Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Subject "Hifadhi"
Now showing 1 - 5 of 5
Results Per Page
Sort Options
Item Majaribio kuhusu uhifadhi wa nafaka kijiji cha Mlali(Wizara ya Kilimo na Chakula, Tanzania, 2014)Wakulima wengi Tanzania wanapata hasara kubwa inayosababishwa na wadudu waharibifu wa mazao yanapohifadhiwa kwenye maghala. Uharibifu huu unatishia uhakika wa chakula kwa kaya. Kaya zingine zina uwezo wa kununua madawa ya kuulia wadudu, lakini madawa haya yana gharama kubwa na yaweza kuwa na madhara kwa afya zao, (na kama yakiwa yameharibika huwa hayafai kwa matumizi). Mradi huu umebuniwa kutafiti ubunifu kwa ajili ya wakulima kuhusu matumizi ya madawa asilia ya “diatomaceous earths” (vumbivumbi linalotokana na masalia ya zamani ya viumbe wa majini), katika kuhifadhi mazao kama njia mbadala vijijini. Kwa njia hiyo watafiti watawajibika kwanza kufanya majaribio na kulinganisha uwezo wa madawa mbalimbali katika zoezi zima la kudhibiti wadudu waharibifu wa nafaka, ziwapo ghalani. Awali, majaribio haya linganifu yatafanywa kwa kipindi cha miezi 8 kuendana na msimu wa kuhifadhi mazao, kuanzia Julai 2002 hadi Machi 2003.Item Mfumo wa stakabadhi wa maghala Tanzania(Warehouse Receipts Regulatory Board, 2000)Mfumo wa Stakabadhi za Maghala ni mfumo unaotumika nchini wa kutumia bidhaa zilizohifadhiwa kwenye maghala badala ya mali zisizohamishika kuwa dhamana ya kupata mikopo kutoka asasi za fedha. Mfumo kama huu pia unatekelezwa nchi nyingine za bara la Afrika pamoja na mabara ya Ulaya na Amerika. Kwa kufuata mfumo huu wakulima wadogo na wakati wakiwa kwenye Ushirika au Vikundi vya wakulima wanakuwa na nguvu ya soko na kuingia katika soko la ushindani ambalo ingekuwa vigumu kutokana na kukosekana kwa mitaji. Pia mfumo huu unasaidia kuzuia upotevu wa mazao unaotokana na uhifadhi dhaifu, kuhifadhi mazao ili kusubiri kuuza wakati muafaka na pia kuongezea bidhaaa thamani kabla ya kuziuza.Item Mwongozo wa Tekinolojia za Utunzaji wa Mazao ya Bustani Baada ya Kuvuna(Kituo cha Utafiti na Habari za Tekinolojia za Baada ya Kuvuna, Chuo Kikuu cha California, Davis, 2003) Kitinoja, L; Kader, A. ALicha ya kutumia kiwango cha kisasa cha teknolojia husika, utunzaji fanisi baada ya kuvuna ni jambo muhimu katika kufikia lengo linalokusudiwa. Wakati wazalishaji wa kiwango kikubwa wananufaika kwa utumiaji wa tekinolojia za kisasa za baada ya kuvuna kwa kuwekeza katika mitambo ya hali ya juu, siyo rahisi kwa wazalishaji wa kiwango kidogo kufanya hivyo, badala yake teknolojia rahisi na za gharama ndogo zinaweza kuwafaa. Wazalishaji wa kiwango kidogo ni walio na mitaji midogo, wakulima wanaouza mazao moja kwa moja sokoni na wafanyabiashara wa kati wanaowauzia mazao wasafirishaji wa nje ya nchi. Mambo mapya yaliyovumbuliwa hivi karibuni katika teknolojia zinazotumika baada ya kuvuna (mazao) yanajibu matamanio ya kuepuka matumizi ya gharama kubwa za utendaji kazi na kupata bidhaa bora. Njia hizi zinaweza zisiwe endelevu kwa kipindi kirefu kutokana na masuala ya kijamii na kiuchumi, kiutamaduni na au mazingira. Kwa mfano, matumizi ya viuatilifu baada ya kuvuna yanaweza kupunguza matukio ya mashambulizi ya wadudu waharibifu lakini yanaweza kuwa na matokeo yenye gharama kifedha na katika mazingira. Pamoja na hayo, kuongezeka kwa mahitaji ya matunda na mboga zinazozalishwa kwa kutumia kilimo hai/kilimo ogani, kunatoa fursa ya upatikanaji wa soko kwa wakulima wa kiwango kidogo na wauzaji. Hali halisi ya wanaohudumia (handlers) mazao kwa kiwango kidogo inajumuisha matumizi ya nguvu kazi ya ziada, ukosefu wa mikopo kwa ajili ya kuwekeza katika teknolojia zinazotumika baada ya kuvuna, nishati ya umeme isiyoaminika, ukosefu wa usafiri mbadala, vifaa vya kuhifadhi na au vifungashio na kuwepo kwa vikwazo vingine. Kwa bahati nzuri, kuna wigo mpana wa teknolojia rahisi za kutumia zinazoweza kuchaguliwa na mbinu nyingi zenye uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu ya watunzaji wa kiwango kidogo na wauzaji wa mazao. Kwa miaka mingi mbinu zilizopo katika mwongozo huu, zimefanikiwa kupunguza upotevu na kutunza ubora wa mazao ya bustani katika sehemu mbalimbali duniani.Item Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna. Kitabu na. 1(Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula., 2003)Nafaka ni mazao makuu ya chakula ambayo hutumiwa na watanzania wote waishio mijini na vijijini. Nafaka zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko mazao mengine ya chakula na mara nyingi nafaka huzalishwa mara moja au mbili kwa mwaka. Kwa hiyo ili iweze kupatikana na kutumika kwa wakati wote ni lazima kuhifadhi. Aidha ili kuweza kuwa na bidhaa zenye thamani ni lazima kusindika. Jitihada zimekuwa zikifanywa na seikali kuongeza tija na uzalishaji wa mazao hayo. Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka. Pamoja na ongezeko la uzalishaji, teknolojia zinazotumika katika uvunaji, utayarishaji na hifadhi ni duni na husababisha upotevu mkubwa wa mazao hayo. Wastani wa tani 1,559,000 za mazao ya nafaka hupotea kila mwaka. Aidha upotevu mkubwa hutokea katika maghala kutokana na kuhifadhi nafaka ambayo haijakauka sawasawa na pia kutokana na mashambulizi ya wadudu waharibifu. Kuongeza uzalishaji pekee hakutakuwa na maana ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kupambana na matatizo yasababishayo upotevu wa mazao hayo. Teknolojia sahihi za utayarishaji wa mazao kabla ya kuhifadhi zisipotumika, nafaka itaharibika hata kama ingehifadhiwa katika ghala bora. Hivyo ni vyema kutumia njia bora za kutayarisha nafaka kama vile kukausha vyema, kusafisha na kufungasha ili kupunguza uharibifu unaosababisha upotevu wa mazao. Lengo la uandaaji wa kitabu hiki ni kuelimisha jamii kuhusu teknolojia sahihi za uvunaji, utayarishaji, ufungashaji, usindikaji na hifadhi ya mazao ya nafaka baada ya kuvuna. Aidha matumizi bora yanayokidhi mahitaji ya lishe ya mazao hayo yameainishwaili kupunguza tatizo la utapia mlo na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na kuongeza kipato. Walengwa wa kitabu hiki ni wakulima na wadau wengine ambao wamejiajiri katika sekta ya kilimo.Item Uboreshaji waVihenge, Hifadhi Bora na Udhibiti wa Viumbe Waharibifu wa Mazao Ghalani(Kurugenzi ya Utafiti na Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA, 2005-01) Makundi, R. H; Misangu, R. N; Reuben, S. O. W. M; Kilonzo, B. M; Ishengoma, C. G; Lyimo, H; Mwatawala, MHifadhi bora ya mazao inahakikisha familia inakuwa na chakula cha kutosheleza mwaka mzima. Pia mazao yanaweza kuuzwa wakati wowote ili kuongeza kipato. Mradi wa hifadhi bora ya mazao na udhibiti wa viumbe waharibifu umebuniwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA),na unafadhiliwa na Programu ya FOCAL,SUA. Mradi huu unawalenga wakulima katika wilaya tatu Tanzania ambazo ni Handeni, Mvomero na Iringa Vijijini. Hifadhi bora na udhibiti wa wadudu, panya na viumbe wengine wanaoharibu mazao ghalani ni muhimu ili kuhakikisha mazao kama mahindi, kunde, maharage, mpunga, n.k. yanayozalishwa na wakulima hayaharibiwi wakati yanapohifadhiwa. Utafiti shirikishi unafanyika juu ya mbinu za asili na za kisasa ili kuboresha hifadhi ya mazao na kudhibiti viumbe waharibifu wa mazao ghalani.