Matumizi Bora ya Ardhi
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Matumizi Bora ya Ardhi by Subject "Ardhi"
Now showing 1 - 11 of 11
Results Per Page
Sort Options
Item Ijue sheria ya ardhi na taratibu zinazohusika kupata, kumiliki na kuuza ardhi vijijini na mjini, Sheria Katika Lugha Rahisi(Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara, 2015-06)Chama Cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) ni chama kilichoanziahwa na Sheria ya Bunge ya 1954 Sura Na.307. Kwa mujibu wa sheria hiyo, Chama kinawajibu wa kuisaidia serikali katik amasuala yahusuyo sheria na pia kuieleimisha jamii kisheria katika kupata haki zao za msingi. Katika kutimiza jukumu lake kwa wanajamii Cham Cha Sheria Tnaganyika kimeeandaa kijarida hiki cha sheria katika lugha Rahisi kiitwacho “IJUE SHERIA YA ARDHI NA TARATIBU ZINAZOHUSIKA KUPATA, KUMILIKI NA KUUZA ARDHI VIJIJINI NA MJINI’’.Item Jinsia na haki kuhusu Ardhi(FAO, 2017) Lukalo, F; Dokhe, EKwa zaidi ya miaka miwili baada ya kuzinduliwa kwa Tume ya Kitaifa ya Ardhi Februari 2013, hatua nyingi zimepigwa za kuboresha usimamizi wa ardhi nchini Kenya. Kuchapisha kitabu hiki ni ufanisi unaohitaji kusherehekea kwa sheria na kanuni mbalimbali ilizobuniwa katika kuzindua katiba ya Kenya inayolenga marekebisho katika sekta ya ardhi ambayo yamewekwa kukidhi mahitaji ya usawa wa jinsia katika masuala ya ardhi. Katiba mpya ndiyo kilele cha ongezeko la hatua zilizopigwa na nchi ili kuinua hadhi ya wanawake na maslahi yao katika ardhi. Katiba mpya inawakilisha hatua kubwa zilizopigwa kuboresha hadhi za wanaume na wanawake katika nyanja zote za maisha. Kwa sababu hiyo pana haja ya kuzingatia ufafanuzi wa ardhi kwa upana (maji na nafasi iliyopo) kama rasilimali asilia na mali nyingine inayopatikana katika ardhi. Ardhi na mali nyingine (kama mifugo, madini yanayochimbuliwa, mashine na kadhalika.) inaweza kutumika kwa kilimo na uzalishaji na vile vile inaweza kuwa chanzo cha uwezeshwaji wa kisiasa miongoni mwa wanawake. Kuwa na uwezo wa kupata ardhi na mali kunatoa nafasi ya makazi na kuwawezesha wanawake kujiunga katika ushindani wa siasa kuhusu rasiliamali; ardhi ni mali inayostahili kujumuishwa katika ndoa na inaweza kutumika kama chombo cha kupata mikopo.Item Kujenga picha ya jamii yetu kwa siku zijazo: sababu na jinsi ya kushiriki kupanga matumizi ya ardhi - Sura ya Pilii(2010)Wote tunaiona wazi: watu wameongezeka, miji imekua, mifugo imeongezeka, mashamba mengi zaidi .... Vilevile uharibifu zaidi wa ardhi, uharibifu wa misitu, mmomonyoko wa udongo .... Migogoro mingi zaidi kati ya wakulima na wafugaji, wachimba madini na wafugaji, wanyamapori na watu .... Mahitaji yetu ya kutumia ardhi yanaongezeka wakati wote, lakini eneo la ardhi haliongezeki. Tutafanyaje ili tuwe na matumizi mazuri na ya kuridhisha ya ardhi tuliyonayo, katika mazingira ya hali ya tabianchi na maliasili, pamoja na tamaduni zetu, njia tunazotumia kumudu maisha, matarajio na ndoto za jamii yetu? Kujibu swali hili ndilo lengo la kupanga matumizi ya ardhi. Na kwa sababu ardhi ni ya msingi kwa jamii, mpango wa matumizi ya ardhi unakuwa bora pale tu jamii inaposhiriki kikamilifu kwenye mchakato. Hapo ndipo linapokamilika suala la “ushirikishwaji” kwenye mpango shirikishi wa matumizi ya ardhi, yaani LUP.Item MATUMIZI BORA YA ARDHI- Mafunzo kutoka Mlima Meru(Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania - TARP II - SUA Project), 2002-09) Lyimo-Macha, J. G; Malimbwi, R. E; Kiranga, E; Kawamala, PChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo Wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Wagani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha mafunzo yatokanayo na ziara iliyofanyika Septemba 2002. Ziara hii iliwashirikisha wakulima na washauri wa wakulima kutoka Kanda ya Mashariki ikijumuisha wilaya za Kilosa, Handeni, Pangani, Mkuranga na Morogoro na kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwajumuisha wakulima na wagani kutoka wilaya za Mbeya, Mafinga, Njombe, Mbinga na Mbozi ambao walitembelea wakulima wa wilaya ya Arumeru, Arusha walioshiriki katika rnradi wa SCAPA. Makala hii pia inapatikana katika lugha ya kiingereza.Item Matumizi bora ya mbolea ya Minjingu kwenye kilimo cha mboga(Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Mikocheni & Kituo cha Ut afiti wa M azao Uyole, 2003)Kipeperushi kinachoelezea mbolea ya Minjingu kama ni mbolea asilia ya kupandia. Mbolea hii inatokana na miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu mkoani Manyara ambayo husagwa na kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu ina kirutubisho cha mimea aina ya fosiforasi kati ya asilimia 12.3-13.2. Tofauti na mbolea nyingine za kupandia zenye madini ya fosiforasi kama vile TSP na DAP ambazo huagizwa nje ya nchi hivyo kugharimu fedha nyingi za kigeni, mbolea hii inayopatikana hapa nchini bei yake ni nafuu.Item Mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji: Mbinu ya mapinduzi ya kijani wilayani Mbarali, Mbeya(EcoAgriculture, 2014-10)Nchini Tanzania, mpango wa matumizi bora ya ardhi vijijini ulirasimishwa miaka ya hivi karibuni ikiwa ni moja ya mikakati katika mchakato wa kuleta maendeleo endelevu vijijini. Utekelezaji wa mpango huu hauna budi kuwa mikononi mwa wanavijiji wenyewe kwa kiasi kikubwa katika kugawa ardhi yao kwa matumizi mbalimbali ya kujikimu kimaisha kwa sasa na siku za baadaye na kuwa na uhifadhi endelevu wa mazingira. Maendeleo endelevu katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya yanaathiriwa na migogoro ya matumizi ya rasilimali ardhi na maji kwa muda mrefu sasa. Hii imetokana na uwezo wa ardhi kupungua kutoa mavuno ya kutosha na uhaba wa maji kwa matumizi mbalimbali hususan umwagiliaji, unyweshaji mifugo, uendelevu wa miminiko la maji kwenye bwawa la umeme, uhifadhi ya bionuai na mazingira. Mpango wa matumizi bora ya ardhi vijijini unasaidia kusimamia na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi, maji na hifadhi ya mazingira.Item Mwongozo wa mafunzo ya kilimo hai Afrika: Usimamizi wa rutuba ya udongo(FIBL, 2012)Wasiwasi unatanda kuhusu uendelevu wa muda mrefu wa sekta ya kilimo. Ardhi yenye rutuba na maji ya kutosha ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza kilimo na kaya. Hata hivyo, katika bara la Afrika uzalishaji unaotokana na ardhi umekuwa ukiendelea kupungua kutokana na shughuli za kilimo kilichoshadidi zinazosababisha uharibifu wa ardhi. Sababu kubwa za uharibifu wa ardhi ni taratibu za kilimo zisizokuwa endelevu kama vile kulima kwenye miteremko mikali bila ya kuchukua hatua za kuhifadhi udongo na maji, kulima zao la aina moja tu, utifuaji wa ardhi uliopitiliza, kupungua kwa mazoea ya kupumzisha ardhi bila ya kuchukua hatua stahiki za kurudishia virutubisho vya ardhi, kuchoma mabaki ya mazao, kugeuza misitu na vichaka kuwa maeneo ya kilimo cha kudumu, au matumizi yaliyopitiliza ya misitu kwa ajili ya kuvuna kuni na mbao, mifugo mingi katika eneo dogo la malisho, na kutokuwepo kwa udhibiti imara wa mboji kwenye udongo.Item Nakala juu ya rutuba ya udongo(Farm Radio International - FRI, 2016)Rutuba ya ugongoimefafanuliawa kama “uwezo wa udongo kusambaza idadi ya kutosha ya virutubisho muhimu na maji yanayohitajika kwa ajili ya ukuaji wa mimea maalum ikiongozwa na vigezo vya kemikali, maumbile, kibaiologia kwenye udongo.” Kilimo ni chanzo kikuu cha chakula na kipato kwa idadi kubwa ya wakazi wa nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara. Udongo ambao hauna rutuba nzuri ni kikwazo kikuu cha kuongeza uzalishaji wa chakula, lishe na vyakula vya nyuzi nyuzi. Kuna uhaba wa matumizi ya pembejeo za kilimo kusini mwa jangwa la Sahara. Ongezeko wa watu unasababisha kupungua kwa ukubwa wa ardhi, na kwa kuwa kuna upungufu wa ardhi yenye rutuba kuna umuhimu wa kufuata taratibu za sayansi ya udongo na uzalishaji mazao.Item Uchoraji Shirikishi wa Ramani ya Rasilimali za Nyanda za Malisho nchini Tanzania: Mwongozo wa Uwandani wa kusaidia Kupanga Mpango na Usimamizi wa Nyanda za Malisho ikiwemo Kupanga Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji(Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Tanzania, 2016)Mifugo ni sehemu muhimu katika uchumi wa vijijini nchini Tanzania. Mifugo si kwamba hutoa nyama na maziwa, lakini pia hutoa ngozi, nguvu kazi na mbolea. Mifugo inatoa mchango muhimu katika bidhaa zinazouzwa nje na Pato Ghafi la Taifa la Tanzania. Mifugo inashika nafasi ya pili ndani ya sekta ya kilimo katika kuchangia Pato Ghafi la Taifa (hii ni karibia asilimia 13 ya Pato Ghafi la Kilimo la Taifa). Hiki ni kiwango kidogo licha ya kuwa na idadi kubwa ya mifugo. Hii inasemekana ni kutokana na kuwepo kwa magonjwa, ambayo yamekuwa kikwazo kwa usafirishaji wa wanyama nje ya nchi. Sekta hii pia inakabiliwa na matatizo ya kutoendana na mahitaji ya soko jipya kama vile Mfumo wa Ubainishaji na Ufuatiliaji wa Mifugo na ustawi wa wanyama. Zaidi ya hayo, upelekaji wa mifugo kati ya masoko madogo na makubwa unaongeza utegemezi wa usafirishaji kwa njia ya reli au barabara ukichangia thamani kubwa ya ardhi kwa ajili ya nyama au mifugo kama ukilinganisha na ilivyo Mashariki ya Kati, hivyo kuifanya kuwa na ushindani mdogoItem Udongo na umuhimu wa kupima udongo(Kilimo Tanzania Blog, 2018-07) Mussa, DLeo tunakwenda kujifunza kuhusu Udongo, aina za udongo, virutubisho vilivyopo kwenye udongo pamoja na upimaji wa udongo. Udongo ni nini? Udongo ni tabaka juu ya ardhi ambalo hufanya kazi kama chombo cha kukuzia mimea. Udongo hujengwa kutokana na shughuli zinazoendelea za hali ya hewa kulingana na vipengele kadhaa vya mazingira. Kwa sehemu kubwa kuundwa kwa udongo hutawaliwa na vipengele vikuu vitano: hali ya nchi (k.m. mvua, joto na upepo), mwinuko wa eneo (mahali eneo lilipo), viumbe hai (mimea na vijidudu), asili ya kitu kilichozalisha udongo (aina ya miamba na madini ambayo udongo unatokananayo) na muda.Item Usimamizi endelevu wa ardhi ya kilimo(Vi Agroforestry, 2015) Wekesa, Amos; Jönsson, MadeleineMABADILIKO YA TABIA NCHI na hali ya hewa isiyotabilika kwa pamoja huchangia changamoto kubwa kwa wakulima wadogo wadogo katika eneo la Afrika Mashariki.Vi Agroforestry inafanya kazi na wakulima pamoja na asasi za wakulima kuongeza ufahamu wao wa mazingira, kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza matumizi ya nishati mbadala/endelevu na pia kuzuia na kupunguza athari za majanga asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.Usimamizi Endelevu wa Ardhi ya Kilimo (SALM) ni mbinu zinazotumiwa na wakulima katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza tija katika uzalishaji kwenye kanda mbalimbali za kilimo ikolojia. Mbinu hizi pia zinaweza kutumiwa katika maeneo ya mijini kwa mfano bustani za mbogamboga, mbinu zinazohusu ukulima, nishati mbadala na usimamizi wa maji na maji taka. Mwongozo huu umeweka mbinu mbalimbali ambazo mkulima anaweza kuzitumia kama hatua ya kweli katika kuongeza tija na faida hata kwa vizazi vijavyo hasa kutokana na ufahamu wa hali ya hewa na tabia ya nchi inayobadilika duniani kote na kuathiri uzalishaji wa tija