vitamu, Magimbi, Viazi vikuu, Viazi mviringo, angawizi na Karoti. Wanawarsha walikubaliana kuwa mazao ya jamii ya mizizi ambayo wakulima wengi wanalima ni matano na hayo yakapcwa kipaumbele kwa kutumia mbinu ya mlinganisho joziItem Mapishi bora(Sokoine university of agriculture, 2004) Kinabo, J.LMfumo wa ulaji unaotumika katika vijiji hivi umegawanyika katika sehemu tano ambazo ni: Baba kula pamoja na watoto wa kiume bila kubagua umri. Mama kula peke yake Mama kula na watoto wa kike bila kubagua umri Watoto wa jinsia zote kula pamoja bila kubagua umriItem Lishe Wakati wa Ujauzito na Kunyonyesha - Vidokezo muhimu(Quality Assurance Project, 2005)Wakati ukiwa mjamzito au unanyonyesha mwili wako unahitaji mlo kamili ambao hutokana na kula vyakula vya aina mbalimbali. Vyakula mbalimbali kila siku husaidia kuhakikisha kuwa unapata nishati na virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini mwako pamoja na mahitaji ya mtoto.Item UHUSIANO WA UHAKIKA WA CHAKULA, UKIMWI NA LISHE BORA: Warsha ilifanyika Makambako - Njombe Tarehe 30 Novemba - 04 Desemba 2004(TARP II-SUA Project, 2005-02) Lyimo, C. S; Malimbwi, R. E; Lyimo-Macha, J. G; Macha, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH) wakishirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), wamekuwa wakitekeleza mradi wa "Uhakika Wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo" (TARP II - SUA Project). Mradi ulianza mwaka 2000 na unagharamiwa na Serikali ya Norway pamoja na serikali ya Tanzania. Madhumuni ya warsha hii yanalenga kuleta ushirikiano wa karibu kati ya wakulima wadogo wadogo ngazi ya kaya, wagani, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na watafiti wa kilimo na mipango katika kuinua uwezo wa maisha ya mtanzania katika ngazi ya kaya; kiuchumi, kiafya na maendeleo kwa ujumla. UKIMWI ni tatizo kubwa linatishia kuwepo kwa binadamu. UKIMWI hauishii kumuua muathirika na kupoteza nguvu kazi tu, lakini pia jamii ya muathirika huathirika kwa narnna moja au nyingine. Nguvu kazi ya muathirika hupotea kwa ajili ya kumuuguza mgonjwa; fedha nyingi hutumika kwani mgojwa anahitaji chakula maalum na dawa; watoto hukosa huduma ya wazazi na hivyo kushindwa kusoma au kupata lishe bora; mgonjwa anapofariki kuna gharama za mazishi na nguvu kazi-hupotea kuhudumia misiba. Warsha ililenga kubaini mtazamo wa jamii kuhusu athari za UKIMWI katika uhakika wa chakula na kukuza elimu ya UKIMWI na lishe bora kwa kutumia wataalamu walioshiriki.Item Mapishi: Vyakula vinavyozalishwa katika mkoa wa Morogoro(TARP II - SUA PROJECT, 2005-02-09) Kinabo, Prof. J. L.; Mnkeni, Dr. A.; Nyaruhucha, Dr. C.; Msuya, Dr. J.; Chale, Bi. F.Mfumo wa ulaji unaotumika katika vijiji hivi umegawanyika katika sehemu nne ambazo ni: 1. Baba kula pamoja na watoto wa kiume bila kubagua umn 2. Mama kula peke yake 3. Mama kula na watoto wa kike bila kubagua umri 4. Watoto wa jinsia zote kula pamoja bila kubagua umri Pamoja na mfumo huu wa ulaji bado kuna athari zitokanazo na utayarishaji mbaya wa chakula ambao ni pamojana kutokula vyakula vya mchanganyiko kutoka mafungu makuu matatu ya chakula. Mahmgu hayo ni vyakula aina ya nafaka/mizizi vinavyotia nguvu mwilini tuweze kufanya kazi za nguvu kama kulima, kutembea mwendo mrefu, kukokota plau/kuendesha trekta, kubeba zege n.k. Vyakula hivyo ni pamoja na nafaka kama mahindi, ulezi, mtama, ngano na mpunga na mizizi ni kama muhogo, viazi vitamu, viazi mviringo, magimbi, viazi vikuu, n.k.. Vyakula vya protini hujenga miili yetu kwa maana ya kurudishia upya sehemu zinazochakaa, kwa mfano misuli kwa watu wazima, kucha, kidonda kupona na kufunga haraka tunapopata majeraha. Kwa upande wa watoto wadogo ambao bado wanakua huwasaidia wakue haraka, Vyakula hivi vimegawanyika katika aina mbili: vile vya asili ya nyama ambavyo ni nyama, samaki, maziwa, mayai na wanyama wa porini, na vile vya asili ya mimea, ni kama maharage, choroko, kunde, mbaazi. njegere na njugu mawe. Vyakula vingine ni kundi la mbogamboga na matunda. Hivi husaidia miili yetu isishambuliwe na maradhi. Vyakula hivyo ni majani ya kunde, majani ya maboga, kisamvu, bamia, karoti, mchicha, mwidu, delega, mnavu, n.k. Matunda ni pamoja na mapapai, mapera, machungwa, embe mafuta n.k. na yale ya asili kama ukwaju, ubuyu, n.k.Item FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO(Mzizi Mkavu Blog, 2006-02) Katuma BlogMchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu. Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana aida kubwa kiafya. Mafuta vya mchaichai hutumika katika viwanda vinavyotengeza pafyumu na sabuni. Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupamban ana athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Wengine huamini kuwa mchaichai huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli. Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa.