Mifugo na Uvuvi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Mifugo na Uvuvi by Subject "Chakula"
Now showing 1 - 4 of 4
Results Per Page
Sort Options
Item Kulisha mifugo kwa kutumia Lucerne ya miti(Kenya Agricultural Research Institute - KARI, 2011)Mti wa Lucerne (tree Lucerne) ni aina mpya ya mmea wenye chakula cha hali ya juu kwa mifugo; na ambao pia hutumika kwa mapambo, kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa maji au upepo, kurutubisha ardhi na kuni.Item Lishe bora kwa kuku wa asili vijijini(Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo - ILRI, 2016)Kuku wana mahitaji tofauti ya vyakula kulingana na umri (vifaranga, wanaokua, wakubwa) na uzalishajili (utagaji au unenepeshaji). Ili kuku waweze kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula cha kutosha na chenye ubora unaotakiwa kulingana na uhitaji wa miili yao. Lishe bora huzuia magonjwa mengi ya kuku hivyo ni muhimu kuku wapewe virutubisho muhimu. Ubora wa lishe ya kuku unaweza kuainishwa katika makundi ya vyakuItem Mlo kamili wa kuku(Kuku site, 2024) Kuku siteMlo kamili wa kuku ni mlo wenye virutubisho vyote muhimu anavyohitaji kuku kwa kiwango na uwiano sahihi, Virutubisho vinavyohitajika katika mlo wa kuku ni kama ifuatavyo: 1.Wanga (carbohydrates) Wanga hutumika kama chanzo cha haraka cha nishati (nguvu) katika mwili wa kuku, na inapatikana katika nafaka mbalimbali kama Mahindi, Pumba ya mahindi, Ngano, Mtama, Mchele n.k 2. Protini ( protein ) Ni kirutubisho muhimu ambacho hujenga mwili. Protini inapatikana katika vyakula kama Mashudu ya Alizeti, Dagaa, Soya, Damu n.k 3.Mafuta (Fat) Mafuta ni muhimu sana katika lishe ya kuku kwani humuwezesha kuku kusharabu fat soluble vitamins kama vitamin A, D, E, na K, huhifadhi nishati, kutunza joto na kulinda ogani muhimu katika mwili wa kuku.Item Mwongozo wa kutengeneza chakula cha samaki na ulishaji wa samaki(Chuo cha kilimo cha Sokoine, 2022) Chuo kikuu cha kilimo cha sokoineSamaki kama viumbe hai wengine wanahitaji kula chakula ili waishi na kukua. Katika mazingira ya asili kama vile mito, maziwa na bahari, samaki hula chakula cha asili kinachopatikana ndani ya maji. Vyakula hivyo ni pamoja na jamii ya mimea na vijidudu wanaopatikana kwenye maji. Lakini, samaki wa kufugwa hususan ufugaji wa kibiashara, huhitaji kulishwa chakula cha ziada chenye ubora iliyo na virutubisho vinavyohitajika ili aweze kukua vyema na kwa haraka zaidi. Uandaaji wa chakula cha ziada cha samaki hutegemea zaidi aina ya samaki, mfumo wa samaki husika katika kumeng’enya (kusaga) chakula pamoja na kiasi cha virutubisho vinachohitajika.