Repository logo
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Српски
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
  • Communities & Collections
  • All of DSpace
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Српски
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Shirika la chakula Duniani"

Now showing 1 - 19 of 19
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Binzari ya manjano
    (Shirika la chakula duniani, 2022-04-22) Shirika la chakula Duniani
    Binzari ya manjano katika majiko ya nchi zote za Asia Kusini, ikiwa ni pamoja na India na Pakistan. Lakini je binzari manjono hutumiwa kwa ajili ya ladha ya chakula au inaweza kuboresha afya na kuzuwia saratani? Utakuta maelfu ya makala zikielezea jinsi binzari ya manjano zinavyoweza kutibu magonjwa kama kiungulia, kukosekana kwa uwezo wa tumbo wa kusaga chakula, kisukari, huzuni na maradhi ya ubongo ya Alzheimer.Inaweze hata kuponya saratani. Maelfu ya tafiti yamekwishafanywa juu ya binzari ya manjano. Kiungo hiki kinasemekana kuwa na manufaa ya kimatibabu, na kiana kiungo kiitwacho curcumin. Majaribio yaliyofanywa kwa panya yameonyesha kuzuia aina nyingi za saratani kukua ndani yake. Lakini binzari manjano huwa na asilimia mbili hadi tatu za curcumin na tunapoila, miili yetu haifyonzi kiasi chote hicho. Hatahivyo, tafiti kuhusu binzari za manjano huripoti kwa nadra kiasi cha kawaida cha binzari hiyo katika mlo. Kwahiyo ulaji wa kiasi kidogo cha Binzari ya manjano kunaweza kuboredha afya yetu au je tunapaswa kutumia virutubisho vya binzari ya manjano au curcumin kujikinga na magonwa.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Biringanya
    (Shirika la chakula duniani, 2022-12-02) Shirika la chakula Duniani
    Biringanya ni moja ya vyakula ambavyo ni maarufu sana katika jamii nyingi ulimwenguni. Hupikwa kama mboga katika maeneo mengi ya Afrika. Kwa upande wa nchi za Ulaya, hupikwa kama kifurahisha kinywa (snack).
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Chakula cha GMO
    (Shirika la chakula duniani, 2022-10-04) Shirika la chakula Duniani
    Pengine umesikia kuhusu uhandisi jeni wa vyakula (GMO) na unaweza ukawa unajiuliza inahusu nini, hapa tunakueleza. Kenya wiki hii imeidhinisha kilimo na uingizaji wa mazao na vyakula vilivyobadilishwa vinasaba, (GMO) na hivyo kumaliza marufuku ya muongo mmoja iliyokuwa imewekwa kutokana na hofu ya kiafya. Inakuja wakati nchi inakabiliwa na ukame mbaya. Ukame mbaya zaidi katika miaka 40 umeacha mamilioni ya watu wakikabiliwa na njaa. Serikali ya Rais William Ruto imegeukia mimea iliyobadilishwa vinasaba kama njia ya kusaidia kuongeza mavuno. Inasema nchi inahitaji mbegu zinazostahimili ukame, wadudu na magonjwa. Muongo mmoja uliopita uzalishaji na uagizaji wa mazao ya GM ulipigwa marufuku kwa sababu ya wasiwasi juu ya hatari zinazowezekana za kiafya. Kwa wazi ulikuwa uamuzi usiopendwa na Amerika, ambayo ni nyumbani kwa wazalishaji wakuu wa mbegu zilizotengenezwa kwa vinasaba.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Kilimo bora cha soya.
    (Shirika la chakula duniani, 2024-04-12) Shirika la chakula Duniani
    Maharagwe ya soya ni moja ya mazao muhimu katika jamii ya mikunde katika nyanja za uzalishaji wa kibiashara kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini (35-40%). Soya inatumika katika kuandaa vyakula vinavyoliwa vikiwa vibichi, vinavyovundikwa na vyakula nikavu, mfano maziwa, tofu, mchuzi pamoja na kimea. Soya hulimwa katika ukanda wa Ikweta. Soya hukomaa katika kipindi cha siku 180 (miezi 6) lakini inaweza kuwa na baadhi zinazokomaa mapema zaidi. Joto chini ya nyuzi joto 21 na juu ya 32 inaweza kuathiri ushavushaji na utengenezaji wa viriba. Na joto zaidi ya nyuzi 40 ni hasara kwa uzalishaji wa mbegu.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Kuanzia ngozi, nyama, maziwa na hata manyoya, ngamia ni lulu katika jamii
    (Shirika la chakula duniani, 2018-02) Shirika la chakula Duniani
    Ngamia ni mnyama muhimu katika maeneo ya ukame au baridi kali anakotumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri, chakula kupitia maziwa na nyama yake, kuwawezesha wanawake kiuchumi na pia kulinda mazingira. Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limeutenga mwaka huu wa 2024 kuwa wa wanyama wa jamii ya ngamia ambao ni waokozi wa jamii za maeneo ya mbali katika zaidi ya mataifa 90.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mihogo inaweza kutumika kupunguza gharama ya juu ya chakula
    (Shirika la chakula duniani, 2022-05-22) Shirika la chakula Duniani
    Kuna mboga kuu mbili za mizizi katika Afrika Magharibi - mihogo na viazi vikuu au magimbi. Muhogo unapatikana mwaka mzima, ni wa bei nafuu na unajulikana, au tukisema kwa usahihi, ulijulikana kuwa chakula cha maskini. Nyingine maarufu ni viazi vikuu, ambayo mwandishi wa Nigeria Chinua Achebe alitaja kama "mfalme wa mazao". Mavuno ya magimbi yanasubiriwa kwa hamu. Hakika, ibada maalum hufanywa kabla ya magimbi kuvunwa na kuliwa, na tunavaa nguo zetu bora zaidi ili kusherehekea zao hilo. Muhogo ni chakula bora cha kila siku na kilikuwa kama chakula cha kawaida cha maskini na watumishi. Ninaona kuwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda anawataka watu wake kugeukia mlo wa mihogo kama dawa ya kuporomoka kwa bei ya ngano wakati huu ambapo gharama ya maisha duniani kote imepanda .
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mwelekeo wa dunia katika kutegemea washawasha, senene na wadudu wengineo kama milo yenye virutubisho vingi
    (Shirika la chakula duniani, 2016-03-09) Shirika la chakula Duniani
    Je umewahi kufikiria kuwa wadudu lishe ni moja ya majawabu ya kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, halikadhalika lishe na kutokomeza umaskini? Kama hapana, basi fuatilia makala hii kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo duniani, IFAD. Kilimo kinaongoza kwa kusababisha mabadiliko ya tabianchi na wakati huo huo ni sehemu ya majawabu ya kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Nyanya
    (Shirika la chakula duniani, 2022-03-17) Shirika la chakula Duniani
    Gramu 80 za nyanya hutoa karibu 5% ya mahitaji ya kila siku ya potasiamu ya mtu mzima. Ulaji wa vyakula vyenye potasiamu husaidia mtumiaji dhidi ya ugonjwa wa kiharusi na inaweza kuhusishwa na kiwango cha chini cha ugonjwa wa moyo. Nyanya pia zina ina lycopene, ambacho hutoa rangi nyekundu. Kuna kundi kubwa la utafiti unaofanywa kuhusu lycopene na sifa zake za kiafya, ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Orodha ya vyakula vitakavyoliwa mwaka 2050
    (Shirika la chakula duniani, 2022-05-22) Shirika la chakula Duniani
    Wanasayansi wameandaa orodha ya mimea ambayo inaweza kuwa sehemu muhimu ya lishe yetu mnamo mwaka 2050, lakini sasa haijulikani. Katika siku zijazo, tunaweza kuwa tunakula ndizi za kutengenezwa au tunda la mti wa pandunus kama kifungua kinywa cha asubuhi.Vita nchini Ukraine vimeashiria ongezeko la hatari la njaa kwani inaangazia mazao machache ambayo yanaweza kusambazwa duniani kote. Takriban asilimia 90 ya kalori ulimwenguni hutoka kwa aina 15 za nafaka. Kwa hivyo wataalamu katika bustani ya Royal Botanic ya London huko Queens wanatafuta mazao yanayofaa kwa siku zijazo. Pia kuna hatari kwamba uzalishaji wa chakula utapungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na bei ya chakula kupanda. Ili kupambana na njaa na kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa, tunahitaji kupanua wigo wa chakula. Anafafanua San Pierre. "Watu duniani kote hula maelfu ya aina za mimea na ni katika mimea hii tunaweza kupata ufumbuzi wa changamoto za chakula kwa siku zijazo," alisema. Kati ya zaidi ya mazao 7,000 yanayoliwa duniani kote, ni aina 417 pekee zinazolimwa kwa ajili ya chakula. Nini kinaweza kuwa chakula cha siku zijazo?
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Samaki wenye mafuta
    (Shirika la chakula duniani, 2022-03-09) Shirika la chakula Duniani
    samaki wenye mafuta ni wazuri kwa afya? ikiwa ni hivyo, ni aina gani bora na unapaswa kula mara ngapi? Nicola Shubrook, mtaalamu wa lishe, anaelezea faida za samaki hawa.Samaki wa mafuta mengi ya asidi ya mafuta ya omega-3. Asidi ya mafuta ya Omega-3 inachukuliwa kuwa muhimu kwa mwili wa binadamu, hupatikana katika vyakula kwani haiwezi kuzalishwa na mwili.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Tumia panzi au senene badala ya nyama ya ngombe
    (Shirika la chakula duniani, 2022-07-22) Shirika la chakula Duniani
    Kwa watu wengi wa Ulaya na Marekani, wazo la kula senene na panzi linaweza kuonekana kuwa la kuchukiza, lakini ni vitafunwa maarufu katika sehemu za Afrika na Asia. Sio tu kwamba wamejaa virutubisho lakini pia hawana madhara kwa hali ya hewa pia. Hewa katika nyumba ya familia moja nchini Uganda imejaa harufu ya kipekee, isiyofanana na harufu ya nyama ya ng'ombe iliyochomwa. Ilikuwa Desemba 2000 na Maggie, alikuwa anakaanga wadudu jamii ya panzi. Kadiri alivyowachochea wadudu hao wa kijani kibichi, kama nzige, ndivyo harufu yake ilivyozidi kuwa yenye nguvu. Walipokuwa wakikaangwa na mvuke ukipanda kutoka kwenye sufuria inaleta msisimko. Haikuwa mara yake ya kwanza wa kula wadudu hao aliwala mara kwa mara wakati wa utoto nchini Uganda, ni watamu wenye lishe na vitafunwa vinavyotafutwa sana. Katika mwaka huo wa 2000, alivuna wadudu hao jamii ya panzi kwa mara ya kwanza. Wadudu hawa, ambao huzaliana karibu na Ziwa Victoria Afrika mashariki, hutoka kwa makundi usiku na kutua kwenye nyasi zenye umande karibu na nyumba yao alfajiri.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Ukulima wa mwani kisiwani Pemba
    (Shirika la chakula duniani, 2021-06) Shirika la chakula Duniani
    Ukulima wa mwani visiwani Pemba wachangamshwa na mradi wa IFAD na GEF . Sasa wakazi hawa wa kisiwa cha Pemba wanazidi kutegemea chanzo mbadala cha mapato kinachoota chini ya maji ya bahari, Mwani.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Ulaji mboga pekee unaweza kuwa na manufaa gani kwa afya ya mwanadamu
    (Shirika la chakula duniani, 2018-09-07) Shirika la chakula Duniani
    Kumeshuhudiwa kuibuka suala la umuhimu wa kula mboga katika miaka ya hivi karibuni hasa kutokana na wasi wasi kuhusu afya zetu, harakati za wateteaji wa haki za wanyama na mazingira. Walaji mboga tu ni wale ambao hawali nyama, kuku, samaki au bidha zozote kutoka kwa wanyama, yakiwemo mayai na bidhaa kama maziwa.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Unga wa nazi na faida zake kiafya
    (Shirika la chakula duniani, 2023-04-04) Shirika la chakula Duniani
    Unga wa nazi ni unga laini unaotengenezwa kwa nyama iliyokaushwa ya nazi. Tui la nazi linapotolewa kwenye nyama ya nazi, kisha hukaushwa kwa joto la chini na kusagwa kuwa unga unaofaa kuoka.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Viungo vya chakula
    (Shirika la chakula duniani, 2020-04-09) Shirika la chakula Duniani
    Utafiti mwingi juu ya pilipili umeonyesha namna pilipili inavyoweza kuathiri afya, lakini matokeo ni mchanganyiko Viungo kwenye chakula vimekuwa vikitumiwa kwa miaka mingi sana. Binzari' Turmeric' na pilipili zimefanyiwa utafiti katika miongo ya hivi karibuni... Lakini je huwa tunatumia viungo hivyo ipasavyo kwa ajili ya afya zetu au la?Na faida za viungo hivyo ni zile ambazo unahisi.Viungo vimekuwa sehemu ya milo yetu ya kila siku maelfu ya miaka ,tumezoea kula viazi vya kukaanga na pilipili, tangawizi kwenye chai na kuongeza kwenye mlo.Lakini hivi karibuni, baadhi ya viungo ambavyo vimekuwa vinatajwa kuwa tiba ya baadhi ya magonjwa ingawa hakuna tangazo rasmi linalothibitisha hoja hiyo.Binzari imekuwa ikitumika katika maeneo ya bara la Asia kwa millennia.Katika utafiti wa mwaka 2014 , haijawekwa wazi bado kuwa utumiaji wa viungo una faida za kiafya
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Zao la Giligilani
    (Shirika la chakula duniani, 2022-11-02) Shirika la chakula Duniani
    Kiungo maarufu katika sehemu nyingi za dunia, giligilani ni shujaa asiyejulikana wa vyakula vya Kihindi. Na sasa mpishi mmoja anataka kukifufua, akiipa giligilani "utukufu unaostahili". Ukichunguza ndani ya viboksi vyovyote vya viungo vya Kihindi, kuna uwezekano mkubwa kukuta viungo - manjano, pilipili nyekundu ya unga na giligilani ya kusaga (mara nyingi vikichanganywa na binzari) - ambayo ni msingi wa vyakula vingi vya mboga. Ingawa haina rangi ya kuvutia kama manjano na haihusiani na ladha yoyote ya viungo vya India, giligilani (inayojulikana sana dhaniya au kothmir nchini India) labda ndiyo inayotumika zaidi kati ya viungo hivi vingi. Mbegu zake zilizosagwa huongeza ladha kwenye vyakula vingi, wakati unga wake, unaweza kutumika kutengeneza Curry Powder. Mmea wake mabua na majani yake mbichi mara nyingi hutumika kama ladha ya kumalizia yenye harufu nzuri na tamu.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Zao la ndizi na faida zake
    (Shirika la chakula duniani, 2023-07-09) Shirika la chakula Duniani
    Ndizi ni mojawapo ya tunda linalopendwa zaidi duniani, likiwa limesheheni vitamini na madini.Ziko faida kadhaa za kiafya za ndizi ambazo ni muhimu kwa mlaji kula tunda hili. Faida hizi ni pamoja na Inasawazisha maji ya mwili "homoni": ndizi ina kiasi kikubwa cha potasiamu na vitamini B6 vitu vinavyokuza uzalishaji wa kiasi cha maji kinachohitajika. Kulingana na wataalamu wa masuala ya lishe, ndizi zina madini ya potassium kwa wingi, ambayo mwili wa binadamu unahitaji, kwa mujibu wa Catherine Collins, kutoka hospitali ya St George mjini London.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Zao la tangawizi na faida zake
    (Shirika la chakula duniani, 2022-11-25) Shirika la chakula Duniani
    Tangawizi ni nini? Tangawizi ni ya familia moja kama manjano na iliki. Asili ya Asia ya Kusini-Mashariki, India na China, tangawizi ni sehemu ya lishe ya eneo hili na inathaminiwa kwa harufu yake, upishi na dawa. Ingawa tunafahamu zaidi mapishi tunayopenda kama vile mkate wa tangawizi ni zaidi ya kionjo imekuwa ikitumika kwa sifa zake za dawa tangu zamani.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Zijue nafaka zenye afya zaidi
    (Shirika la chakula duniani, 2023-04-29) Shirika la chakula Duniani
    Nafaka ni aina ya nyasi inayokuzwa kwa ajili ya "tunda" lake linaloweza kuliwa, linalojulikana zaidi kama nafaka.Nafaka hulimwa nyingi na hutoa virutubisho vingi zaidi vya chakula kuliko zao lolote, iwe ni moja kwa moja kwa chakula cha binadamu na kwa njia isiyo ya moja kwa moja ya malisho ya mifugo.Katika hali ya asili, nafaka ina wingi wa vitamini, madini, wanga, mafuta, na protini. Mara nyingi buckwheat na quinoa huchanganywa kama kundi la nafaka lakini ni ukweli ni kwamba hizi ni mbegu za mimea. Lakini kwa kuwa matumizi yao ya upishi yanafanana, imejumuishwa katika orodha hii

DSpace software copyright © 2002-2025 LYRASIS

  • Cookie settings
  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback