Matumizi Bora ya Ardhi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Matumizi Bora ya Ardhi by Subject "Hali ya hewa"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Jinsi wakulima hukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa(Farm Radio International - FRI, 2009-12)Kujifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu kwa wakulima kwa sababu ya athari wanayoweza kuwa nayo kwenye kilimo. Wakulima wanaweza kutarajia kiasi cha joto kilichopanda na dhoruba za mara kwa mara, mafuriko na hali za ukame. Hali ya hewa itakuwa inabadilikabadilika zaidi na hivyo ngumu kutabiri. Wakulima wanahitaji kuelewa mabadiliko ya hali ya hewa na anga ili kufanya mipango kuhusu mavuno yanayobadilika na tofauti, ukosefu wa maji, na uwezekano wa ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa. Makala haya yanatoa habari msingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakayokusaidia kutayarisha vipindi vya redio kuhusu mada hii. Unavweza kuwaambia wakulima katika eneo lako kuhusu njia kadhaa ambazo kwazo, mabadiliko ya hewa huwaathiri wakulima. Kisha unaweza kujadili mikakati ambayo wakulima wa eneo hilo wanaweza kutumia ili kufanikiwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ongea na wakulima ili uelewe changamoto yao imekuwa nini kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa. Je, wamepata njia mpya, au kutumia njia za jadi zinazowasaidia kukabiliana na hali hii mpya.Item Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira(Afrika Kontakt, 2017)La Via Campesina na Afrika Kontakt tunakiri kuwa tuko nyuma sana katika kukabiliana na tatizo linalotukabili la mabadiliko ya tabianchi. Sehemu kubwa ya tatizo bado haijatatuliwa, ambayo ni mifumo yetu ya kiulimwengu ya masuala ya kijamii na kiuchumi inayosababisha mabadiliko ya tabianchi. Kwahiyo, lazima tupambane kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inabadilishwa. Zaidi ya hapo, tunatakiwa kushiriki katika mchakato mzima wa kutafuta njia na mikakati mbadala ya kuleta mabadiliko halisi. Wakati wa mkutano wa Mazingira wa Paris yaani COP21, wanaharakati wa masuala ya tabianchi walikuwa wakipaza sauti zao kuhusu mabadiliko ya mfumo, na siyo mabadiliko ya tabianchi. Wengi wa wanaharakati hao hapo awali walikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Wanaharakati hao huliona suala la mabadiliko ya tabianchi kama jambo halisi na ambalo hutokea kila siku. Kwa mujibu wa maelezo yao, hatutakiwi kuwasubiri wanasiasa kuchukua hatua, na badala yake wamekuwa wakichukua hatua ambazo kwa bahati mbaya zimekuwa zikipuuzwa na wanasiasa wengi na watunga sera au wamekuwa wakidharauliwa na mfumo. Lengo la kitabu hiki cha mwongozo ni kuonyesha athari za mabadiliko ya tabianchi zinazowakabili wakulima wadogo, lakini pia kugusia suluhisho ambazo wanaweza kuzitumia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia maarifa ya wakulima wadogo kutoka Uganda, Tanzania, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, na Msumbiji. Kutokana na ukweli kuwa jamii za zilizoko katika nchi hizo wanategemea sana mazingira asilia na maliasili zake, wamekuwa wahanga wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi. Lakini uhusiano wao wa karibu na mazingira umewesha uwepo wa maarifa kutoka kizazi kimoja hadi kingine ambayo yanatumika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi. Hali iliyopo sasa kwenye majadiliano ya kimataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na madhara makubwa ya mabadiliko ya tabianchi vinahitaji kuchukuliwa hatua za dharura. Kwa sasa tunaelewa fika kuwa mfumo wa uzalishaji uliosababisha mabadiliko ya tabianchi hauwezi kutumika kukabiliana na tatizo ambalo wenyewe ulisababisha. Badala yake tunatakiwa kufungua macho yetu ili tuweze kutambua njia zilizopo na tuweze kuziendeleza na kuzitanua ili zisaidie katika mapambano. Hili linajumuisha mabadiliko kwenye mfumo wa uzalishaji wa dunia nzima.Item Nguvu kazi, mitizamo juu ya hali ya hewa na udongo kwenye maeneo ya umwagiliaji yaliyopo Siipow nchini Kenya na Engaruka nchini Tanzania(Department of Human Geography - University of Stockholm, 2015) Caretta, Martina A.; Westerberg, Lars-Ove; Borjeson, Lowe; Ostberg, WilhemKijitabu hiki kinatoa matokeo ya mradi wa miaka 4 (2011-2015) yaliyofanywa na wanajiografia wanne kutoka chuo kikuu cha Stockholm. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vidogo viwili, ambavyo ni Siipow nchini Kenya na Engaruka nchiniTanzania. Kwa ujumla mradi huu uliangalia vitu vikuu vitatu: udongo, hali ya hewa na nguvu kazi. Mambo haya makuu yanaweza kuonyesha aina ya mabadiliko yaliyowahi kujitokeza katika mifumo ya umwagiliaji katika maeneo haya na sababu mahususi zilizosababisha mabadiliko hayo. Katika kijitabu hiki matokeo ya utafiti yameonyeshwa kufuatana na maeneo ya utafiti na hususani: mbinu za kilimo, mgawanyo wa majukumu ya kazi kwa wanawake na wanaume, sifa za udongo na maji, mabadiliko ya hali ya hewa na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na jinsi ambavyo mambo haya yote kwa ujumla yamekuwa yakibadilika kadri muda unavyokwenda.