Matumizi bora ya zana za Kilimo

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 17 of 17
  • Item
    Mbinu bora za kunyunyizia dawa kwenye pamba
    (Chuo cha kilimo cha Sokoine, 1995) Mashaka, R. I
    Kitabu hiki kinampatia mkulima mbinu bora za kunyunyizia dawa kwenye pamba ili kuondoa vijidudu vinavyoharibu ukuaaji wa pamba. Pia jinsi ya kutumia zana za kilimo na mavazi sahihi wakati wa kunyunyizia dawa. Mkulima anatakiwa kujua ni wakati gani wa kunyunyizia dawa kwenye pamba kutoka kwa wataalam.
  • Item
    Uhamasishaji wa Teknolojia yakupima unyevu kwenye ardhi au “Teknolojia ya Kinyonga”
    (Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 2023) Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
    Tekinoljia hii hupima uwepo wa unyevu nyevu ndani ya udongo, na kinapima kiasi cha mvutano ambacho mmea unatumia kupata maji kutoka kwenye udongo. Kina taa za rangi nne na hufukiwa ndani ya udongo ili kupima unyevunyevu.
  • Item
    Vyama vya Wamwagiliaji
    (Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 2023) Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
    Kanuni ya 97 ya kanuni za Umwagiliaji inaelekeza uundaji wa kamati ya usuluhishi wa migogoro yenye wajumbe wasiopungua 3 na wasiozidi 5 wali- ochaguliwa miongoni mwa wanachama. Wajumbe wa kamati ya usuluhishi watachaguliwa katika mku- tano mkuu ambao hawatatokana na wajumbe au viongozi waliopo katika kamati kuu ya Usimamizi.
  • Item
    Uanzishwaji na uwezeshwaji wa vikundi vya wakulima wadogo wadogo.
    (PANTIL chuo kikuu cha sokoine cha kilimo, 2016-06-15) Hella, Dk. J.P
    Kikundi cha wakulima ni chombo muhimu katika jamii, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi hasa pale vinapoanzishwa kwa kuzingatia sheria na taratibu ambazo wanavikundi wamejiwekea. Mafanikio huwa makubwa zaidi kama wanakikundi hushiriki katika kupanga na kutoa maamuzi ya jinsi ya kuendesha shughuli za kikundi tokea hatua za mwanzo. Kwa kufanya hivyo, na hivyo uwezekano wa kutekeleza yale waliyojipangia huongezeka. Kikundi cha wakulima huanzishwa na kuendeshwa kwa kuzingatia katiba ya kikundi, ambayo hutoa miongozo na maelekezo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha vikundi vinakuwa ni vyombo imara na hai kiuchumi. Aidha uanzishaji wa kikundi hulenga kuwapa uwezo na kuwawezesha wanachama kutekeleza madhumuni waliyojiwekea katika kuboresha hali zao za maisha. Kikundi cha wakulima kinaweza kuanzishwa mahali popote ambapo pana watu walio katika eneo moja linalowawezesha kufanya shughuli zao za pamoja kwa urahisi na ambao wataonesha nia yao kwa kulipa viingilio na hisa. Idadi ya chini ya watu wanaotakiwa kuanzisha kikundi ni kumi. Hata hivyo, idadi pekee haitoshelezi bali la msingi zaidi ni uhai wa kiuchumi.
  • Item
    Mitazamo na mienendo ya uwezeshaji wakulima Tanzania.
    (Program u ya PANTIL Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kurugenzi ya Utafiti na Uzamili, 2010-05-19) Mwaseba, Dismas L .; Mattee, Amon Z.
    Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeteke1eza tafiti zilizofadhiliwa na Serikali ya Norway kupitia shirika 1ao la NORAD kuanzia na TAN 90, TAN 20 na TARP - SUA, FOCAL na mwishowe PANTIL. Mradi wa PANTIL una lengo la kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mafunzo kwa vitendo, utafiti, na ushauri. Mradi pia unalenga katika kujenga misingi imara ya utafiti na ushauri kilimo na maliasili inayokidhi mahitaji ya jamii za wakulima na kutoa fursa mpya kwao. Aidha, mradi unatilia mkazo, mbinu fungamanishi ya nyanja anuai na maisha endelevu itakayosaidia walengwa kunufaika na huduma zaidi ya tekinolojia ya kilimo na ufugaji bora.
  • Item
    Enhancing pro-poor innovations in natural resources and agricultural value-chains (EPINAV)
    (EPINAV, 2012-06-10) Kilima, F. T.; Magayane, F. T.
    The program of enhancing pro-poor innovations in natural resources and agricultural value-chain (EPINAV) is a Norwegian government supported initiative being implemented by SOKOINE UNIVERSITY of AGRICULTURE and a Norwegian University of Life Sciences (UMB) in collaboration with other partners within Tanzania and Norway
  • Item
    Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula
    (© PELUM Tanzania 2013, 2013-09-13) PELUM Tanzania
    PELUM Tanzania ni mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yanayofanya kazi na wakulima na wafugaji wadogo nchini Tanzania. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1995 na kusajiliwa kisheria mwaka 2002. Kazi kuu ya PELUM Tanzania ni kuhamasisha na kuendeleza kilimo endelevu kwa kujenga uwezo wa Mashirika Wanachama kwa njia ya kutandaa, kutunza na kueneza habari pamoja na ushawishi na utetezi. Walengwa wakuu wa PELUM Tanzania ni Mashirika Wanachama ambapo wanufaikaji ni wakulima na wafugaji wadogo wanaohudumiwa na Mashirika Wanachama. Kwa sasa mtandao huu unaundwa na Mashirika Wanachama 33 yanayohudumia wakulima na wafugaji wadogo zaidi ya milioni moja na laki mbili katika mikoa 16 ya Tanzania Bara.
  • Item
    Mwongozo wa kuunganisha uhitaji na huduma za kilimo
    (Research Into Use, 2010-09-29) Media Net Ltd, T
    Mwongozo huu wa kuunganisha uhitaji na huduma za kilimo umeandaliwa kutokana na uzoefu na mafanikio ya Program ya Research Into Use,(RIU) katika mkoa wa Morogoro.
  • Item
    Umuhimu wa Kilimo na shughuli za mabwana shamba Afrika
    (DW, 2008-04-28) Dahman, Mohamed
    Wakati huu ambapo kuna wasi wasi mkubwa wa kimataifa kuhusu mustakbali wa upatikanaji wa chakula duniani haya ni matamshi yanayofaa kutafakariwa : ' Nafundisha watoto wa chuo kikuu kilimo na shughuli za mabwana shamba lakini wengi wao hupendelea kujifunza kazi nyengine hususan fani ya teknolojia ya mawasiliano ya habari kwa sababu kilimo ni kwa ajili ya watu wasiokwenda shule.
  • Item
    Mazao Sahihi Muongozo wa Redio
    (2013-11-23)
    Mabadiliko ya tabia nchi yanatarajiwa kuwa na athari kubwa katika uzalishaji wa chakula kote Afrika na duniani, na tayari inaweza kuwa yanachangia kuongezeka kwa ukosefu wa chakula na utapiamlo katika Afrika (FAO).
  • Item
    Matumizi ya mbolea za kukuzia kwenye mahindi
    (Kilimo Blog, 2010-04-23) Kilimo Blog
    Mbolea za kukuzia ni mbolea zinzotumika kuupa mmea afya nzur na mavuno kuwa mazuri wakati wa kuvuna, mbolea hizi zikitumika vibaya pia huleta madhara makubwa kwa mlaji na ardhi kwa ujumla, zipo mbolea za aina nying lakin leo nitazungumzia.
  • Item
    Tekinolojia endelevu: Mafunzo kutoka Mbozi na Njombe
    (TARP II Project - SUA, 2003)
    Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Washauri wa Ugani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara iliyofanyika mwezi Agosti 2003. Ziara hii iliwashirikisha wakulima, wagani na watafiti kutoka Kanda ya Mashariki na kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikijumuisha Manispaa ya Morogoro, wilaya za lringa na Mbarali. Wanaziara hawa waliwatembelea wakulima wa wilaya za Mbozi na Njombe ili kuona na kujifunza zaidi kuhusu teknolojia muhimu ambazo tayari wameazimia kuzitekeleza mara watakaporudi nyumbani kwao. Taarifa hii pia inapatikana katika lugha ya Kiingereza.
  • Item
    Tathmini ya mfumo wa utoaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima kupitia ruzuku Tanzania
    (EPINAV - SUA, 2013)
    Mojawapo ya kikwazo kikubwa kinachomkwamisha mkulima mdogo kulima kwa tija ni kumudu gharama za matumizi ya pembejeo za kilimo (mbolea na mbegu bora). Katika kuhakikisha Serikali ya Tanzania inamsaidia mkulima kumudu gharama hizo, mwaka 2008/2009 Serikali ilianzisha na kutekeleza utaratibu wa kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo kwa njia ya ruzuku kwa kupitia mfumo wa vocha (National Agricultural Inputs Voucher System - NAIVS). Katika kufuatilia ufanisi wa mpango huu, utafiti umefanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), chini ya mradi wa Enhancing Pro-poor Innovation in Natural Resources and Agricultural Value Chains (EPINAV).
  • Item
    Matumizi bora ya mbolea ya minjingu kwenye kilimo cha mboga
    (Kituo cha Utafiti wa Mazao Mikocheni & Kituo cha Utafiti wa Mazao Uyole, 2012)
    Kipeperushi kinachoelezea matumizi sahihi ya mbolea ya Minjingu katika ukulima wa mboga mboga.
  • Item
    Mwongozo wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi: Mwitikio wa Tanzania katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, Upungufu wa Chakula na Lishe Duni
    (FAO, 2017)
    Mwongozo wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi umeandaliwa kutokana na nyaraka zinaoonyesha dhamira ya Serikali ya Tanzania za kufanya sekta ya kilimo iweze kuhimili mabadiliko ya tabianchi hadi kufikia mwaka 2030.
  • Item
    Indicative fertilizers prices by zone, region and stock point by means of transport
    (TANZANIA FERTILIZER REGULATORY AUTHORITY, 2017)
    Bei elekezi za mboloea kutokana na vituo, mikoa, kanda na kwa njia ya usafirishaji kama zilizvyotolewa na Mamlaka ya Kusimamia Mbolea Tanzania.
  • Item
    Hatamu za punda
    (TARP II - SUA Project, 2011)
    Kipeperushi kinacholelezea jinsi ya kufunga hatamu za punda kwa akiwa mmoja au wengi kwa wakati mmoja.