Matumizi Bora ya Ardhi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Matumizi Bora ya Ardhi by Title
Now showing 1 - 20 of 51
Results Per Page
Sort Options
Item Acaccia(Sokoine university of agriculture, 2023-09-16) sarmiento, lourdesAcacia ya Constantinople Ni mti wa asili katika bara la Asia . Inaweza kupima hadi mita12, ingawa ni nadra kwake kuzidi mita 6-7 katika kilimo. Haina ukuaji wa haraka sana au polepole sana, badala yake kiwango cha ukuaji ni cha kati. Katika maeneo yenye upepo inahitaji kuwa chini ya mkufunzi kwa angalau mwaka mmoja au miwili, kwani shina linaweza kuvunjika kwa urahisi, haswa ikiwa mfano ni mchanga. Unaweza kutumia logi ya kuni ambayo unaweza kuzika karibu na mfano mdogo au tumia zabibu ya chuma isiyo nene sana. Kwa kamba kidogo itakuwa sawa.Item Athari za mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi wa Zanzibar: Muhtasari wa Ripoti ya mwisho 2012(Serikali ya Mapinduzi Zanzibar - SMZ, 2012)Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini ya athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi kwa visiwa hivi,njia muhimu za kuweza kukabiliana nazo na fursa ya kupunguza ongezeko la hewa mkaa.Utafiti huu umegundua matokeo muhimu yanayofafanuliwa kama ifuatavyo hapa chini. Uchumi wa Zanzibar unategemea sana tabianchi na sehemu kubwa ya Pato la Taifa, ajira na maisha yanahusiana na shughuli zinazotokana na tabianchi (za pwani, kilimo na utalii). Tabianchi ya Zanzibar imebadilika katika miongo ya hivi karibuni.Tumeshuhudia ongezeko la joto, mvua zisizotabirika,upepo mkali na bahari kupanda juu.Aidha, pia kuna ongezeko la matukio mengi makubwa ( tafauti ya tabianchi).Jambo hili la mwisho limesababisha ukame na mafuriko ambayo yameleta gharama kubwa za kiuchumi kwa Pato la Taifa. Matukio ya namna hii yanaonekana kuongezeka. Aidha, ni wazi kuwa Zanzibar bado haijaweza kukabiliana ipasvyo na tabianchi iliopo na kuna haja ya kuchukuwa hatua za haraka ambazo zinaweza kuleta faida kubwa za kiuchumi katika kushughulikia kasoro za kukabiliana na hali iliopo.Item Cascade bonsai(Sokoine university of agriculture, 2023-09-23) Arcoya, EncarniBonsai ya maporomoko ya maji kwa kweli ni mti mdogo unaojulikana na ukweli kwamba shina limeinama kuelekea msingi wa sufuria., kwa namna ambayo matawi na majani yanakua chini, na kufanya sufuria hizi zinapaswa kuwa katika maeneo yajuu kwa sababu matawi mengi ni marefu kuliko sufuria na yanahitaji nafasi kwa urefu.Ni moja ya vielelezo nzuri zaidi kwenye soko, lakini pia ni ngumu kupata, kwani zinahitaji mkonowa mwanadamu kufikia sura hiyo (mara nyingi) na kupata bonsai "kuuza" ni muhimu kwamba miaka kadhaa ipite. .Kati ya hizi, kuna aina mbili ambazo unapaswa kuzingatia: Bonsai ya maporomoko ya maji: Ni bonsai nzuri zaidi, kwani shina huanguka kwenye msingi wa sufuria na ukuaji hutokeachini, na baadhi ya matawi na majani hufuata mwanga (juu). Bonsai ya nusu mteremko:Hizi ndizo rahisi zaidi kupata, lakini hiyo haimaanishi kuwa ni za bei nafuu. Zinatofautiana na zingine kwa kuwa kuanguka kwa mti hakutamkiwi kama kwenye maporomoko ya maji na huwafanya kuwa na umbo la mwelekeo kidogo. Lakini zaidi kidogo.Item Efficient utilisation of river valleys - experiences from mbarali(TARP II Project - SUA, 2002) Batamuzi, E. K; Tarimo, A. J. PIn the Southern Highlands zones, within zone exchange visit was carried out from April 14 to 19, 2002. In this visit, farmers, extension agents and researchers from Kyela rice growing areas visited their counterparts in the Usangu plains to exchange experiences in ric.ecultivation and other agricultural enterprises being carried during the year. The theme of the visit was "Efficient Utilization of River valleys", a concept aimed at improving awareness of rice producing farmers in land and water management, including cropping systems and their interaction with livestock production systems. It is well understood that land and water are necessary resources for agricultural production. These essential resources have often led to wars between tribes within a country or between countries. Rarely do water and agricultural land are efficiently utilized in agricultural production in most developing countries. The two resources often occur concurrently in valley bottoms for the major part of the year. Thus, valley bottoms offer a unique environment guaranteeing profitable agricultural production if sustainably managed.Item Hifadhi ya Asili ya Amani Tanzania: Miradi ya Equator Wanavijiji na Maendeleo Himili ya Jamii(Equator Initiative: Environment and Energy Group - United Nations Development Programme - UNDP, 2012)Hifadhi ya Asili ya Amani ilitangazwa kisheria na Serikali ya Tanzania katika gazeti la serikali mwaka 1997, ikiwa na lengo la kuihifadhi bayoanuwai ya Milima ya Usamabara Mashariki. Safu ya Mashariki ya Milima ya Usambara imeorodheshwa kama kituo cha kimataifa cha bayoanuwai ya mimea na inajivunia kuwa ya pili kwa kuwa na aina nyingi za mimea katika bara la Afrika. Pia ilitangazwa na UNESCO kuwa Hifadhi ya Binadamu na Viumbe hai, mwaka 2000. Hifadhi hii ya viumbe hai yenye eneo la takribani hekta 83,600 inajumuisha misitu ya mvua na ardhi ya nyasi na miti ya uwanda wa chini. Ina sifa ya kuwa na mimea mingi iliyo katika hatari ya kutoweka (ikiwemo mimea mingi ya madawa) na ni makazi ya zaidi ya aina kumi na tatu za ndege wasiopatikana mahali pengine. Pia misitu hii mikuu hutoa maji kwa wakazi zaidi ya 300,000 katika mji wa Tanga, na wenyeji wa milimani wanategemea misitu hii kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaisha.Item Ijue sheria ya ardhi na taratibu zinazohusika kupata, kumiliki na kuuza ardhi vijijini na mjini, Sheria Katika Lugha Rahisi(Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara, 2015-06)Chama Cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) ni chama kilichoanziahwa na Sheria ya Bunge ya 1954 Sura Na.307. Kwa mujibu wa sheria hiyo, Chama kinawajibu wa kuisaidia serikali katik amasuala yahusuyo sheria na pia kuieleimisha jamii kisheria katika kupata haki zao za msingi. Katika kutimiza jukumu lake kwa wanajamii Cham Cha Sheria Tnaganyika kimeeandaa kijarida hiki cha sheria katika lugha Rahisi kiitwacho “IJUE SHERIA YA ARDHI NA TARATIBU ZINAZOHUSIKA KUPATA, KUMILIKI NA KUUZA ARDHI VIJIJINI NA MJINI’’.Item Jarida la Umasikini na Mazingira - Toleo Na. 6 Jan - June 2009(Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), Idara ya Mazingira kwa ufadhili wa Mradi wa Umaskini na Mazingira, 2009)Jarida hili linatolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), Idara ya Mazingira kwa ufadhili wa Mradi wa Umaskini na Mazingira kwa lengo la kutoa elimu na kujenga uelewa wa jamii na wadau mbalimbali kuhusu uhusiano uliopo kati ya umaskini na mazingira. Taarifa na makala zilizochapishwa katika jarida hili ni: Juhudi za Kuondoa Umaskini kwa wakazi wa Jiji la Dar zitabaki kuwa Ndoto Kama Uchafuzi wa Mazingira hautadhibitiwa!!! • Katibu Mkuu Atembelea Mbeya na Kupongeza Jitihada za Utunzaji wa Mazingira; • Kupunguza Gesijoto Kupitia Kudhibiti Ukataji Miti Na Uharibifu Wa Misitu Katika Nchi Zinazoendelea; • Utunzaji wa Mazingira Wasaidia Vijana Kujitegemea; • Tuzo ya Rais ya Uongozi na Ubora wa Hifadhi ya Mazingira katika Uchimbaji Madini kuchangia Juhudi za uchimbaji endelevu Tanzania;Item Jinsi wakulima hukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa(Farm Radio International - FRI, 2009-12)Kujifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu kwa wakulima kwa sababu ya athari wanayoweza kuwa nayo kwenye kilimo. Wakulima wanaweza kutarajia kiasi cha joto kilichopanda na dhoruba za mara kwa mara, mafuriko na hali za ukame. Hali ya hewa itakuwa inabadilikabadilika zaidi na hivyo ngumu kutabiri. Wakulima wanahitaji kuelewa mabadiliko ya hali ya hewa na anga ili kufanya mipango kuhusu mavuno yanayobadilika na tofauti, ukosefu wa maji, na uwezekano wa ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa. Makala haya yanatoa habari msingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakayokusaidia kutayarisha vipindi vya redio kuhusu mada hii. Unavweza kuwaambia wakulima katika eneo lako kuhusu njia kadhaa ambazo kwazo, mabadiliko ya hewa huwaathiri wakulima. Kisha unaweza kujadili mikakati ambayo wakulima wa eneo hilo wanaweza kutumia ili kufanikiwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ongea na wakulima ili uelewe changamoto yao imekuwa nini kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa. Je, wamepata njia mpya, au kutumia njia za jadi zinazowasaidia kukabiliana na hali hii mpya.Item Jinsia na haki kuhusu Ardhi(FAO, 2017) Lukalo, F; Dokhe, EKwa zaidi ya miaka miwili baada ya kuzinduliwa kwa Tume ya Kitaifa ya Ardhi Februari 2013, hatua nyingi zimepigwa za kuboresha usimamizi wa ardhi nchini Kenya. Kuchapisha kitabu hiki ni ufanisi unaohitaji kusherehekea kwa sheria na kanuni mbalimbali ilizobuniwa katika kuzindua katiba ya Kenya inayolenga marekebisho katika sekta ya ardhi ambayo yamewekwa kukidhi mahitaji ya usawa wa jinsia katika masuala ya ardhi. Katiba mpya ndiyo kilele cha ongezeko la hatua zilizopigwa na nchi ili kuinua hadhi ya wanawake na maslahi yao katika ardhi. Katiba mpya inawakilisha hatua kubwa zilizopigwa kuboresha hadhi za wanaume na wanawake katika nyanja zote za maisha. Kwa sababu hiyo pana haja ya kuzingatia ufafanuzi wa ardhi kwa upana (maji na nafasi iliyopo) kama rasilimali asilia na mali nyingine inayopatikana katika ardhi. Ardhi na mali nyingine (kama mifugo, madini yanayochimbuliwa, mashine na kadhalika.) inaweza kutumika kwa kilimo na uzalishaji na vile vile inaweza kuwa chanzo cha uwezeshwaji wa kisiasa miongoni mwa wanawake. Kuwa na uwezo wa kupata ardhi na mali kunatoa nafasi ya makazi na kuwawezesha wanawake kujiunga katika ushindani wa siasa kuhusu rasiliamali; ardhi ni mali inayostahili kujumuishwa katika ndoa na inaweza kutumika kama chombo cha kupata mikopo.Item Kijitabu cha viua magugu na matumizi yake(CROPBASE (T) L, 1996) CFU-TanzaniaJapokuwa kitengo cha Kilimo Hifadhi (CFU) hakihimizi matumizi ya Viua Magugu vya aina fulani au Viuatilifu vingine vya kukinga mimea, wakulima wanafahamu kuwa Viua Magugu vikitumika kwa usahihi aidhaa kwenye Kilimo Hifadhi au Kilimo cha mazoea huokoa muda mwingi unaotumika kwenye palizi linaloumiza mgongo. Wakulima ambao wanatumia viuatilifu hivi kwa usahihi wanaokoa muda mwingi na gharama zinazotumika kuajiri vibarua kufanya palizi. Wazalishaji na wafanyabiashara wanaosambaza Viua Magugu na Viuatilifu vingine vya mimea wamerahisisha upatikanaji wa viuatilifu husika kote nchi Zambia na ukanda mzima wa kusini mwa Afrika. Hii imefanya wakulima wengi kununua na kutumia viuatilifu mara kwa mara kwenye mashamba yao bila hata kuwa na mafunzo/elimu yakutosha. Wakulima aidha wa Kilimo Hifadhi au wa kilimo cha mazoea hutumia viuatilifu katika mfumo wao wa uzalishaji ili kuongeza kipato kwa lengo la kuongeza ubora wa maisha katika familia. CFU ni shirika kubwa na lenye uzoefu wa kutoa mafunzo ya Kilimo Hifadhi nchini Zambia na kwingineko. Hivyo basi, itakuwa ni kutokuwajibika kama CFU haitatoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu. CFU inaendelea kutoa mafunzo ya kina kuhusu Viua Magugu na matumizi yake kwa wafanyakazi/watumishi wake wote. Mafunzo haya hutolewa kwa Mabwana shamba ambao nao wanawafundisha waratibu wa wakulima. Baada ya hapo waratibu hutoa mafunzo hayo kwa wakulima wengine. Mafunzo haya ni kwa yeyote anayetaka kushiriki na hakuna malipo au gharama yoyote. Watumishi wengi kutoka wizara ya kilimo na kutoka mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali wamenufaika na mafunzo haya yanayotolewa kwa kina na kwa mbinu shirikishi. Kijitabu hiki kimeandaliwa na CFU kama muhtasari wa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viua Magugu ambayo yameshatolewa kwa maelfu ya wakulima na wanyunyizaji wa viatilifu hivi. Kijitabu hiki hakilengi kuwa mbadala wa mafunzo ya ana kwa ana.Item Kilimo bora cha nyasi(Shirika la kilimo Uyole, 1990-05) Myoya, T.JKatika Nyanda za Juu za Kusini ni Mikoa miwili tu (Iringa na Mbeya) ambayo idadi ya ng'ombe wa maziwa imeongezeka sang. Hii ni baada ya kuanzishwa kwa mradi wa kushughulikia wafugaji wadogo wadogo kati ya nchi ya Uswisi na Tanzania. Katika sehemu hizi nyasi za asili zilizopo ni zile za kuezekea na utafiti uliofanyika Uyole unaonyesha kuwa nyasi hizi kutoa chakula kidogo kwa msimu. Vile vile baada ya msimu wa-mvua kuanza nyasi hizi hukua upesi upesi na baada ya miezi miwili tu, hutoa mbegu na hivyo ubora wake kupungua. Hi mifugo ya kisasa iweze kutoa maziwa mengi inahitaji chakula chenye asili mia protini zaidi ya saba kiasi ambacho hakipatikani kwenye nyasi za asili. Hivyo kwa ufugaji wa kisasa ni lazima mbinu nyingine za kuweza kupata malisho bora zitumike. Hata hivyo katika nyanda hizi msimu wa ukuaji wa mimea ni siku 180 tu yaani toka mwanzo wa Desemba hadi mwisho wa Mei. Baada ya hapo malisho hayakui kwa sababu ya baridi kali ya usiku, hasa mwezi wa sita mpaka wa nane, na baada ya hapo kwa ajili ya ukosefu wa unyevu. Hivyo tunakabiliwa na miezi sita ambayo lazima mbinu ya kupata chakula bora zitumike.Item Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira(Afrika Kontakt, 2017)La Via Campesina na Afrika Kontakt tunakiri kuwa tuko nyuma sana katika kukabiliana na tatizo linalotukabili la mabadiliko ya tabianchi. Sehemu kubwa ya tatizo bado haijatatuliwa, ambayo ni mifumo yetu ya kiulimwengu ya masuala ya kijamii na kiuchumi inayosababisha mabadiliko ya tabianchi. Kwahiyo, lazima tupambane kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inabadilishwa. Zaidi ya hapo, tunatakiwa kushiriki katika mchakato mzima wa kutafuta njia na mikakati mbadala ya kuleta mabadiliko halisi. Wakati wa mkutano wa Mazingira wa Paris yaani COP21, wanaharakati wa masuala ya tabianchi walikuwa wakipaza sauti zao kuhusu mabadiliko ya mfumo, na siyo mabadiliko ya tabianchi. Wengi wa wanaharakati hao hapo awali walikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Wanaharakati hao huliona suala la mabadiliko ya tabianchi kama jambo halisi na ambalo hutokea kila siku. Kwa mujibu wa maelezo yao, hatutakiwi kuwasubiri wanasiasa kuchukua hatua, na badala yake wamekuwa wakichukua hatua ambazo kwa bahati mbaya zimekuwa zikipuuzwa na wanasiasa wengi na watunga sera au wamekuwa wakidharauliwa na mfumo. Lengo la kitabu hiki cha mwongozo ni kuonyesha athari za mabadiliko ya tabianchi zinazowakabili wakulima wadogo, lakini pia kugusia suluhisho ambazo wanaweza kuzitumia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia maarifa ya wakulima wadogo kutoka Uganda, Tanzania, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, na Msumbiji. Kutokana na ukweli kuwa jamii za zilizoko katika nchi hizo wanategemea sana mazingira asilia na maliasili zake, wamekuwa wahanga wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi. Lakini uhusiano wao wa karibu na mazingira umewesha uwepo wa maarifa kutoka kizazi kimoja hadi kingine ambayo yanatumika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi. Hali iliyopo sasa kwenye majadiliano ya kimataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na madhara makubwa ya mabadiliko ya tabianchi vinahitaji kuchukuliwa hatua za dharura. Kwa sasa tunaelewa fika kuwa mfumo wa uzalishaji uliosababisha mabadiliko ya tabianchi hauwezi kutumika kukabiliana na tatizo ambalo wenyewe ulisababisha. Badala yake tunatakiwa kufungua macho yetu ili tuweze kutambua njia zilizopo na tuweze kuziendeleza na kuzitanua ili zisaidie katika mapambano. Hili linajumuisha mabadiliko kwenye mfumo wa uzalishaji wa dunia nzima.Item Kilimo na hifadhi ya mazingira(Inades Formation Tanzania, 1993) Gilla, AlliKwa muda mrefu wazee wetu wamekuwa wakitegemea kilimo. Mahitaji yao yote yamekuwa yakitokana na mashamba yao na misitu. Hawakuwa na shida kubwa ya chakula au kuni Leo hii mabadiliko mengi yametokea. Watu wameongezeka sana. Sasa hivi huwezi kufungua shamba mahali popote tu; kila shamba lina mwenyewe. Sio ajabu siku hizi kusikia kesi nyingi zinazohusu mashamba na mipaka. Sasa hivi huwezi kulima kilimo cha kuhamahama au kupumzisha shamba kama walivyofanya wazee. . Siku hizi rutuba ya udongo imepungua sana; matokeo yake mavuno nayo yamepungua. Sehemu nyingine watu wanatumia mbolea kupita kiasi na kuharibu udongo. Sasa hivi upatikanaji wa kuni umekuwa wa tabu. Katika sehemu za milimani kama Mgeta matatizo hayo ni makubwa zaidi. Wakulima wa huko kila siku wanayashuhudia matatizo haya.Item Kilimo rafiki na mazingira(TFCG, 2016)Kipeperushi kinachoelezea kilimo chenye kutumia mbinu bora za kilimo zenye tija kwa mkulima na kuyalinda mazingira. Ni mfumo unaohusisha ulimaji / matumizi ya udongo na mazao kwa utaratibu ambao hupunguza mmomonyoko wa udongo na utoaji wa hewa ukaa mashambaniItem Kitabu cha mbinu bora(Tanzania Osaka Alumni - TOA, 2012)Maboresho ya Serikali za Mitaa Tanzania yamelenga katika utoaji bora wa huduma wa Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sera za kitaifa za Serikali Kuu. Maboresho yamekaribisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, washirika wa maendeleo na wadau wengine tangu awamu ya kwanza hadi sasa. Sera ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) iliwekwa dhahiri mwaka 1998 na utekelezaji wake wa maboresho ya Serikali za Mitaa ulianza mwaka 2000. Kupitia ushirikiano huu maboresho ya Serikali za Mitaa hapa Tanzania yamefanikiwa kuleta Serikali za Mitaa za kidemokrasia, matumizi bora ya raslimali watu, kuongozeka kwa ruzuku toka hazina, kuimarika kwa utawala bora katika Serikali za Mitaa, kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi, na kwa ujumla kuongezeka kwa uhuru wa serikali za mitaa katika utoaji huduma.Item Kitabu cha mwongozo wa mafunzo kwa wawezeshaji wa shamba darasa wa Mradi wa Igunga Eco-Village(Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Tanzania, 2018)Kitabu hiki cha mwongozo wa wawezeshaji wa mashamba darasa kitatumiwa na wawezeshaji hao kutoa mafunzo kwenye mashamba darasa na jamii zinazowazunguka. Kitabu hiki pia kinatoa mwongozo katika mafunzo ya ujenzi wa jiko banifu, biogesi, Kilimo cha kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na ufugaji wa kuku wa asili na samaki. Kitabu hiki pia kinatoa mwongozo katika masuala ya maji na usafi wa mazingira, gharama nafuu katika ujenzi wa choo na chujio la kuchujia maji kwa gharama nafuu, kifaa cha kukarabati na kuchimba lambo, uchimbaji wa kisima na pampu ya kamba.Item Kitabu cha Mwongozo: Upitishaji wa Sheria Ndogo katika Ngazi ya Kijiji(Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, 2011-08)Mwongozo huu wa upitishaji wa Sheria Ndogo katika ngazi ya Kijiji umetokana na Sheria za Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya Sura 287 toleo la 2002 pamoja na Sera ya Serikali ya kugatua madaraka kwa kukabidhi kazi, haki, wajibu pamoja na rasilimali fedha kwa wananchi kupitia Serikali za Mitaa. Aidha, changamoto mbalimbali zilizoko vijijini kupitia program mbalimbali kama vile Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Mfuko ya Maendeleo ya Jamii (TASAF), hifadhi ya Mazingira na Kilimo kwanza, zimetoa msukumo mkubwa kuwa na haja ya kuwa na mwongozo kama huu unaowezesha vijiji kuandaa sheria zake ndogo zitakazosaidia kukabiliana na changamoto hizo mfano kuhimiza watu kushiriki na kuchangia kwenye shughuli za maendeleo na kushiriki kwenye ulinzi shirikishi katika maeneo yao.Item Kujenga picha ya jamii yetu kwa siku zijazo: sababu na jinsi ya kushiriki kupanga matumizi ya ardhi - Sura ya Pilii(2010)Wote tunaiona wazi: watu wameongezeka, miji imekua, mifugo imeongezeka, mashamba mengi zaidi .... Vilevile uharibifu zaidi wa ardhi, uharibifu wa misitu, mmomonyoko wa udongo .... Migogoro mingi zaidi kati ya wakulima na wafugaji, wachimba madini na wafugaji, wanyamapori na watu .... Mahitaji yetu ya kutumia ardhi yanaongezeka wakati wote, lakini eneo la ardhi haliongezeki. Tutafanyaje ili tuwe na matumizi mazuri na ya kuridhisha ya ardhi tuliyonayo, katika mazingira ya hali ya tabianchi na maliasili, pamoja na tamaduni zetu, njia tunazotumia kumudu maisha, matarajio na ndoto za jamii yetu? Kujibu swali hili ndilo lengo la kupanga matumizi ya ardhi. Na kwa sababu ardhi ni ya msingi kwa jamii, mpango wa matumizi ya ardhi unakuwa bora pale tu jamii inaposhiriki kikamilifu kwenye mchakato. Hapo ndipo linapokamilika suala la “ushirikishwaji” kwenye mpango shirikishi wa matumizi ya ardhi, yaani LUP.Item Kulima kwa plau(Kilimo Hai Blog, 2018-06)Katika nchi yetu, wakulima wengi wameshazoea kutumia ng'ombe au punda kukokota plau au mkokoteni. Wanafurahi uzoefu huo kwa sababu wameshapata faida nyingi. Wakulima wengine bado wanasitasita kutumia ng'ombe wao kufanya kazi.Item Maazimio ya wananchi kwa Vyama vya siasa kuhusu uhifadhi wa misitu na mazingira: Uchaguzi wa 2015(Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania - MJUMITA na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania - TFCG, 2015-06)Misitu ni rasilimali muhimu sana ambayo nchi yetu imejaliwa. Inakadiriwa Tanzania ina misitu yenye ukubwa wa hekta milioni 48.1 ambayo ni sawa na asilimia 38 ya eneo lote la ardhi ya nchi yetu. Misitu hii hata hivyo inakabiliwa na upoteaji wa kiwango cha eneo la hekta 400,000 kwa mwaka, na hii inasababishwa na kilimo cha kuhama hama, mifugo, moto na uvunaji holela na usio endelevu wa mazao ya misitu na shughuli zingine za kibinadamu. Kutokana na changamoto zinazoikabili misitu na jamii inayoishi pembezoni mwa misitu, jamii imeamua kuandaa majumuisho ya changamoto hizo na mapendekezo ya namna ya utatuzi wake. Lengo ni kutumia fursa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 katika utatuzi wa changamoto za misitu na jamii ili misitu yetu iendelee kutoa huduma ya kiikolojia, kiuchumi na kijamii kwa muda mrefu.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »