Usindikaji na Masoko
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Usindikaji na Masoko by Subject "Biashara"
Now showing 1 - 8 of 8
Results Per Page
Sort Options
Item Elimu ya Ujasiriamali: Kuelekea kwenye Maendeleo Endelevu Tanzania(Haki Elimu, 2021) Muhura, ChirakaNchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa mfano, zimejaliwa raslimali ambazo zinaweza kub- adilishwa kuwa mali. Lakini suala ni jinsi ya kuzigeuza raslimali hizo ili kuwa vitu halisi. Elimu isiyofaa imeelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha kuzibadilisha raslimali hizo kuwa vitu halisi. Elimu ya Tanzania inasemekana kuwa ni elimu inayowaandaa watu kuwa waajiriwa wa maofsini, japokuwa nafasi za kazi ni chache ukilinganisha na idadi ya watu wanaotafuta kazi za kuajiriwa. Kwa ufupi, elimu yetu haijengi ubunifu na udadisi ambao ungewawezesha watu ama kujiajiri (ujasiriamali) au kuzipanua fursa za ajira ambazo zingewawezesha watu wengi kupata ajira. Fursa za ajira hazijatumiwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuweza kuwachukua watu wote wenye sifa za kuajiriwa. Chapisho hili kwa hiyo linaibua jinsi elimu ya ujasiriamali inavyoweza kuibadilisha nchi kutoka kwenye utegemezi na kuwa nchi yenye kujitegemea.Item Hatua za utengenezaji wa juisi ya makakara kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011-11) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. B; Chove, BKipeperushi kinachoeleza jinsi ya usindikaji wa jiusi ya makakara - passion kwa ajili ya biashara.Item Kutunza kumbukumbu za biashara kwa wakufunzi na wasindikaji: Mradi wa kusindika kibiashara matunda na mbogamboga unaotekelezwa Tanzania na Rwanda(ASARECA, 2011-10) Tiisekwa, F. A; Kashindye, ABaada ya kusoma kijitabu hiki msomaji anatefgemewa kuweza: - Kutunza vizuri kumbukumbu na hati za biashara. - Kuujua umuhimu na thamani ya kumbukumbu za biashara. - Kuzitathmini benki na kuweza kuchagua akaunti ya benki inayofaa. - Kuambatisha gharama kwenye bidhaa na kupanga bei na mishahara ambavyo vitawasaidia katika uainishaji. - Kujua umuhimu wa orodha ya bidhaa na jinsi ya kuisimamia ili kupunguza gharama.Item MATATIZOYA MASOKO YA MAZAO YA WAKULIMA - Warsha ya Nne ya Wakulima wa Kanda ya Mashariki Iliyofanyika VETA Tanga 24-26 Juni 2002(TARP II-SUA Project, 2002-06) Razack, O. M; Lyimo-Macha, J. GChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD). Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na pia kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na ., washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo: 1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo 2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima wadogowadogo 3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi 4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo. Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima waKanda ya Mashariki Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa VETA, Tanga, tarehe 24-26 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Item Mbinu bora za kilimo kwa wakufunzi na wasindikaji(Idara ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia - SUA, 2011-02) Tiisekwa, B. P. M; Ndibakunze, B. K; Suleiman, R; Tiisekwa, A. BMatunda na mbogamboga ni mazao muhimu katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, kama yalivyo muhimu katika ulimwengu wote. Mazao haya ni chanzo cha vitamini, madini, antioxidants, kambakamba za chakula and wanga ambayo ni mahitaji muhimu ya mwili. Virutubisho hivi huongeza ubora wa chakula na huzuia binadamu kupata magonjwa sugu. Hata hivyo, matunda na mbogamboga huharibika kirahisi sana na hivyo hupoteza kwa haraka sana thamani yake ya lishe na ya kiuchumi. Makadirio ya upotevu wa matunda na mbogamboga baada ya mavuno katika nchi zinazoendelea ni asilimia 40%. Hii inamaanisha kuwa katika kipindi ambacho siyo cha mavuno, kaya hukabiliwa na upungufu wa matunda na mbogamboga kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa namna ya kuhifadhi na kusindika kwa ajili ya matumizi katika mwaka mzima. Matokeo ya muda mrefu ya hali hii ni uhaba wa bidhaa iliyosindikwa katika ngazi ya chini na kutokidhi mahitaji ya viwango vya ubora kwa masoko ya ndani na nje nchi. Changamoto hizi zimeisukuma ASARECA kuwekeza katika utafiti na maendeleo katika teknolojia za mazao freshi na kuongeza thamani na mapato yatokanayo na bidhaa hizo.Item Mwongozo wa Kikundi Kuhusu Mafunzo ya Kukuza na Kuendeleza Kilimo Biashara(Vi Agroforestry, 2016) Ruto, Grace; Odhong', CharlesMWONGOZO HUU UMEANDALIWA ILI KUWEZESHA KUWAFUNDISHA wakulima katika ukuzaji wa biashara, hivyo kuwezesha wakulima wanaofanya kilimo cha kujikimu kubadilisha kutoka kulima kwa ajili ya chakula cha familia tu hadi kilimo kama shughuli ya kibiashara. Mwongozo huu una lengo la kuwapa wakulima ujuzi, mtazamo, na ustadi unaohitajika kubadilisha na kukuza biashara zao kwa namna endelevu ili ziwe biashara za kilimo zenye mafanikio. Mwongozo huu unaangazia dhana za msingi kuhusu uwekezaji, kanuni za msingi kuhusu mnyororo wa thamani, huduma muhimu za ukuzaji wa biashara, namna ya kutumia soko kwa mafanikio, usimamizi wa fedha na ujuzi wa upangaji wa biashara ulio muhimu katika kufanikiwa kwa mjasiriamali anayejihusisha na kilimo biashara.Item Ni muhimu kuuza kwa pamoja: Faida ya soko la pamoja(Farm Radio International, 2014-09)Zao la muhogo limekuwa likifanyiwa biashara katika miji mbalimbali hapa Tanzania. Wanawake wafanya biashara wadogo wadogo wamekuwa wakiuza mihogo katika viunga mbalimbali vya miji katika foleni za magari na pia idadi ya watumiaji wanaonunua unga wa muhogo katika maduka mbalimbali inaongezeka. (Hiki ni kipindi kwa ajili ya wataarishaji wa Vipindi vya Redio)Item Ujasiriamali katika biashara Tanzania(2005) Makindara, J. RKijitabu kinazungumzia kwa ujumla mambo ya kuangalia katika ujasiriamali uanzishaji na uendeshaji wa biashara katika mazingira ya Tanzania