Chakula na Lishe
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Chakula na Lishe by Author "Edwin, Tuzie"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Lishe kwa mtoto mwenye virusi vya ukimwi umri wa miaka 2 hadi 9(COUNSENUTH, 2006-08-15) Mwasi, Fatma; Materu, Mary G.; Edwin, TuzieLishe bora ni rnuhimu kwa watoto wote hususan wenye virusi vya UKIMWI kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yao. Watoto wanakua kwa haraka hivyo wana mahitaji makubwa ya chakula ili kuwapatia virutubishi muhimu yaani nishati-lishe, protini, madini na vitamini. Watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI wako katika hatari kubwa ya kupata utapiamlo kutokana na: • Ongezeko la mahitaji ya virutubishi hasa nishati-lishe. • Maradhi ya mara kwa mara. • Ulaji duni. • Uyeyushwaji na ufyonzwaji duni wa virutubishi mwilini. Mengi ya maradhi yanayoambatana na kuishi na virusi vya UKIMWI na UKIMWI huathiri mfumo mzima wa ulaj i wa chakula na kusababisha lishe duni. Lishe duni hudhoofisha mfumo wa kinga na hivyo humuweka mtoto katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali kwa urahisi. Maradhi na utapiamlo kwa pamoja huhatarisha maisha ya mtoto mwenye virusi vya UKIMWI.