Uzalishaji Mazao
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Uzalishaji Mazao by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 514
Results Per Page
Sort Options
Item KILIMO CHA MTAMA(20-03-13) KILIMO BLOGMtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika kujengaea uwa .Item Halmashauri ya taifa ya mazao(Nuta Press, 1971) wizara ya kilimoKabla ya Tanzania kupata uhuru, serikaii ya kikoloni ilijiingiza sana katika mazao ya biashara na nchi za nje na haikujali sanajuu ya mazao yaliyotumika humu nchini hasa yale ya chakula ambayo wananchi hutumia. Siasa yao ya kikoloni wakati huo ilikuwa kuku- za mazao ambayo yangeuzwa na kukuza uchumi wa nchi zao. Siasa hiyo kwa kweli iliweza kuleta madhara kwa mazao ambayo yangetumika au kuliwa humu nchini, kwa hiyo upanuzi wa kilimo cha mazao machache kuliifanya Tanganyika kutesemea mazao kama katani na kahawa kuwa mazao makuu ya biashara na nchi za nje.Item Tomato disease control(NEW-MEXICO STATE UNIVERSITY COOPERATIVE EXTENSION SERVICE., 1971-08) Shannon, EmroyTomatoes are attacked by several disease organisms that reduce both yield and quality. Control of these diseases means the difference between profit and loss. Effective control consists of knowing what diseases you have and implementing an effective control program.Item Grasshopper control(Washington, D.C., 1973-05-08) Western Region, Agricultural Research ServiceGrasshoppers are found in every part of the United States, but serious outbreaks seldom develop east of the Mississippi River; they occur mostly in the western two-thirds of the country. Grasshoppers often severely damage range grasses. They also contribute to soil erosion and "dustbowl" conditions. Their feeding is one of the principal reasons for loss of productive grasslands in many of the Western States. Many cultivated crops are also damaged by grasshoppers. When range grass is scarce and outbreaks are severe, grasshoppers often migrate into and severely damage the foliage of alfalfa, clover, corn, small grains, tobacco, sugarbeets, cotton, lettuce, potatoes, and fruit trees. In fruit orchards, grasshoppers sometimes completely strip the leaves and may kill young trees. You can control grasshoppers by applying insecticides. If your farming practices will permit, cultural measures can be used to help keep grasshoppers in check.Item Controlling Diseases of Raspberries and Blackberries(U.S. DEPARTMENT OF AGRICULTURE., 1975-04-30) Agriculture, U.S. departmentThe most effective control measures for raspberry and blackberry diseases are those taken before the diseases become serious. Varieties adapted to a locality and resistant to the major diseases should be planted, if available. Plants certified as being substantially disease free by a State plant inspection service should be used. Cultural practices that promote vigorous growth are also important in growing healthy raspberries and blackberries.Item Siasa ya Tanu katika Kilimo.(Afisa kilimo msaidizi ofisi yakilimo Tanu., 1977) Kimiti, P.PTANU ya sasa ina kazi kubwa sana, maana TANU inafanya kazi ya kuelimisha, kueleza na kujcnga Taifa letu ili litoke katika hali ya unyongc na kuwa katika hali ya neema na nguvu. Kania sote tunavyoelcwa ni kwamba katika kuwaongoza wananchi. ni budi kwanza tuwasikilize, tushirikiane nao na tufanye kazi pamoja nao. Uhusiano uliopo kati ya Serikali na chama cha TANU ni mkubwa. J ambo la kukumbukwa ni kwamba chama siyo chombo cha Serikali, bali ni Serikali ambayo ndiyo chombo kinachotumiwa na chama katika kutekeleza matakwa yo vote ya wananchi ambao sisi sote tunawatumikia. Hii ndiyo maana tunasema kuwa chama kina wajibu mkubwa wa kufanya, katika kufikiria misingi ambayo baada ya kuwekwa kwa uwazi, ni budi Serikali ifuate na kutekeleza. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ni sehemu ya Serikali. Hivyo Wizara hii ina wajibu mkubwa sana katika kuitekeleza siasa ya TANU ambayo ndiyo inayoongoza Serikali.Item Korosho(Wizara ya kilimo, 1983) Mradi wa mafunzo ya wakulimaUzalishaji wa korosho duniani umekua ukiongezeka kila mwaka kutokana na jitihada zinazoendelea katika nchi mbalimbali kufanya upanuzi wa maeneo ya kilimo cha korosho, pamoja na matumizi ya teknolojiaka- ma vile matumizi ya mbegu bora. Aidha, katika bara la Afrika kumekuwa na jitihada za kuongeza ubanguaji wa korosho pamoja na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na korosho.Item Karanga(Sokoine university of agriculture, 1987) wizara ya kilimoKaranga ni zao zuri sana ambalo hutumika kama chakula na mafuta pia,karanga hupandwa sehemu tofauti nchini Tanzania.karanga hupandwa kwa kufuata kanuni zifuatazo kabla ya kupanda, chagua mbegu ambazo hazishambuliwi na wadudu au magonjwa, ondoa mbegu zilizo sinyaa na kutupa mbali kabla ya kupanda.Item Kanuni za kilimo bora cha minazi(Dar Es Salaam University Press, 1992) National Coconut Development ProgrammeIli kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda. Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa. Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda.Item Utengenezaji na matumizi ya mboleavunde katika kilimo.(Tanzania Educational Publishers Ltd, 1992) Ngeze, Pius BMimca inapokuwa shambani hufyonza virutubisho vya mimea kutokaudongoni. Kali ya virutubisho hivyo, vilivyo muhimu zaidi ni nitrojeni, fosforasi, potasi, kalisi na feri. Mimea hutumia virutubisho hivyo kwa kukua, kuzaa, kujiimarisha na kupevusha matunda ili kutupatia mavuno yaliyo mengi na bora. Karibu sehemu zote za mimea zina virutubisho. Sehemu hizo ni mizizi, mashina,majani, maua na matunda. Lakini, si sehemu zote hizo hutumiwa na binadamu kwa chakula. Kwa kawaida sehemu zinazotumiwa ni maua, majani, mbegu matunda au tyuba. Hata hivyo, sehemu halisi inayotumika hutegemea aina ya zao au mmea. Sehemu zinazobaki ambazo hazitumiwi na binadamu au mifugo kwa chakula hubaki na virutubisho hivyo. Iwapo sehemu kama hizo zitaachwa ziharibike ovyo huko shambani, au kuzichoma moto, hasa nje ya shamba, aina hizo za vyakula zitapotea bure bila kuwafaidia wakulima wala taifa. Njia ya kuhakikisha kwamba masalia hayo ya mimea yanawafaidia wakulima ni kuyarudisha udongoni. Njia iliyo bora ya kufanya hivyo ni kuyaozesha masalia ya mimea na kuyatumia kutengeneza mboleavunde. Vivyo hivyo kwa masalia ya wanyama (hasa mifugo). Wanyama hula mimea. Kiasi cha chakula hicho hutumiwa na wanyama hao kwa kukua, kuzaa, kufanya kazi na kuishi. Kiasi kilichobaki hutolewa nje kama kinyesi. Kinyesi hicho kina virutubisho muhimu vya mimea. Njia nzuri ya kutumia kinyesi hicho cha mifugo ni kukitumia kutengeneza samadi na mboleavunde na kuziweka udongoni ili kustawisha mazao. Kufanya hivyo ni kudumisha uhai wa udongo na viumbehai vingine.Item Mafunzo ya kilimo(Sokoine university of agriculture, 1994) Inades Formation TnzaniaKaranga ni moja ya mazao ambayo yana kiasi kikubwa cha mafuta hadi kufikia asilimia 30.Punje ya karanga pia ina kiasi kikubwa cha protini hadi kufikia asilimia 44.Hivyo karanga zinaweza kutoa hivi viini lishe mbalimbali.Faida nyingine ni kwamba karanga pia huongeza rutuba ya udongo na majani yake hutumika kulishia mifugo.Item Utafiti wa binadamu na mazingira mikoa ya kati Tanzania(UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, 1994-05-23) Ostberg, WilhelmMpango wa utafiti wa Binadamu na Mazingira Mikoa ya Kati Tanzania unaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Institute of Resource Assessment (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es-salaam, nchini Tanzania, na Environment and Development Studies Unit (EDSU), School of Geography, Stockholm University, Sweden. Watafiti wapatao kurni na tano kutoka nyanja mbalimbali wanahusika na utafiti huu. Vyuo hivyo viwili vinashirikiana katika rnipango mbalimbali ya kuandaa na kutekeleza shughuli za utafiti. Mpango huu unaratibiwa na Mkurugenzi wa IRA, Profesa Idris Kikula na Mkuu wa kitengo cha EDSU, Profesa Carl Christiansson. Fedha kwa ajili ya mpango huu zimetolewa na the Swedish Agency for Research Cooperation with the Developing Countries, SAREC. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kutumika na idara mbalimbali za serikali na mashirika ya umma,miradi ya Hifadhi Ardhi na Mazingira na mashirika mbalimbali ya kimataifa yaliyo katika rnikoa hiyo. Wakati huo huo matokeo ya utafiti huo yatasaidia katika kuelewa hali halisi ya mazingira na maturnizi ya ardhi katika rnikoa inayohusika. Makala haya yana taarifa ya utafiti uliofanyika katika kuchangia mpango huo. Orodha ya makala mengine yanayohusiana na mpango huo wa utafiti yanapatikana kutoka Institute of Resource Assessment, Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, S.L.P.35097, Dar es-salaam au kutoka the Environment and Development Studies, School of Geography, Stockholm University, S-106 91 Stockholm, Sweden.Item Maana ya maendeleo ni nini? Mfano wa Mafia, Tanzania(Changia Maendeleo Mafia - CHAMAMA, 1994-08)Hotuba hii imetolewa tarehe 1 Agosti 1994 Lizu Hotel, Kilindoni, Mafia na Professor Patricia Caplan, BA, MA, Ph.D.Goldsmiths College, University of London ambaye alisema Naona nimepewa heshima kubwa kuweza kupata nafasi ya kuwahutubia watu wengi kama hivi wakiwa na nyadhifa tofauti, leo hii. Pamoja na kunipatia nafasi hii, mimi bado napata wasiwasi kidogo kuongelea maendeleo ya Mafia hasa mimi nikiwa si Mtanzania. Isitoshe, watu wengi wa Mafia wameniita inara nyingi mimi mwenyeji. Nashukuru kw a heshima hiyo tukufu. Heshima hiyo, pia, imenif anya mpaka mimi nione Mafia kama mji w angu w a pili, ambao imejaa w azazi w angu, ndugu zangu, dada zangu, kaka zangu, akina babu na bibi zangu, na marafiki zangu. Miaka 29 iliyopita tangu nifike Mafia mwaka sitini na tano, nimew eza kujif unza mambo mengi, na w atu w amekuw a tayari kunif undisha mambo mengi, lakini kila mara, naona bado yapo mengi ya kujifunza na kwamba nahitaji muda zaidi. Na huenda, kw a bahati mbaya, mengine sikuyajua vizuri, nadhani mtanis amehe. Nimeamua kuzungumza kw a Kisw ahili na nadhani mtakubaliana nami kuw a Kisw ahili changu si kizuri sana lakini mtakuw a radhi kunivumilia na kunisikiliza. Baada ya hayo, machache, naomba sasa tuingie katika maada maalum nitakayoizungumzia leo hii.Item Mbinu bora za kupunguza mashambulizi ya wadudu kwenye viazi vitamu(Kituo cha utafiti wa kilimo Ukiriguru, 1995) Braun, MViazi vitamu ni mojawapo ya vyakula ambavyo hutumika sana nchini, watu wengi hutumia kama kitafunwa cha asubuhi,Pia wengine hutumia kama chakula ambapo hupikwa kama mlo wa kawaida wakati wa mchana au usiku.Hivyo basi kuna tofauti ya kuviandaa, unaweza kukaanga au kuchemsha pia.Item Kilimo cha bustani(Sokoine University of Agriculture, 1996) Maerere, A.PUTANGULIZI Kilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo. Kilimo cha bustani ni chanzo cha ajira na pato kwa wakulima na watu wengine. Mboga na matunda yanatupatia virutubisho vya kujenga, kutia nguvu na kulinda mwili. Zaidi ya hivyo, mimea ya mapambo hutumika katika kuremba na kuboresha sehemu za makazi, majengo, barabara na sehemu zingine za wazi za jumuia. Hii ni muhimu sana katika swala zima la kuhifadhi mazingira. Pamoja na umuhimu huo, kilimo cha bustani hakijazingatiwa sana hapa nchini hasa katika kueneza taaluma yake. Siku zote kipaumbele kimekuwa kikiwekwa katika kuhimiza kilimo bora cha mazao ya asili ya biashara na ya chakula kama nafaka. Jarida hili limetokana na juhudi za mradi wa SUA-TU katika kueneza taaluma ya kilimo cha bustani katika vijiji vya mkoa wa Morogoro. Katika baadhi ya vijiji hapa mkoani, taaluma hii ilikuwa ni ngeni kabisa mradi ulipoanzishwa hapo mwaka 1996. Kwa ujumla jarida hili linajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa wakulima wa vijiji vya Changa, Msongozi, Maharaka (Morogoro vijijini), Katurukila (Kilombero), Kitange I, Kwipapa, Malui na Tindiga (Kilosa). Sehemu yake ya kwanza ni juu ya uzalishaji wa miche ya mboga na matunda katika kitalu na utunzaji wake. Sehemu ya pili na ya tatu zinajihusisha na kilimo cha mboga ikiwa ni pamoja na uyoga. Sehemu ya mwisho ni juu ya masoko na uuzaji wa mboga na matunda, swala ambalo ni muhimu katika kumfanya mkulima afaidike na juhudi zake baada ya kuzalisha. Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wakulima wote walioshirikiana na wataalamu wa mradi wa SUA-TU na pia shirika la USAID la Marekani ambalo ndilo lilikuwa mfadhili mkuu wa mradiItem Kilimo cha bustani - Mafunzo kwa wakulima(SUA - TU linkage Project, 1997) Maerere, A. P; Kusolwa, P. M; Msogoya, T. S; Mgembe, E. R; Msita, H. B; Turuka, F. M; Senkondo, F. JKilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo. Kilimo cha bustani ni chanzo cha ajira na pato kwa wakulima na watu wengine. Mboga na matunda yanatupatia virutubisho vya kujenga, kutia nguvu na kulinda mwili. Zaidi ya hivyo, mimea ya mapambo hutumika katika kuremba na kuboresha sehemu za makazi, majengo, barabara na sehemu zingine za wazi za jumuia. Hii ni muhimu sana katika swala zima la kuhifadhi mazingira. Pamoja na umuhimu huo, kilimo cha bustani hakijazingatiwa sana hapa nchini hasa katika kueneza taaluma yake. Siku zote kipaumbele kimekuwa kikiwekwa katika kuhimiza kilimo bora cha mazao ya asili ya biashara na ya chakula kama nafaka. Jarida hili limetokana na juhudi za mradi wa SUA-TU katika kueneza taaluma ya kilimo cha bustani katika vijiji vya mkoa wa Morogoro. Katika baadhi ya vijiji hapa mkoani, taaluma hii ilikuwa ni ngeni kabisa mradi ulipoanzishwa hapo mwaka 1996. Kwa ujumla jarida hili linajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa wakulima wa vijiji vya Changa, Msongozi, Maharaka (Morogoro vijijini), Katurukila (Kilombero), Kitange I, Kwipapa, Malui na Tindiga (Kilosa). Sehemu yake ya kwanza ni juu ya uzalishaji wa miche ya mboga na matunda katika kitalu na utunzaji wake. Sehemu ya pili na ya tatu zinajihusisha na kilimo cha mboga ikiwa ni pamoja na uyoga. Sehemu ya mwisho ni juu ya masoko na uuzaji wa mboga na matunda, swala ambalo ni muhimu katika kumfanya mkulima afaidike na juhudi zake baada ya kuzalisha. Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wakulima wote walioshirikiana na wataalamu wa mradi wa SUA-TU na pia shirika la USAID la Marekani ambalo ndilo lilikuwa mfadhili mkuu wa mradi.Item Jinsi ya kulima mgagani: kilimo bora cha mgagani(Melkisedeki, 1998) Melkisedeki, MelkisedekiMigagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku. Mgagani wa kawaida, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu. Mboga ya mgagani huitwa magagani.Item Kilimo cha pamba Tanzania(kiwanda cha uchapaji cha taifa, 1999) Idara ya uhusiano na elimu a wakulima mamlaka ya pamba TanzaniaPAMBA ni zao ambalo hustawi vizuri sana katika sehemu kubwa ya nchi yetu. Pamba hustawi katika udongo wa aina mbali mbali mradi tu maji yawe yanapenya kwa urahisi na usiwe na chachu (acidic) kwa wingi. Kiasi cha inchi ishirini za mvua hustawisha pamba vema, kama ikinyesha kwa mpango mzuri. Mwinuko wa kuanzia usawa wa bahari hadi futi 4,500 kutoka usawa wa bahari ndiyo hasa hufaa kwa ustawishaji wa pamba.Item Questions and answers concerning the National agricultural product board = Maswali na majibu kuhusu Hali mashauri ya Taifa ya mazao(Halmashauri ya Taifa ya Mazao, 1999) Halmashauri ya Taifa ya MazaoThe aim of this pamphlet is to supplement our earlier ones like the “Official Handbook” and “Halmashauri ya Taifa Isimamiayo Mazao” in making the citizens of this country more informed about their National Agricultural Products Board. It is particularly intended to be read by leaders of this nation so that after acquiring better understanding of the Board, its functions and ideals they are in a better position to educate the people through out the country and clear up some of the misinformation, or lack of information, about the Board whose activities so affect their daily lives. We have based our ansivers on die questions that have been asked, or are likely to be asked, by the public through the contacts we have established with them — newspapers, broadcasts or visits by Board Representatives to the Regions. We however realize that even with these it is difficult to reach every one in die country — so we ask you the reader of this pamphlet to assist us, and the nation generally, wherever you go by explaining what you have read to the people you come across.Item Kilimo bora cha mpunga wa umwagiliaji(2000)Maandalizi sahihi ya shamba ni jambo la msingi katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu bora zinazoshauriwa kutoonyesha matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika uzalishaji. Kimsingi maandalizi ya shamba yanatakiwa yafanyike kwa usahihi na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa.