Browsing by Author "Taasisi ya chakula na lishe"
Now showing 1 - 7 of 7
Results Per Page
Sort Options
Item Baadhi ya vyakula na viungo vinavyosaidia kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya.(Taasisi ya chakula na lishe., 2018) Taasisi ya chakula na lisheWatu wanaishi na virusi vya ukimwi na wenye ukimwi mara nyingi hupata matatizo ya ulaji ,umeng'enywaji, ufyonzwaji wa chakula mwilini ,mengine ni kupoteza hamu ya kula,mafua ya mara kwa mara ,vidonda vya kooni na kuharisha.Baadhi ya vyakula na viungo hivyo tangawizi,karoti nk.Item Chakula dawa(Sokoine university of agriculture, 2022-10-22) Taasisi ya chakula na lisheChakula dawa ni chakula kilichotengenezwa na kurutubishwa kwa nishati,vitamin na madini.Chakula hiki kimetengenezwa ma mafuta na hakihitaji kuchanganywa na maji.Chakula dawa hutumika katika kutibu utapiamlo kwa sababu huwa kina nishati,vitamin na madini kiasi kikubwa.Item Kitunguu saumu(Taasisi ya chakula na lishe., 2022-12-03) Taasisi ya chakula na lisheKitunguu saumu ni kiungo muhimu katika kaya nyingi kwenye mapishi. Pia kinajulikana kwa sifa zake za dawa. Mtaalamu wa Lishe Kerry Torrens anaeleza kwa nini? Kitunguu saumu ni moja ya mimea ya zamani zaidi duniani na ni mmea mgumu wa kudumu wa familia ya Liliaceae. Mimea mingine ya familia hii ni pamoja na kitunguu maji na kitunguu cha majani.Wanatofautishwa na harufu ya kupendeza na ladha maalum.Tembe zake zenye mfanano wa weupe hivi ndizo zinazotumika.Item LISHE(Wizara ya afya, 2021) Taasisi ya chakula na lisheKuboresha lishe ni msingi katika kufanikisha malengo yote ya Maendeleo Endelevu. Uwepo wa utapiamlo sugu (udumavu) unadhoofisha maendeleo katika uhakika wa chakula, uboreshaji wa elimu, na afya bora ya mama na mtoto nchini Tanzania. Lishe duni ndio sababu kubwa ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania na inakadiriwa kugharimu serikali asilimia 2.6 ya Pato la Taifa kila mwaka. Upotezaji huu wa mapato uko katika sekta ya kilimo na husababishwa na ukuaji duni wa akili na mwili unaotokana na utapiamlo.Kulingana na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2015-2016, takriban theluthi ya watoto wote chini ya miaka mitano wana udumavu na asilimia 14 wana upungufu wa uzito. Sababu kuu zinazoongoza kuleta utapiamlo ni ukosefu wa lishe mchanganyiko na bora kwa kila kaya, upatikanaji mbovu wa huduma za afya (pamoja na maji safi na salama, usafi wa mazingira), na mienendo duni ya lishe. Hali ya upungufu wa damu kwa mama ni shida nyingine kubwa nchini Tanzania, ikiwa na asilimia 57 ya wanawake wajawazito na asilimia 46 ya mama wanaonyonyesha wanaathiriwa.Item MAFUNZO YA LISHE KWA AJILI YA WATOA HUDUMA WA VITUO VINAVYOTOA HUDUMA ZA AFYA(Wizara ya afya, 2019-01-01) Taasisi ya chakula na lisheJumuiya ya Afya ya Nchi Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika imeendelea na uhamasishaji na msaada wa kitaaamu katika nchi husika ikiwemo Tanzania. Hii ni mojawapo ya mpango mkakati maalum wa kupunguza utapiamlo katika nchi hizi. Jumuiya inahamasisha kubadilishana uzoefu, taratibu sahihi, kubainisha vipaumbele, kujenga uwezo na kuhamasisha uwepo wa sera na program wezeshi zinazoboresha lishe katika nchi husika.Mafunzo kwa watoa huduma za lishe ni muhimu katika utekelezaji wa afua muhimu na zenye matokeo mazuri katika kuboresha lishe. Kuwajengea uwezo watoa huduma hao kutaongeza nguvu katika kuboresha wa utoaji wa huduma kwa walengwa katika ngazi zote. Aidha, Jumuiya ya Afya ya Nchi Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika uliandaa kitini cha mafunzo ya lishe kinacholenga kujengea uwezo, ujuzi na umahiri wezeshi kwa watoa huduma za lishe katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya jamii. Maandalizi ya kitini cha mafunzo ya lishe yalitokana na matokeo ya tathmini katika uwezo wa kutoa huduma za lishe kwa kada mbalimbali iliyofanyika mwaka 2011 katika nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika uliofanywa na shirika la Hellen Keller International.Jumuiya imetoa rai kwa nchi zote kufanya mapitio na kurasimisha kitini hicho katika manzigira ya nchi husika ili watoa huduma za lishe waweze kutoa huduma stahiki. Tanzania pia ina upungufu wa wataalamu wenye elimu, ujuzi na umahiri wa kutosha kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma za lishe kwa jamii. Hivyo, serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Afya Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imefanya mapitio na kurasimisha kitini hicho ili kiweze kutumika kufundisha walengwa watakaotoa huduma na hatimaye kupunguza utapiamlo nchini.Kitini kimegawanyika katika makundi mawili, mojawapo ni kile cha Mafunzo ya Lishe kwa watoa huduma za afya katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya. Kingine ni kile cha Mafunzo ya Lishe kwa Watoa Huduma za Afya Katika Ngazi ya Jamii. Ni matumaini yetu kwamba matumizi ya vitini hivi yataimarisha na kuongeza kasi na msukumo mpya wa taratibu mbalimbali zinazolenga kuboresha lishe nchiniItem Tathmini ya hali ya lishe,unasihi na huduma za lishe (NACS)(Wizara ya afya, 2017-12) Taasisi ya chakula na lisheTaasisi ya chakula na lishe Tanzania (TFNC). 2013. Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo: Bango kitita lenye ujumbe muhimu. Dar es Salaam, Tanzania: Taasisi ya chakula na lishe Tanzania na kuchapishwa kwa ufadhili wa shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF). Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi mbichi vyakula hivi ndivyo vinavyochukua sehemu kubwa ya mlo na kwa kawaida ndiyo vyakula vikuu. Vyakula katika kundi hili ni pamoja na mahindi, mchele, mtama, ulezi, ngano, uwele, viazi vikuu, viazi vitamu, mihogo, magimbi, viazi mviringo na ndizi mbichi.Item Zuia magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kwa kuzingatia.(Taasisi ya chakula na lishe., 2011-08) Taasisi ya chakula na lisheUlaji usiozingatia kiasi na mchanganyiko wa makundi yote ya chakula kama nafaka, mizizi na ndizi,vyakula vyenye asili ya wanyama na jamii ya kunde,mbogamboga na mtunda huchangia kwa kiasi kikubwa viashiria hatari vya magonjwa sugu kama vile ongezeko la lehemu na sukari kwenye damu.Hatima ya hali ni kupatwa na magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari,shindikizo kubwa la damu,ugonjwa wa moyo,baadhi ya saratan na mengineyo.