Matumizi Bora ya Ardhi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Matumizi Bora ya Ardhi by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 51
Results Per Page
Sort Options
Item Kilimo bora cha nyasi(Shirika la kilimo Uyole, 1990-05) Myoya, T.JKatika Nyanda za Juu za Kusini ni Mikoa miwili tu (Iringa na Mbeya) ambayo idadi ya ng'ombe wa maziwa imeongezeka sang. Hii ni baada ya kuanzishwa kwa mradi wa kushughulikia wafugaji wadogo wadogo kati ya nchi ya Uswisi na Tanzania. Katika sehemu hizi nyasi za asili zilizopo ni zile za kuezekea na utafiti uliofanyika Uyole unaonyesha kuwa nyasi hizi kutoa chakula kidogo kwa msimu. Vile vile baada ya msimu wa-mvua kuanza nyasi hizi hukua upesi upesi na baada ya miezi miwili tu, hutoa mbegu na hivyo ubora wake kupungua. Hi mifugo ya kisasa iweze kutoa maziwa mengi inahitaji chakula chenye asili mia protini zaidi ya saba kiasi ambacho hakipatikani kwenye nyasi za asili. Hivyo kwa ufugaji wa kisasa ni lazima mbinu nyingine za kuweza kupata malisho bora zitumike. Hata hivyo katika nyanda hizi msimu wa ukuaji wa mimea ni siku 180 tu yaani toka mwanzo wa Desemba hadi mwisho wa Mei. Baada ya hapo malisho hayakui kwa sababu ya baridi kali ya usiku, hasa mwezi wa sita mpaka wa nane, na baada ya hapo kwa ajili ya ukosefu wa unyevu. Hivyo tunakabiliwa na miezi sita ambayo lazima mbinu ya kupata chakula bora zitumike.Item Mafunzo ya kilimo.(INADES-FORMATION TANZANIA., 1990-07-19) Inades-formation, TanzaniaNi asubuhi na mapema Bwana shamba anakutana na Matonya akiwa na shoka beganiJ hengo mkononi na kibuyu cha maji. Hiki ni kipindi cha kiangazi Miti imepNkutisha majani nyasi na vichaka vyote vimekauka majani yote. Upepo unatimua vumbi kila mahali hasa katika maeneo yenye njia za mifugo mashambani na hata barabarani. Na maeneo ya milimani yameanza kuchomwa moto.Item Kilimo na hifadhi ya mazingira(Inades Formation Tanzania, 1993) Gilla, AlliKwa muda mrefu wazee wetu wamekuwa wakitegemea kilimo. Mahitaji yao yote yamekuwa yakitokana na mashamba yao na misitu. Hawakuwa na shida kubwa ya chakula au kuni Leo hii mabadiliko mengi yametokea. Watu wameongezeka sana. Sasa hivi huwezi kufungua shamba mahali popote tu; kila shamba lina mwenyewe. Sio ajabu siku hizi kusikia kesi nyingi zinazohusu mashamba na mipaka. Sasa hivi huwezi kulima kilimo cha kuhamahama au kupumzisha shamba kama walivyofanya wazee. . Siku hizi rutuba ya udongo imepungua sana; matokeo yake mavuno nayo yamepungua. Sehemu nyingine watu wanatumia mbolea kupita kiasi na kuharibu udongo. Sasa hivi upatikanaji wa kuni umekuwa wa tabu. Katika sehemu za milimani kama Mgeta matatizo hayo ni makubwa zaidi. Wakulima wa huko kila siku wanayashuhudia matatizo haya.Item Kijitabu cha viua magugu na matumizi yake(CROPBASE (T) L, 1996) CFU-TanzaniaJapokuwa kitengo cha Kilimo Hifadhi (CFU) hakihimizi matumizi ya Viua Magugu vya aina fulani au Viuatilifu vingine vya kukinga mimea, wakulima wanafahamu kuwa Viua Magugu vikitumika kwa usahihi aidhaa kwenye Kilimo Hifadhi au Kilimo cha mazoea huokoa muda mwingi unaotumika kwenye palizi linaloumiza mgongo. Wakulima ambao wanatumia viuatilifu hivi kwa usahihi wanaokoa muda mwingi na gharama zinazotumika kuajiri vibarua kufanya palizi. Wazalishaji na wafanyabiashara wanaosambaza Viua Magugu na Viuatilifu vingine vya mimea wamerahisisha upatikanaji wa viuatilifu husika kote nchi Zambia na ukanda mzima wa kusini mwa Afrika. Hii imefanya wakulima wengi kununua na kutumia viuatilifu mara kwa mara kwenye mashamba yao bila hata kuwa na mafunzo/elimu yakutosha. Wakulima aidha wa Kilimo Hifadhi au wa kilimo cha mazoea hutumia viuatilifu katika mfumo wao wa uzalishaji ili kuongeza kipato kwa lengo la kuongeza ubora wa maisha katika familia. CFU ni shirika kubwa na lenye uzoefu wa kutoa mafunzo ya Kilimo Hifadhi nchini Zambia na kwingineko. Hivyo basi, itakuwa ni kutokuwajibika kama CFU haitatoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu. CFU inaendelea kutoa mafunzo ya kina kuhusu Viua Magugu na matumizi yake kwa wafanyakazi/watumishi wake wote. Mafunzo haya hutolewa kwa Mabwana shamba ambao nao wanawafundisha waratibu wa wakulima. Baada ya hapo waratibu hutoa mafunzo hayo kwa wakulima wengine. Mafunzo haya ni kwa yeyote anayetaka kushiriki na hakuna malipo au gharama yoyote. Watumishi wengi kutoka wizara ya kilimo na kutoka mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali wamenufaika na mafunzo haya yanayotolewa kwa kina na kwa mbinu shirikishi. Kijitabu hiki kimeandaliwa na CFU kama muhtasari wa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viua Magugu ambayo yameshatolewa kwa maelfu ya wakulima na wanyunyizaji wa viatilifu hivi. Kijitabu hiki hakilengi kuwa mbadala wa mafunzo ya ana kwa ana.Item Ziara ya mafunzo kwa wakulima kati ya nyanda za mashariki na ya nyanda za juu kusini(TARP II - SUA Project, 2001) Lyimo-Macha, J. G; Batamuzi, E. K; Tarimo, A. J. PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula, pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Washauri wa Ugani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara mbili (kanda moja kwenda kanda nyingine) zilizofanyika mwezi Agosti na Septemba 2001. Ziara ya kwanza ya kimafunzo ya wakulima iliwashirikisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Mbinga, Njombe, Makete na Mbeya (Kanda ya nyanda za juu kusini) hawa waliwatembelea wakulima wenzao wa wilaya ya Lushoto. Ziara ya pili iliwajumuisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Bagamoyo, Morogoro Vijijini na Kilosa (Kanda ya Mashariki) ambao waliwatembelea wakulima wa wilaya za Njombe na Mbarali.Item Efficient utilisation of river valleys - experiences from mbarali(TARP II Project - SUA, 2002) Batamuzi, E. K; Tarimo, A. J. PIn the Southern Highlands zones, within zone exchange visit was carried out from April 14 to 19, 2002. In this visit, farmers, extension agents and researchers from Kyela rice growing areas visited their counterparts in the Usangu plains to exchange experiences in ric.ecultivation and other agricultural enterprises being carried during the year. The theme of the visit was "Efficient Utilization of River valleys", a concept aimed at improving awareness of rice producing farmers in land and water management, including cropping systems and their interaction with livestock production systems. It is well understood that land and water are necessary resources for agricultural production. These essential resources have often led to wars between tribes within a country or between countries. Rarely do water and agricultural land are efficiently utilized in agricultural production in most developing countries. The two resources often occur concurrently in valley bottoms for the major part of the year. Thus, valley bottoms offer a unique environment guaranteeing profitable agricultural production if sustainably managed.Item MATUMIZI BORA YA ARDHI- Mafunzo kutoka Mlima Meru(Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania - TARP II - SUA Project), 2002-09) Lyimo-Macha, J. G; Malimbwi, R. E; Kiranga, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo Wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Wagani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha mafunzo yatokanayo na ziara iliyofanyika Septemba 2002. Ziara hii iliwashirikisha wakulima na washauri wa wakulima kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha wilaya za Kilosa, Handeni, Pangani, Mkuranga na Morogoro na kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwajumuisha wakulima na wagani kutoka wilaya za Mbeya, Mafinga, Njombe, Mbinga na Mbozi ambao walitembelea wakulima wa wilaya ya Arumeru, Arusha walioshiriki katika rnradi wa SCAPA. Makala hii pia inapatikana katika lugha ya kiingereza.Item Matumizi bora ya mbolea ya Minjingu kwenye kilimo cha mboga(Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Mikocheni & Kituo cha Ut afiti wa M azao Uyole, 2003)Kipeperushi kinachoelezea mbolea ya Minjingu kama ni mbolea asilia ya kupandia. Mbolea hii inatokana na miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu mkoani Manyara ambayo husagwa na kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu ina kirutubisho cha mimea aina ya fosiforasi kati ya asilimia 12.3-13.2. Tofauti na mbolea nyingine za kupandia zenye madini ya fosiforasi kama vile TSP na DAP ambazo huagizwa nje ya nchi hivyo kugharimu fedha nyingi za kigeni, mbolea hii inayopatikana hapa nchini bei yake ni nafuu.Item MPANGO WA KUHAMISHA SHUGHULI ZA KIPATO (MKUSHUKI) KWA WALIOCHUKULIWA MASHAMBA YAO KWA AJILI YA HIFADHI YA UBIOANUWAI KATIKA USHOROBA WA MSITU WA DEREMA :Ushoroba wa misitu ya Derema: Milima ya Usambara Mashariki(Mradi wa Hifadhi na Usimamizi wa Misitu Tanzania - TFCMP, 2006-09)Kati kati ya mwaka 2002, wakulima 1128 waliokuwa wakiishi sehemu ya kaskazini mashariki ya Tanzania, kwenye miteremko mikali ya milima ya Usambara Mashariki, waliambiwa kwamba mazao katika mashamba yao madogomadogo katika misitu, nje ya vijiji vyao ilibidi yafyekwe ili kuihifadhi misitu hiyo. “Ushoroba Mpya wa Derema” utakuwa ni kiungo kati ya hifadhi mbili za misitu ambayo inalindwa na mwendelezo wa makazi ya mamia ya ndege, wanyama watambaao, wadudu, spishi za wadudu na mimea ambayo ni adimu sana, na mingine ambayo inatishiwa kutoweka. Wakulima walilipwa fidia ya mazao ambayo yalikuwa katika mpaka wenye upana wa mita tatu kuzunguka ushoroba; mpaka ambao uliwekwa kwa kufyeka mimea iliyokuwa katika mpaka huo. Mazao yao ndani mpaka –yenye thamani kubwa, yale ya iliki, mdalasini, karafuu na pilipili manga, pamoja na baadhi ya miti ya matunda – yalihesabiwa na kuorodheshwa kwa ajili ya kulipiwa fidia baadaye.Item Virus diseases of orchids(Califonia Agricultural, 2008-09-18) Kado, Clarence I.Virus diseases are probably responsible for the mosaic and necrotic symptoms in orchids that are often blamed on other disorders. This circular discusses the four viruses of orchids that have been identified thus far: cymbidium mosaic, orchid tobacco mosaic, vanda mosaic, and cymbidium ringspot. Symptoms in several orchid genera are described, and methods are suggested for disease control. It also tells how to test for these orchid virus diseases on non-orchidaceous, herbaceous plants.Item Jarida la Umasikini na Mazingira - Toleo Na. 6 Jan - June 2009(Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), Idara ya Mazingira kwa ufadhili wa Mradi wa Umaskini na Mazingira, 2009)Jarida hili linatolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), Idara ya Mazingira kwa ufadhili wa Mradi wa Umaskini na Mazingira kwa lengo la kutoa elimu na kujenga uelewa wa jamii na wadau mbalimbali kuhusu uhusiano uliopo kati ya umaskini na mazingira. Taarifa na makala zilizochapishwa katika jarida hili ni: Juhudi za Kuondoa Umaskini kwa wakazi wa Jiji la Dar zitabaki kuwa Ndoto Kama Uchafuzi wa Mazingira hautadhibitiwa!!! • Katibu Mkuu Atembelea Mbeya na Kupongeza Jitihada za Utunzaji wa Mazingira; • Kupunguza Gesijoto Kupitia Kudhibiti Ukataji Miti Na Uharibifu Wa Misitu Katika Nchi Zinazoendelea; • Utunzaji wa Mazingira Wasaidia Vijana Kujitegemea; • Tuzo ya Rais ya Uongozi na Ubora wa Hifadhi ya Mazingira katika Uchimbaji Madini kuchangia Juhudi za uchimbaji endelevu Tanzania;Item Jinsi wakulima hukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa(Farm Radio International - FRI, 2009-12)Kujifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu kwa wakulima kwa sababu ya athari wanayoweza kuwa nayo kwenye kilimo. Wakulima wanaweza kutarajia kiasi cha joto kilichopanda na dhoruba za mara kwa mara, mafuriko na hali za ukame. Hali ya hewa itakuwa inabadilikabadilika zaidi na hivyo ngumu kutabiri. Wakulima wanahitaji kuelewa mabadiliko ya hali ya hewa na anga ili kufanya mipango kuhusu mavuno yanayobadilika na tofauti, ukosefu wa maji, na uwezekano wa ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa. Makala haya yanatoa habari msingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakayokusaidia kutayarisha vipindi vya redio kuhusu mada hii. Unavweza kuwaambia wakulima katika eneo lako kuhusu njia kadhaa ambazo kwazo, mabadiliko ya hewa huwaathiri wakulima. Kisha unaweza kujadili mikakati ambayo wakulima wa eneo hilo wanaweza kutumia ili kufanikiwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ongea na wakulima ili uelewe changamoto yao imekuwa nini kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa. Je, wamepata njia mpya, au kutumia njia za jadi zinazowasaidia kukabiliana na hali hii mpya.Item Kujenga picha ya jamii yetu kwa siku zijazo: sababu na jinsi ya kushiriki kupanga matumizi ya ardhi - Sura ya Pilii(2010)Wote tunaiona wazi: watu wameongezeka, miji imekua, mifugo imeongezeka, mashamba mengi zaidi .... Vilevile uharibifu zaidi wa ardhi, uharibifu wa misitu, mmomonyoko wa udongo .... Migogoro mingi zaidi kati ya wakulima na wafugaji, wachimba madini na wafugaji, wanyamapori na watu .... Mahitaji yetu ya kutumia ardhi yanaongezeka wakati wote, lakini eneo la ardhi haliongezeki. Tutafanyaje ili tuwe na matumizi mazuri na ya kuridhisha ya ardhi tuliyonayo, katika mazingira ya hali ya tabianchi na maliasili, pamoja na tamaduni zetu, njia tunazotumia kumudu maisha, matarajio na ndoto za jamii yetu? Kujibu swali hili ndilo lengo la kupanga matumizi ya ardhi. Na kwa sababu ardhi ni ya msingi kwa jamii, mpango wa matumizi ya ardhi unakuwa bora pale tu jamii inaposhiriki kikamilifu kwenye mchakato. Hapo ndipo linapokamilika suala la “ushirikishwaji” kwenye mpango shirikishi wa matumizi ya ardhi, yaani LUP.Item MKURABITA nyenzo ya Serikali inayoibukia kuwawezesha wanyonge walio wengi nchini: Kujenga uwezo wa Halmashauri za Wilaya(Ofisi ya Waziri Mkuu, 2010)Kufuatia kukamilika kwa Awamu ya Uandaaji wa Maboresho Julai 2008, MKURABITA iliingia katika awamu yake ya Tatu ambayo ni Utekelezaji wa Maboresho. Menejimenti ya MKURABITA ilianza kwa kutekeleza baadhi ya mapendekezo hayo yanayo husiana na urasimishaji wa rasilimali vijijini na hata mijini kwa utaratibu iliyoita “FRONT RUNNERS” kwa mbinu ya Ujengeaji uwezo Halmashauri za wilaya. Katika utaratibu huu MKURABITA ilianza na wilaya kumi ambazo ni Makete, Njombe, Wete, Musoma, Serengeti, Manyoni, Mpwapwa, Mvomero, Rufiji na Nachingwea.Item Tunza Jamii Yako, Tunza Mazingira Yako kwa Maisha Bora: Jihusishe. Jipangie. Amua(The Green Belt Movement, 2010)Kijitabu hiki kimetengenezwa na Shirika la FHI 360 likishirikiana na Green Belt Movement kama sehemu ya tathmini kwa afya ya umma. Green Belt Movement ina lengo la kulinda mazingira ikiwa ni pamoja na uongozi mzuri kwa wale wanaoishi humo. Kijitabu hiki kitashughulikia uhusiano kati ya Mazingira bora, usalama wa riziki na familia zenye afya, miongoni mwa mengine.Item Taasisi ya utafiti na utetezi wa haki za ardhi(HAKIARDHI, 2011-01-06) Fabian, Beatha; Eliseus, GogfreyMfumo wa milki ya ardhi nchini Tanzania umefanyiwa maboresho makubwa kuanzia miaka ya tisini kwa kutunga sera ya ardhi ya taifa ya mwaka 1995 iliyofuatiwa na sheria mpya za ardhi namba 4 na sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 zote 1999.Item Tathmini ya asali za kiangazi katika mabonde a mpunga(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-03) Wizara ya KilimoNdugu Wakulima; sote tunakubaliana kwamba kilimo cha umwagiliaji maji ndio mkombozi wetu kwa ukulima wa mpunga, umuhimu wake umezidi kuwa mkubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa yanayotokea duniani kote, hali inayosababisha kilimo cha kutegemea mvua kutokuwa cha uhakika na cha matumaini. Hivyo, tunahitaji kujipanga vyema na kukiimarisha kilimo cha umwagiliaji maji ili tuwe na uhakika wa chakula na kupunguza uagizaji. Kwa mujibu wa Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji wa mwaka 2003, Zanzibar tunalo eneo la ekari 21,300 ambazo zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji maji. Hadi sasa eneo lililojengwa miundombinu ni ekari 1,750 sawa na asilimia 8% tu ya eneo lote. Eneo lililobaki lenye ukubwa wa ekari 19,550 kati ya hizo ekari 200 zimejengwa makinga maji, ekari zilizobaki 19,350 zinaendelea kutumika kwa uzalishaji wa mpunga wa kutegemea mvua. Ndugu Wakulima pamoja na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu, bado tunakabiliwa na changamoto za gharama kubwa za ujenzi wa miundombinu, ukarabati wa visima na pampu kutokana na teknolojia duni upungufu wa wataalamu na elimu ya uendeshaji wa jumuiya za wakulima na upungufu mkubwa wa mitaji, utegemezi mkubwa wa nishati ya umeme, uharibifu wa vianzio vya maji pamoja na ukosefu wa zana maalum za utayarishaji wa ardhi. Kutokana na changamoto hizo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji maji linalimwa kwa kutegemea mvua hali ambayo inapelekea uzalishaji na tija ndogo. Ndugu Wakulima, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 2011 – 2016 Wizara ya Kilimo na Maliasili imekusudia kuutekeleza kikamilifu Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji ambao unatarajiwa kutatua changamoto zote za kilimo hicho. Wizara imezungumza na Serikali ya Korea kupitia Benki ya EXIM – ambao wamekamilisha uhakiki wa eneo la ekari 5250 ambalo litajengwa mindombinu ya umwagiliaji maji. Serikali ya Japan na Benki ya BADEA pia wameonesha nia ya kutusaidia katika Kilimo cha umwagiliaji maji. Ndugu Wakulima, Wizara imekusudia kuendeleza ujenzi wa miundombinu na utunzaji wa vianzio vya maji ili sekta ya umwagiliaji maji ipate maendeleo endelevu na kuwawezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga. Kuzijengea uwezo Jumuiya za Wakulima wa umwagiliaji maji ziweze kushiriki kikamilifu katika uendeshaji na utunzaji wa miundombinu, uhifadhi wa vianzio vya maji na utoaji wa huduma za Kilimo. Wizara inaendelea kuwashajihisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuchagua miradi ya kijamii ya umwagiliaji maji ikiwemo ujenzi wa miundombinu na makinga maji kila wanapopata fursa ya usaidizi wa Washirika wa Maendeleo. Ndugu Wakulima, napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa wakulima wa mpunga wa umwagiliaji maji watumie mbegu bora na pembejeo zinazotolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo na kuhakikisha kuwa miundombinu ya umwagiliaji maji iliyojengwa kwa gharama kubwa tunaitumia kikamilifu katika uzaalishaji wa zao hili.Item Maeneo ya Kilimo ya Unguja na Pemba(Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar, 2011-06) Wizara ya KilimoItem Kitabu cha Mwongozo: Upitishaji wa Sheria Ndogo katika Ngazi ya Kijiji(Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, 2011-08)Mwongozo huu wa upitishaji wa Sheria Ndogo katika ngazi ya Kijiji umetokana na Sheria za Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya Sura 287 toleo la 2002 pamoja na Sera ya Serikali ya kugatua madaraka kwa kukabidhi kazi, haki, wajibu pamoja na rasilimali fedha kwa wananchi kupitia Serikali za Mitaa. Aidha, changamoto mbalimbali zilizoko vijijini kupitia program mbalimbali kama vile Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Mfuko ya Maendeleo ya Jamii (TASAF), hifadhi ya Mazingira na Kilimo kwanza, zimetoa msukumo mkubwa kuwa na haja ya kuwa na mwongozo kama huu unaowezesha vijiji kuandaa sheria zake ndogo zitakazosaidia kukabiliana na changamoto hizo mfano kuhimiza watu kushiriki na kuchangia kwenye shughuli za maendeleo na kushiriki kwenye ulinzi shirikishi katika maeneo yao.Item Kitabu cha mbinu bora(Tanzania Osaka Alumni - TOA, 2012)Maboresho ya Serikali za Mitaa Tanzania yamelenga katika utoaji bora wa huduma wa Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sera za kitaifa za Serikali Kuu. Maboresho yamekaribisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, washirika wa maendeleo na wadau wengine tangu awamu ya kwanza hadi sasa. Sera ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) iliwekwa dhahiri mwaka 1998 na utekelezaji wake wa maboresho ya Serikali za Mitaa ulianza mwaka 2000. Kupitia ushirikiano huu maboresho ya Serikali za Mitaa hapa Tanzania yamefanikiwa kuleta Serikali za Mitaa za kidemokrasia, matumizi bora ya raslimali watu, kuongozeka kwa ruzuku toka hazina, kuimarika kwa utawala bora katika Serikali za Mitaa, kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi, na kwa ujumla kuongezeka kwa uhuru wa serikali za mitaa katika utoaji huduma.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »