Matumizi Bora ya Ardhi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Matumizi Bora ya Ardhi by Subject "Amani"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Hifadhi ya Asili ya Amani Tanzania: Miradi ya Equator Wanavijiji na Maendeleo Himili ya Jamii(Equator Initiative: Environment and Energy Group - United Nations Development Programme - UNDP, 2012)Hifadhi ya Asili ya Amani ilitangazwa kisheria na Serikali ya Tanzania katika gazeti la serikali mwaka 1997, ikiwa na lengo la kuihifadhi bayoanuwai ya Milima ya Usamabara Mashariki. Safu ya Mashariki ya Milima ya Usambara imeorodheshwa kama kituo cha kimataifa cha bayoanuwai ya mimea na inajivunia kuwa ya pili kwa kuwa na aina nyingi za mimea katika bara la Afrika. Pia ilitangazwa na UNESCO kuwa Hifadhi ya Binadamu na Viumbe hai, mwaka 2000. Hifadhi hii ya viumbe hai yenye eneo la takribani hekta 83,600 inajumuisha misitu ya mvua na ardhi ya nyasi na miti ya uwanda wa chini. Ina sifa ya kuwa na mimea mingi iliyo katika hatari ya kutoweka (ikiwemo mimea mingi ya madawa) na ni makazi ya zaidi ya aina kumi na tatu za ndege wasiopatikana mahali pengine. Pia misitu hii mikuu hutoa maji kwa wakazi zaidi ya 300,000 katika mji wa Tanga, na wenyeji wa milimani wanategemea misitu hii kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaisha.